lwamu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 927
- 1,077
Uliza na maana ya Opus dei ili upate total package.samahani wakuu hivi "The holly grail" ina maana gani.
Kweli kabisa mkuu.Ninachojua mimi huyu jamaa alikuwa ni mwanachama wa vyama vya siri na alikuwa anajua siri kadhaa ya vyama hivi na baadhi ya siri hizo aliziweka kwenye michoro yake kwa codes fulani fulani lakini hakuwa akijua lolote kuhusu maisha ya Yesu kiasi kwamba tumtilie maanani kwa kiwango hiki....
😱!Kutokana na tafsiri za hiyo picha inasemekana miongoni mwa wanafunzi wa Yesu Maria Magdalena naye alikuwemo.
Na alishiriki chakula na Bwana ambaye pia inasemekana alikua ni bwana wake na walizaa mtoto.
Hii nimeisoma kwenye kitabu cha the Davinc Code.
Hakuna kitabu chochote ambacho kiliandikwa kumhusu yesu kipindi yupo yeye anaishi. Vitabu vyote (jumlisha na vile vilivyowekwa kwenye bible na vilivyokataliwa kuwekwa humo) vimeandikwa kipindi yesu ameshakufa, tena ni miaka karibu arobaini (miongo minne).Tunaomba source ya kitabu iwe ni ya maisha ya yesu kipindi iko na imeandikwa pia kipindi iko.tofauti na hapo ni ujinga kusoma ujinga.ni sawa baada ya miaka 1000 mtu anaandika kitabu kuwa raisi wa kwanza Tanzania ni kleist sykes na sio nyerere alafu kizazi kingine kione ni sawa kwa ivo vitabu uchwara
Sent using Jamii Forums mobile app
Unazungumzia vitabu gani?Hakuna kitabu chochote ambacho kiliandikwa kumhusu yesu kipindi yupo yeye anaishi. Vitabu vyote (jumlisha na vile vilivyowekwa kwenye bible na vilivyokataliwa kuwekwa humo) vimeandikwa kipindi yesu ameshakufa, tena ni miaka karibu arobaini (miongo minne).
Huu ni uongo mkubwa kabisa...Yaani ni kwamba, baada ya yesu kufa, kulitokea kimya cha miaka arobaini pasipo habari yoyote kumhusu yesu..! Hakukuwa na kitabu wala kipande cha karatasi kumhusu yesu.! Wataalamu wa historia wanajiuliza, kwanini habari nzito za matendo ya yesu zisisikike kwa kipindi chote hicho mpaka baada ya miaka arobaini?
Mathayo,Yohana,Petro,Yakobo [ndugu yake Yesu] na wengine weengi tu...Mkuu Eiyer amesema kuwa waandishi wa bible baadhi yao waliwahi ishi na yesu..! Labda nimuombe tu anitajie huyo mwandishi anayemzungumzia yeye.! Ni marco or paulo au hao wengine..?!
Hii nadharia ni ya kziamani sana na wapinga Ukristo wenzako walishaachana nayo kwasababu kama kungekuwa hakuna ushahidi wa kihistoria wa uwepo wa Yesu hapa duniani wangeshakuwa wamelisema hili tayari....Kuna nadharia moja inasema kwamba, yesu hakuwahi kutokea kwenye uso wa ardhi ya dunia hii! Story ya yesu ipo insanely similar to story za miungu mingine ya zamani kuliko yeye..! Kuanzia kuzaliwa na mama bikra bila ya baba, mpaka miujiza yote aliyoifanya baada ya kukua (habari za yesu zinajulikana kutoka kuzaliwa mpaka anamiaka saba or kumi, then kunatokea kimya. Hakuna habari yoyote kumsuhu yesu mpaka anafika miaka thelathini! Kwanini?!)
Then inakuja issue ya kuuwawa msalabani mpaka kufufuka, kote huko kunafanana kabisa na miungu mingine ya zamani kabla yake..! Actually mpaka ile picha ya bikira maria akimnyonyesha yesu nayo imekuwa hijacked kutoka kwa mungu wa kimisri..! Is it a coincidence..?!
Tafakari!
Ubavu
Sent using Jamii Forums mobile app
Unazungumzia vitabu gani?
Kuna vitabu viliandikwa wakati Yesu hajaja duniani na ambavyo viliandikwa baada ya yeye kuwepo hapa duniani....So kumbe ni kweli kuwa hakuna kitabu kilicho andikwa kumhusu yesu wakati akiwa hai.
Huu ni uongo mkubwa kabisa...
Unadanganya makusudi au ni kwasababu hujui ukweli ni upi?
Kwanza unapaswa kujua ni kwa namna ipi Wayahudi na Waisraeli kwa ujumla wao walikuwa wanatunza habari za manabii na watu wengine kabla hujaanza kudai madai ambayo siyo ya kweli,yaani unadanganya kwa makusudi au kwa kutokujua....
Baada ya Yesu kufa na kufufuka habari zake ziliendelea kuwepo lakini haikuwa kwa maandishi kwasababu kipindi kile Wayahudi walikuwa wakitunza kumbukumbu kwa kukariri tu na siyo kwa maandishi...Hahahahahaha @eiyer acha uongo bana.! Wayahudi wakariri historia?? Hakuna watu wanaopenda kuweka habari zao kwenye document kama wayahudi..! Unakumbuka habari za dead sea scrolls.?? Unadhani kwann waliziandika zile kama huwa wanakaririshana..?!
Wale jamaa walikuwa wataalamu wazuri wa kudocument historia zao. Kama waliweza kudocument vita mbali mbali kuanzia muda uliopiganwa mpaka mandhari sembuse habari nzito kama za yesu..?!
Injili ya kwanza kuandikwa iliandikwa na Marko miaka 30 baada ya Yesu kuondoka duniani na iliandikwa kwasababu aliamua tu na yaliyoandika ni machache sana kulinganisha na aliyotenda Yesu hapa duniani...Well nadhani bado unakubaliana na mimi...
Vitabu vingi tu vuliandikwa muda mfupi kabla ya Warumi kuivamia Jerusalem mwaka 70 A.D na ushahidi upo mwingi tu wa safari za Paulo,Petro,Yohana [aliyefungwa kisiwani Patmo kwasababu ya kuhubiri habari za Yesu],Bathlomayo, na wengine wengi tu...
Au hata hujui Yohana alifungwa kisiwai humo kwasababu ya kuhubiri kwake Injili kwenye miaka ya 50 A.D?
Muwe mnauliza....
Mathayo,Yohana,Petro,Yakobo [ndugu yake Yesu] na wengine weengi tu...
Dhana ya kufanana kwa Yesu na hao wapagani wengine wala siyo ishu,nitakupa mfano mmoja wa kijinga......
Ajali inaweza kutokea sehemu A namna ajali iliyotokea ikafanana na ajali iliyotokea sehemu B,kufanana kwa ajali hizi kutafanya ajali moja iwe ni uongo?
Mambo mengine bana.....
Nashukuru kwa kujua kabisa kuwa mfano wako ni wa kijinga ambao haufanani na hauna mashiko kabisa na habari nilizoleta mimi
Sent using Jamii Forums mobile app
Onyesha mahusiano kati ya post yako na mada husikawhat is your point buddy?
1.st Mary's?
2. age?
prove to members that i am wrong from my post!!!acha vioja.
Kimsingi una haki ya kuamini utakacho na hiyo ni haki yako ya msingi kabisa,lakini pale unapotaka kupinga imani ya mtu mwingine kwa kutumia imani yako unapaswa ujenge hoja za kueleweka na zenye mantiki ili uweze kueleweka....Mkuu bado naona unazunguka zunguka tu. Yaani unakubaliana na mimi kuwa story za yesu ziliandikwa baada ya yeye kufa... Tena kuna uwezekano mkubwa kuwa waandishi wa story hizo wala hawakuwa wale twelve apostles..!
Issue ya kuhifadhi habari zao kwa njia ya hadithi, inaonyesha wazi ya kuwa uwezekano wa kuongezwa chunvi ni mkubwa zaidi..!
Ahsante kwa ku-acknoledge kuwa mfano wako ni wa kijinga na haufanani kabisa na issue niliyoleta hapa..!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe hizi zote ni imani tu..! Ahaaa ! Basi mkuu nmekuelewa..!Kimsingi una haki ya kuamini utakacho na hiyo ni haki yako ya msingi kabisa,lakini pale unapotaka kupinga imani ya mtu mwingine kwa kutumia imani yako unapaswa ujenge hoja za kueleweka na zenye mantiki ili uweze kueleweka....
Unachokifanya hapa ni kupinga ninachokiamini mimi kwa kutumia imani yako ambayo imejengeka kwenye assumption za kutosha,sasa sijui ni nani anaweza kukuelewa...
Assumption kama "inawezekana hata story za Yesu hazikuandikwa na apostles" siwezi hata kuijibu kwasababu hata wewe uliyeandiaka huna uhakika na unachodai.Unajimaliza wewe mwenyewe....
Dhana nyingine ya "Issue ya kuhifadhi habari zao kwa njia ya hadithi, inaonyesha wazi ya kuwa uwezekano wa kuongezwa chunvi ni mkubwa zaidi" nayo ni ya kukisia tu,unajibuje mambo ambayo mtu anakisia?
Suala la Injili kuandikwa baada ya Yesu kuondoka hapa duniani ni la wazi kabisa na wala halina uzito wowote kwenye maelezo yako na hakuna kipya....
Shida yako ni kwamba ulikuwa unadhani unaandika kitu cha ajabu na kisichojulikana na wengi na ulidhani kina uzito sana wakati sivyo.....
Hakuna kipya kwenye madai yako....
kwanza uyo yesu ni kweli ana asili ya kizungu au propaganda tuNadhani ni wengi tumewahi kuisikia au hata kuiona picha maarufu duniani hasa kwa waumini wa dini ya kikristo ya THE LAST SUPPER iliochorwa na mtu anaedhaniwa kuwa miongoni mwa watu wenye akili nyingi (genious) kupata kutokea katika ulimwengu huu. Mtu huyo si mwingine ni LEONARDO DA VINCI.
Kimsingi wengi wetu mie nikiwa mmoja wao nilikua nadhani ni picha ndogo tu ya kawaida lakini inasemekana kwamba picha hio ina urefu wa futi 15 na upana wa futi 29. Vile vile kuna taarifa kwamba picha hio siku za nyuma ilikua ni siri na ilifichwa mpaka ilipofika yapata mwaka 1999 ndipo kwa mara ya kwanza iliwekwa kwenye maonyesho rasmi.
DA VINCI anajulikana kwa kutumia sana alama za siri kuficha jumbe mbalimbali katika sanaa zake. Na inasemekana hio ilitokana na na kuwepo kwa sheria kali kwa wale wote waliokuwa na mawazo tofauti dhidi ya roma katika kipindi cha renaisence
Turudi kwenye mada ya msingi;
Kwenye picha ya THE LAST SUPER inaonyesha yesu akipata mlo wa mwisho na mitume wake 12. Lakini kama tujuavyo miongoni mwa mitume 12 wa yesu hakuwa kuonekana mwanamke , wote walikua wanaume.
Lakini kwa upande wa kulia wa yesu katika picha hio anaonekana mtu anaedhani kwamba ni MARY MAGDALENE.
Swali la msingi ni kwamba
Je DA VINCI ALITAKA KUELEZA NINI KUPITIA PICHA HII KWA KUMUWEKA MTU AMBAE ANALETA UTATA WENGINE WAKISEMA NI MARY MAGDALENE LAKINI WAPO WANAOSEMA NI JOHN THE BAPTIST.
KARIBUNI.
kwanza uyo yesu ni kweli ana asili ya kizungu au propaganda tu
😂😂😂😂whats so special about kujua vitu vingi?Kwanza hiyo picha inaweza kuwa na mambo mengi kama madai yako yanavyoonesha lakini kusema "ina mambo mengi kuhusu Ukristo" unakuwa hujaeleweka...
Unajua Ukristo ni nini?
Ni wewe tu unayetaka tusiichukulie poa,tena unajisemea tu ukiwa umekaa mahali huku ukinywa juicy ya maembe au ugali na dagaa...
Kwanini isichukuliwe poa?
Au kwa sababu umesema wewe?
Leonardo Da Vinci ni nani hadi udhani yupo deep na Ukristo?
Nani amekuambia Ukristo ni dini?
Unajua Ukristo ni nini?
Unajua Yesu ni nani?
Unajua Leonardo Da Vinci aliishi duniani na kutofautiana na Yesu kwa miaka mingapi?
Ni nini maana ya "kuwa deep" sana?
Una ushahidi wa haya?
Hata kama ikiwa ni kweli,who is Vatican anyway?
"Ku realise biblia" ndiyo nini?
Biblia ni nini kwa ufahamu wako?
Inawezekana vipo hivyo vitabu pale St. Peter's Square,lakini hivyo vitabu ni vitabu gani na vinahusu nini na kwa ushahidi upi?
Kama ni vitabu vya historia ya kanisa?
Kuna siri nyingi duniani,nafahamu hili na inawezekana pale zikawepo,lakini hizo siri zinahusiana vipi na suala hili?
Kutibuliwa kwa Da Vinci na Warumi kuna mahusiano gani na suala hili?
Warumi ni akina nani hapa duniani hadi ukitibuana nao iwe ni jambo la namna hii?
Alama ya V ina maana gani?
Aliyekuambia yule ni Yesu ni nani?
Nani kakueleza yule ni Maria Magdalene?
Una ushahidi?
Hata mimi na wengine hapa kuna vitu vingu tunavijua,so what?
What so special about "kujua vitu vingi"?
What is "Vitu vingi" anyway?
Kwanini unataka unayemuuliza ahisi?
Au hata wewe hujui?
Au na wewe unahisi?
Ushahidi wa nadharia yako hii kuhusiana na ushoga wa kanisa katoliki na ushoga uko wapi?
Genius ni nani na ushahidi wako kuwa walikuwa mashoga uko wapi na kuwa kwao mashoga kunahusiana vipi na kanisa Katoliki?
Kwanza huna uhakika,umejenga hoja zako katika msingi wa kitu ambacho huna uhakika,hili ni tatizo la kwanza kubwa....
Ni vizuri hayo unayojua ukayaweka hapa kuliko kuandika mambo yanayoongeza maswali kuliko majibu...
Huwa nakuelewa sana mkuu watu wanapenda upuuzi pasipo kuumiza akili zao katika hata nyuzi wanazotoa. Kuishia kuleta mambo yasiyo ya great thinkersKuna mambo huwa yananisikitisha sana tena sana.....
Hii dunia ni yajabu kweli kweli.Yale mambo ambayo ni conspiracy yanaonekana ndiyo ukweli wenyewe na ukweli unaonekana ni conspiracy.Ukiangalia kwa mfano hili suala la hii inayoitwa picha ya last super,inajulikana ilichorea na mtu aliyeishi miaka mingi sana baada ya kuwepo kwa Yesu na inajulikana kabisa ni ya kubuni tu,ni kwanini watu wanaichukulia kwa namna kubwa kiasi hiki?
Mleta mada umetaka tuijadili picha hii,ni kwanini tuijadili wakati siyo kitu halisi na ni cha kubuni tu? Tena aliyebuni ni mtu tu na interest zake.Leonado da Vinci ni nani haswa hadi tuzingatie michoro yake kuhusu nyakati ambapo hakuwepo?
Ninachojua mimi huyu jamaa alikuwa ni mwanachama wa vyama vya siri na alikuwa anajua siri kadhaa ya vyama hivi na baadhi ya siri hizo aliziweka kwenye michoro yake kwa codes fulani fulani lakini hakuwa akijua lolote kuhusu maisha ya Yesu kiasi kwamba tumtilie maanani kwa kiwango hiki....
Kama tukague kile alichokuwa anakijua kuhusu haya mambo yao ya sirini hapo sawa lakini siyo kukagua michoro yake ya kubuni kama vile ni michoro halisi inayowakilisha maisha ya Yesu....