Nini tunahitaji kwanza? - (tazama picha na amua)

Hizi ni picha za jana baada ya mvua kunyesha katikati ya Dar (picha kwa hisani ya MICHUZI JR

mafuriko.jpg
mafuriko2.jpg

mafuriko3.jpg
mafuriko4.jpg

..."mind the Gap" baina ya hizo crates na uwezo wa kuruka hao mabibi na mabwana ndipo utapogundua upeo wa akili za walengwa, na huyo kijana aliyejipatia 'ajira' ya chap chap...

BTW, Huyu mheshimiwa (mkanda nje na skuna zake) 'unadhani' aliruka salama bila kuyakanyaga hayo maji??? NEVER...

Hata serikali ikijenga miundo mbinu, ikiwemo better sewerage, bado wananchi hao hao watavitupa hovyo vifuko vya plastiki nk na tatizo kujirudia pale pale...

Tubadilike!!!

1672.jpg

maji.JPG
 
Tunachohitaji ni aina fulani hivi ya dikteta (kama kuna aina), mpenda maendeleo, anayejali haki za binadamu, mwenye uchungu na nchi yake na mwenye maono....mimi naamini kabisa kuwa katika kipindi cha miaka 10 akitokea mtu wa namna hiyo, nchi inaweza kubadilika in a good way nakuwa nchi yenye matumaini na si kinyume.

SteveD,

Nasema Mkuu wa Wilaya aliyechapa mboko....tunahitaji mtu kama huyu ili nchi kubadilika ndo rights za watu baadae!

Rights gani ktk kulea ufisadi, uzembe na uvivu? Angalia EPA hadi sasa hela ya kodi eti inatumika kuangalia wale jamaa kama wana hatia...wakati wana majumba kila kona ya Dar! Na wanahonga hakimu kwa pesa hiyo2 na kuachiwa na baadae kudai kulipwa fidia!!!!!

Yaani mboko kwanza..tena mbele ya mke wake...then ndo sheria!!

Lee alikuwa Warizi Mkuu wa Singapore...na watu walichapwa mboko kama nyumba ni chafu, haujalipa kodi, uzembe n.k leo hii Singapore ipo mbele zaidi ya nchi za Ulaya!

Will the Lee Thesis work in Tz?

Ndo maana watu tunapoongelea Human Rights...saa ingine sikubaliani!

Angalia China hakuna cha Human Rights.. ni mboko au ni shaba ukiiba..je leo China iko wapi?

Aje mpinzani, awe CCM ni hayo hayo...mfumo wa sheria kwanza...na kikosi maalumu kuona sheria zinatekelezwa kwa nguvu!!

Ndo human rights baadae!
 
Labda itafutwe mitumbwi!Suala la vipaumbele limekuwa ni tatizo katika Taifa letu kwa muda mrefu.Tunataka tukimbizane na kasi ya ulimwengu bila kupima 'uwezo' wetu.Just think of rada,ndege ya prezidaa na mengine mengi tu.Jiulize waliopitisha maamuzi ya kununua 'anasa' hizo walikuwa hawajawahi kuziona adha hzi ambazo pia ni aibu.We need some new people with new vision.

Kwani unafikiri hela haikutolewa kwa ajili ya kutengeneza sewage system?
Waulize 60bil zilienda wapi?

Nchi ya wajanja kila kitu ni ujanja ujanja tu, kila linalofanyika lina maslahi binafsi ya mtu ingawa linakula kodi za wananchi.
Hebu fikiria katikati ya mwaka jana nikiwa nimemtembelea rafiki yangu pale Kibangu lilipita gari la DAWASCO wakisisitiza kuwa shida ya maji imeisha kwa wakazi wa eneo hilo. Lakini juzi juzi nimempigia swahiba kuhusu maendeleo ya tangazo la wauza maji wa dawasco akanambia hakuna dalili.
Sasa watanzania wenzangu tunataka nani atufanyie wakati wenyewe tumeunda taasisi mbalimbali na tukaajili wataalamu kwa ajili ya kutula baada ya kutuhudumia?
 
Hayo maji ya mvua sio kazi ya DAWASCO. Hao ni City Council na Municipal zake tatu ndio wa kulaumiwa. Hata hivyo nchi hii utamlaumu nani kwa lipi!
 
Kwa nini wahamasishwe wananchi kuchangia gari la wagonjwa, wakati serikali kuu zinahamasishana kununua 4x4 vehicles (specifically the shangingis) kwa watumishi wake ambao kazi zao nyingi zinafanyika mijini!

Ndugu yangu wee, hao unaowaongelea kuchangishwa, wakati mwingine ununuzi wa kilo ya sukari (which costs around TZS 1200) inawapa taabu! Tena sukari yaweza kuonekana ni anasa, chumvi!!

Hali ni mbaya vijijini, kuliko tunavyofikiri..
 
..."mind the Gap" baina ya hizo crates na uwezo wa kuruka hao mabibi na mabwana ndipo utapogundua upeo wa akili za walengwa, na huyo kijana aliyejipatia 'ajira' ya chap chap...

BTW, Huyu mheshimiwa (mkanda nje na skuna zake) 'unadhani' aliruka salama bila kuyakanyaga hayo maji??? NEVER...

Hata serikali ikijenga miundo mbinu, ikiwemo better sewerage, bado wananchi hao hao watavitupa hovyo vifuko vya plastiki nk na tatizo kujirudia pale pale...

Tubadilike!!!

View attachment 3650

View attachment 3651

Big up,apo umenena jambo,pita pate ubungo stand mitaro imeziba,wafanya biashara wajioni wanavyo tupa taka ndani ya mitaro.japokuwa serikali nayo ina sehemu yake ya lawama lakini wananchi nao inabidi tubadilike sana tena sana,jitu lina nunua maji ya chupa au take away lipo ndani ya gari,likimaliza tu haja zake linatupa nje ya dirisha,anakwambia serilakali ipo itafagia.
Hivi wale wachina waliokuwa bize wanajenga jenga(chambers)posta,kariakoo na maeneo mengine walikuwa wana jenga nini? ilikuwa kuboresha sewages system au?
 
Jamani hivi hawa wachina wa Dawasco wamerekebisha kitu gani na pesa hizo za mkopo kutoka benki ya dunia kwa Dawasco? Au ilikuwa ni kiini macho kuchimba miataro jijini?
 
Nakumbuka kuna siku Kandoro alikuwa kwenye kipindi ITV akawa anajisifia sana wametengeneza vizuri miundo mbinu katika jiji mifano kibao akasema nenda Gerezani,Ilala,Manzese toka aongee tokea kipindi kile makatapilar yalipo ishia kusembua na kuweka karami kakizushi ndo wakawa wameishia hapo hapo.
Kweli Miafrica ndivyo tulivyo bora arudi mkoloni tu atuchape mboko atufundishe upya jinsi ya kutawala.
Najua hapo wametegeshea mpaka mwishoni au mwanzoni mwakani wata anza tena kuzuga zuga kusembua ili wachaguliwe na Miafrica.
 
Nchi akiacha kuendeshwa kisiasa hapo ndipo itakuwa mwanzo mzuri wa Tanzania mpya. Tazama sekonadri za Kata na Shule za msingi!!! Hivi hawa waliokuja na mpango huu walifanya homework yao vizuri? Sitaki kuamini kwamba hawa wliobuni mpango huu ni watu walioenda darsani!!!!
 
Ni vision inahitajika.........bila kujua nchi hii tunataka kwenda wapi mambo mengi tutakuwa tunapiga marktime tu.

Lakini na sisi wananchi nadhani tuna asilimia kubwa tunayochangia kwenye hizi messes kwa kuwa kwetu waoga wa kuhoji, kudai na kuwawajibisha viongozi wetu. May be uelewa ni mdogo au tatizo ni nini wenzangu mnisaidie.

Tatizo ni lile ulilolisema mwanzo WOGA. Hili ndilo lililotufikisha hapa tulipo. Takriban miaka 50 tangu uhuru mpaka leo bado tunaona picha kama hizo. Mtu ungetegemea kuwa hadi sasa nchi ingekuwa na upinzani wenye nguvu. at least 45% ya wabunge wangekuwa wa upinzani. Lakini woga wetu both wa kimaumbile na wa kifikra umetufanya tukubali utawala wa aina moja tu kwa miaka yote ingawa unonyesha wazi kuwa hauna muelekeo wa maendeleo. Katika kipindi hicho, nchi zote za kifarika zimeshuhudia mabadiliko ya aina fulani katika siasa/utawala. Ni Tanzania tu ndio bado ina mfumo ulele wa chama kile kile.

Hebu jamani tujitutumue. Tutafute pa kuanzia..
 
Kikubwa tunachohitaji ni viongozi walio na akili zilizopevuka na zinazoweza kupambaua lipi lipawe kipaumbele kwanza. Pili tuache mtazamo wa short cut. kupata pesa chap chap. Nikimaanisha nyingi ya hivi vitu (Kwa mfano Wa Vitambulisho) huwa ni dili za wakubwa (10%)
 
Princelee,
Mkuu utapata watu wengi sana wala usiwe na hofu kwani Wadanganyika hawataki kufanya kazi isipokuwa uchumaji wa aina hii..Umekaa kijiweni fedha inaingia!...
Damn! ama kweli sioni pa kuanzia ikiwa DECI wanaweza kutapeli watu kama Stanford bank na wakapata washabiki kibao, offer yako poa kabisa...
 
...tunajua kabisa source ya matatizo yetu yote na umaskini ni viongozi wasio na vision, wazembe,wezi na wala rushwa,tunajua kabisa tunaweza kujiletea maendeleo wenyewe kwa kutumia akili zetu na resources tulizonazo,sasa naomba tusizunguke sana maana tatizo tunalijua na tuanze kutafuta njia rahisi ya kupambana nalo kwa sasa bila ya kuwa kwenye power,naamini technology inaweza kusaidia sana maana ukiangalia vizuri kashfa zote za Richmond,EPA,BOT Towers etc zilianza kama tetesi lakini zilishika moto baada ya watu na magazeti kuanza kupiga kelele na kutoa details bila woga through websites kama JF,vijarida vicheche kama vya mwanakijiji,internet radio,magazeti binafsi etc nafikiri technology ni powerful weapon ambayo itatuondolea hawa mafisadi na ninaamini ndio ilimwondoa Lowassa na kina Karamagi na hata hizi arrest za mafisadi ni kazi ya technology,naona tuendelee na hii kazi tunayoifanya na wenye DATA za ufisadi na majina ya wezi wetu wasiache kuziweka na kuzisambaza kila kona inayowezekana ili watu wote waone...soma topic kama ya National ID jinsi watu walivyoichambua in deep na kutoa kila sababu inayo make sense,nina uhakika JK akisoma mawazo ya mle atabadilisha mawazo na kutupilia mbali project nzima,nina uhakika kuna watu humu wanajua in full details line by line jinsi wizi unavyofanyika na majina ya wahusika kuanzia ikulu mpaka TRA,wizarani etc andikeni maana ndio msaada wenu wa kumaliza ufisadi....inauma sana wakuu 97% ya gold inaishia kwa wajanja halafu wanatuambia wametusaidia kutuchimbia visima,hizi dharau lazima ziishe!
 
Source ya matatizo yetu ni foundation ile tuliowekewa na Mwalimu kubali ama kataa.Hadi tukubali hili ndio tutaweza kumove forward.Ukisema kweli kuhusu Mwalimu humu wanakujia juu na mashoka kama umeua, think twice.

SAHIBA,
 
sahiba,
Mkuu unaanza kuhofia hoja yako mwenye kabla hujaiweka... Hapa ni uwanja wa mjadala hakuna mtu anayeweza kuja juu na mashoka zaidi ya kupinga hoja yako kwa mifano iliyowazi..
Sasa kwa mfano unaposema foundation ya mwalimu ni ipi hiyo!..walioamua kuuza mashirika ni sisi wenyewe kinyume cha Ujamaa na waliouza ni viongozi ambao sisi wenyewe tuliwasdifia dhidi ya misingi ya mwalimu. Sasa iweje matokeo ya kubomoa misingi ile irudi tena kuwa tatizo ni misingi ya mwalimu..
Nambie hata kitu kimoja kiuchumi ambacho hadi leo hii utekelezaji wake unafuata Ujamaa!...
 
Suala sio kuufuata ama kutoufuata huo Ujamaa lakini nchi hii imejengwa na huo ujamaa hata kama hatuufuati sasa.Misisngi ya huo ujamaa 1967 ndio inayoiyumbisha nchi hadi sasa tutake tusitake.Baada ya kutaifisha mali za watu na kuchukua hivyo viwanda na kwa kiasi kikubwa vimetushinda big time kuviendesha.Wait a minute,imetuchukua miaka mingi sana kuwashawishi tena hao wawekezaji kurudi tena na kuwekeza kwetu kwa sababu ya ile misingi ya Mwalimu ya kijamaa. THINK twice.

SAHIBA.
 
Source ya matatizo yetu ni foundation ile tuliowekewa na Mwalimu kubali ama kataa.Hadi tukubali hili ndio tutaweza kumove forward.Ukisema kweli kuhusu Mwalimu humu wanakujia juu na mashoka kama umeua, think twice.

SAHIBA,

Ha ha ha! mkuu Sahiba, ukimlaumu Mwalimu hutauwawa, ni zile hoja zako ndo zitakuhukumu!
 
Heshima mbele mkuu...kwa kweli inasikitisha sana ukiangalia picha kaka hizo hapo juu...We fikiria hapo ni katika jiji la Dar es salaam..vp kuhusu Mtwara,Singida,Lindi na mikoa mingine hali ikoje??...Na kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya mipango miji,wanafanya nini hasa hawa???,Hivi serikali haiangalii haya????...Na tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya zaidi maana kipaumbele cha viongozi wetu wa kisiasa sasa hivi(mkumbo ambao mpaka watendaji wa serikali wameanza kuufuata) ni kuibuliana kashfa na wengine kuibuka na kuzijibu(badala ya kutatua matatizo ya kimsingi ya wananchi kama matatizo ya barabara,miundombinu ya maji safi na taka,elimu,afya nk)...Kazi ni kubwa sana MMK maana kilichopo sasa serikali kwa sasa badala ya kutauta matatizo ya msingi ya wananchi sasa ni kila kukicha inaibuka kashfa mara hii mara ile na viongoiz badala ya kufanya kazi wanakaa na kujiandaa/kuanza kujibu kashfa hizo..Tutafika kweli????,inasikitisha mno,fikiria Dunia ya sasa binadamu(ambaye ana hali mbaya mno kiafya) anapelekwa hospitali kwa mkokoteni unaovutwa kwa Punda ilhali kuna mzito yeye kazi yake ni kila siku kubadilisha mashangingi(magari ya kifahari)...nchi hii bwana aaaaaaaaaaaaaaaaargh....Ifikie kipindi wale tunaowapa dhamana ya kutuongoza watutendee haki jamani(kutuletea maendeleo) na si watunyonye(waingie madarakani klwa lengo la kuchuma/kutajirika na kutuacha wapiga kura tukitaabika kwa maisha magumu)....Watanzania tunahitaji kubadilika jamani(hata kama Miafrika ndivyo tulivyo).....Inasikitisha kwa kweli

Mipango Miji--soma habari ya mpango wa mji wa Kigali.

allAfrica.com: Rwanda: Kigali Master Plan to Be Unveiled Today (Page 1 of 1)
 
Tatizo hapa ni uongozi ikiwa hii ndio njia pekee ya kumfikisha mgonjwa hospital maana kiongozi anashindwa hata kuwahamasisha wananchi wakaona umuhimu wa kuchangishana na kununua ambulance hata kama itachukua miaka miwili ama mitatu hili ni tatizo.viongozi haohao wanaongoza kuuza mashamba na viwanja vya wazi na kwa manufaa yao.,,,think twice.

SAHIBA.

Sahiba Baba,
Kiongozi gani atakuwa na huo muda wa kuhamasisha?? MBUNGE haonekani kwenye jimbo mpaka uchguzi ukaribie, anasukuma SHANGINGI MKOANI, MKUU WA WILAYA kadhalika. Na kwa nini hasa kwenye huduma muhimu kama hizi tufikie kuchangishwa???? Kwa nini tusiseme safari hii hakuna MASHANGINGI kwa Wabunge tuna peleka MAGARI YA WAGONJWA Vijijini?? Wabunge wanaweza kusafiiri kwa njia za kawaida kwani wana ratiba ya vikao vya mwaka mzima ni lazima waweze kujipanga. Magari yatolewe kwa wale hasa ambao wanahitaji, tena sio bure iweni MKOPO unaokatwa kila mwezi ili PESA hiyo irudi kwa SEREKALI na ikahudumie MIRADI mingine. Swala la kuhamasha lije hapo Dar es salaam Kwani DUNIA YOTE ya VIONGZI iko hapo Serekali itoe VIFAA NA WATAALAMU Ihamasishe WANANCHI wasaidie kuchimba na kujenga hiyo mitaro na mdaraja na usafii na LAZIMA WAPATIWE POSHO FULANI isiwe kazi ya Kanisa au Mskiti.
 
Tatizo hapa ni uongozi ikiwa hii ndio njia pekee ya kumfikisha mgonjwa hospital maana kiongozi anashindwa hata kuwahamasisha wananchi wakaona umuhimu wa kuchangishana na kununua ambulance hata kama itachukua miaka miwili ama mitatu hili ni tatizo.viongozi haohao wanaongoza kuuza mashamba na viwanja vya wazi na kwa manufaa yao.,,,think twice.

SAHIBA.

...Nini tunahitaji kwanza?

...Ambulance ya kumfikishia mgonjwa hospitalini, au Hospitali yenye uwezo wa kumhudumia huyo Mgonjwa?

...kuna haja gani Ambulance kwenye vumbi hilo wakati na uhakika zahanati/hospitali wilayani hapo hata dakitari ni mbinde kumpata, achilia mbali vifaa, madawa na huduma za uhakika...!
 
Back
Top Bottom