Mwambelamwanitu
Member
- Aug 24, 2025
- 5
- 3
Wakuu, salama?
Kuna hali inashangaza sana.
Mimi ni mkazi wa meneo ya Goba, kabla ya mwezi November mwaka jana (2025) tulikuwa tunapata maji vizuri kabisa na kwa presha kubwa lakini nakumbuka kuelekea mwishoni mwa mwaka jana around hiyo November kuna hali ya upungufu wa maji ilitokea maeneo mengi ya Dar hadi ikamlazimu Waziri wa maji kuja kuweka kambi Dar pamoja na kutoa taarifa kwamba hali ile ilisababishwa na mvua kuchelewa kunyesha huko mikoani na kupelekea hata kutolewa ratiba ya mgao wa maji.
Mungu akasaidia mvua zikaanza kunyesha na waziri akatangaza tena rasmi kwamba mgao wa maji umeisha na DAWASA wahakikishe maji yanatoka vizuri maeneo yote.
Na ni kweli baada ya waziri kutangaza ule upungufu wa maji kwisha na mgao kwisha kwa muda kama wa wiki moja hivi au mbili hivi tulipata maji vizuri kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma lakini baada ya hapo ni kama Waziri wa maji aliondoka na maji yake, maji ikawa ni tatizo tena, yaani hata yakitoka ni kwa presha ndogo na mara kadhaa tumewapigia DAWASA simu wanasema umeme unasumbua au kuna wakati wanakuja na lugha kwamba pampu moja ya kusukuma maji kutoka tank kubwa la Tegeta na wazo imeharibika kati ya mbili zilizokuwepo na ni miezi sasa imekatika hiyo hali ikiwa inaendelea na ni bila hata kutoa taarifa rasmi hata kwenye page zao za mitandao ya kijamii
Cha kushangaza pia kuna maajabu yafuatayo:
Yanayofikirisha na kutia shaka:
DAWASA kuhujumu jitihada za Waziri wa maji ambaye kimsingi amekuwa anajitahidi sana
Kufungua maji siku mvua inanyesha tofauti na siku za jua kali tukiwa hatuna maji na tunayahitaji inaleta picha kwamba kuna rushwa imeingia DAWASA kutoka kwa wenye biashara ya kuuza maji kwenye magari au pia baadhi ya wafanyakazi wa DAWASA watakuwa pia wanafanya biashara hiyo na hivyo kutengeneza uhaba wa maji na kufanya biashara yao iwe na demand kubwa
Wafanyakazi wa DAWASA wamesoma udhaifu wa mtendaji mkuu mpya wa DAWASA na kutumia udhaifu huo kufanya wanavyotaka na kujinufaisha hasa ukiringanisha na mtendaji mkuu wa zamani ndugu Luhemeja ambaye kwa kweli alipokuwepo pale DAWASA mambo yalikuwa yanaenda vizuri na alikuwa anajitahidi kufuatilia mambo mengi na utendaji hadi kwenye kazi za site/field unakuta anakuwepo
Hitimisho: DAWASA iangaliwe na kuchunguzwa kuna tatizo kubwa pale, viwango na ubora wa utendaji kazi umekuwa unashuka na sisi wananchi ndiyo tunaopata shida...
Kuna hali inashangaza sana.
Mimi ni mkazi wa meneo ya Goba, kabla ya mwezi November mwaka jana (2025) tulikuwa tunapata maji vizuri kabisa na kwa presha kubwa lakini nakumbuka kuelekea mwishoni mwa mwaka jana around hiyo November kuna hali ya upungufu wa maji ilitokea maeneo mengi ya Dar hadi ikamlazimu Waziri wa maji kuja kuweka kambi Dar pamoja na kutoa taarifa kwamba hali ile ilisababishwa na mvua kuchelewa kunyesha huko mikoani na kupelekea hata kutolewa ratiba ya mgao wa maji.
Mungu akasaidia mvua zikaanza kunyesha na waziri akatangaza tena rasmi kwamba mgao wa maji umeisha na DAWASA wahakikishe maji yanatoka vizuri maeneo yote.
Na ni kweli baada ya waziri kutangaza ule upungufu wa maji kwisha na mgao kwisha kwa muda kama wa wiki moja hivi au mbili hivi tulipata maji vizuri kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma lakini baada ya hapo ni kama Waziri wa maji aliondoka na maji yake, maji ikawa ni tatizo tena, yaani hata yakitoka ni kwa presha ndogo na mara kadhaa tumewapigia DAWASA simu wanasema umeme unasumbua au kuna wakati wanakuja na lugha kwamba pampu moja ya kusukuma maji kutoka tank kubwa la Tegeta na wazo imeharibika kati ya mbili zilizokuwepo na ni miezi sasa imekatika hiyo hali ikiwa inaendelea na ni bila hata kutoa taarifa rasmi hata kwenye page zao za mitandao ya kijamii
Cha kushangaza pia kuna maajabu yafuatayo:
- Kuna wakati Waziri wa maji alikuja kwa ziara ya kikazi Dar na kwa siku alizokuwepo maji yakawa yanatoka japo sio kwa presha kubwa lakini yalitoka
- Kuna wakati naibu waziri wa maji naye alikuja Dar kwa ziara ya kikazi pia maji yakawa yanatoka japo sio kwa presha kubwa lakini yalitoka
- Zikifika tarehe za kusoma mita utaona maji yanatoka siku hiyo wanayopita baada ya hapo yanapotea tena
- Kuna sehemu line ya DAWASA imepita na maji yakitoka huwa yanavuja na Jirani yangu alipiga simu ku-report hiyo leakage cha ajabu fundi alifika kupaangalia akasema panahitajika vifaa maalumu (spares) za kupafanyia marekebisho na hajawahi kurudi tena na akipigiwa simu anasema bado hajapewa vifaa. Yaani imagine hawajali hata kuhusu upotevu wa maji kitu ambacho Waziri amekuwa anasisitiza sana kifanyiwe kazi
- Kuna tangazo TMA walitoa tahadhari ya mvua siku tatu Dar, cha ajabu zaidi siku mvua inanyesha na DAWASA ndiyo wakafungua maji yakawa yanatoka huku na mvua inanyesha

Yanayofikirisha na kutia shaka:
DAWASA kuhujumu jitihada za Waziri wa maji ambaye kimsingi amekuwa anajitahidi sana
Kufungua maji siku mvua inanyesha tofauti na siku za jua kali tukiwa hatuna maji na tunayahitaji inaleta picha kwamba kuna rushwa imeingia DAWASA kutoka kwa wenye biashara ya kuuza maji kwenye magari au pia baadhi ya wafanyakazi wa DAWASA watakuwa pia wanafanya biashara hiyo na hivyo kutengeneza uhaba wa maji na kufanya biashara yao iwe na demand kubwa
Wafanyakazi wa DAWASA wamesoma udhaifu wa mtendaji mkuu mpya wa DAWASA na kutumia udhaifu huo kufanya wanavyotaka na kujinufaisha hasa ukiringanisha na mtendaji mkuu wa zamani ndugu Luhemeja ambaye kwa kweli alipokuwepo pale DAWASA mambo yalikuwa yanaenda vizuri na alikuwa anajitahidi kufuatilia mambo mengi na utendaji hadi kwenye kazi za site/field unakuta anakuwepoHitimisho: DAWASA iangaliwe na kuchunguzwa kuna tatizo kubwa pale, viwango na ubora wa utendaji kazi umekuwa unashuka na sisi wananchi ndiyo tunaopata shida...