Nini tafsiri halisi ya picha ya the last supper?

aseenga

Senior Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
106
Reaction score
86
Nadhani ni wengi tumewahi kuisikia au hata kuiona picha maarufu duniani hasa kwa waumini wa dini ya kikristo ya THE LAST SUPPER iliochorwa na mtu anaedhaniwa kuwa miongoni mwa watu wenye akili nyingi (genious) kupata kutokea katika ulimwengu huu. Mtu huyo si mwingine ni LEONARDO DA VINCI.

Kimsingi wengi wetu mie nikiwa mmoja wao nilikua nadhani ni picha ndogo tu ya kawaida lakini inasemekana kwamba picha hio ina urefu wa futi 15 na upana wa futi 29. Vile vile kuna taarifa kwamba picha hio siku za nyuma ilikua ni siri na ilifichwa mpaka ilipofika yapata mwaka 1999 ndipo kwa mara ya kwanza iliwekwa kwenye maonyesho rasmi.

DA VINCI anajulikana kwa kutumia sana alama za siri kuficha jumbe mbalimbali katika sanaa zake. Na inasemekana hio ilitokana na na kuwepo kwa sheria kali kwa wale wote waliokuwa na mawazo tofauti dhidi ya roma katika kipindi cha renaisence

Turudi kwenye mada ya msingi;
Kwenye picha ya THE LAST SUPER inaonyesha yesu akipata mlo wa mwisho na mitume wake 12. Lakini kama tujuavyo miongoni mwa mitume 12 wa yesu hakuwa kuonekana mwanamke , wote walikua wanaume.
Lakini kwa upande wa kulia wa yesu katika picha hio anaonekana mtu anaedhani kwamba ni MARY MAGDALENE.

Swali la msingi ni kwamba
Je DA VINCI ALITAKA KUELEZA NINI KUPITIA PICHA HII KWA KUMUWEKA MTU AMBAE ANALETA UTATA WENGINE WAKISEMA NI MARY MAGDALENE LAKINI WAPO WANAOSEMA NI JOHN THE BAPTIST.
KARIBUNI.
 
the last supper.jpg
 
Kuna mambo huwa yananisikitisha sana tena sana.....

Hii dunia ni yajabu kweli kweli.Yale mambo ambayo ni conspiracy yanaonekana ndiyo ukweli wenyewe na ukweli unaonekana ni conspiracy.Ukiangalia kwa mfano hili suala la hii inayoitwa picha ya last super,inajulikana ilichorea na mtu aliyeishi miaka mingi sana baada ya kuwepo kwa Yesu na inajulikana kabisa ni ya kubuni tu,ni kwanini watu wanaichukulia kwa namna kubwa kiasi hiki?

Mleta mada umetaka tuijadili picha hii,ni kwanini tuijadili wakati siyo kitu halisi na ni cha kubuni tu? Tena aliyebuni ni mtu tu na interest zake.Leonado da Vinci ni nani haswa hadi tuzingatie michoro yake kuhusu nyakati ambapo hakuwepo?

Ninachojua mimi huyu jamaa alikuwa ni mwanachama wa vyama vya siri na alikuwa anajua siri kadhaa ya vyama hivi na baadhi ya siri hizo aliziweka kwenye michoro yake kwa codes fulani fulani lakini hakuwa akijua lolote kuhusu maisha ya Yesu kiasi kwamba tumtilie maanani kwa kiwango hiki....

Kama tukague kile alichokuwa anakijua kuhusu haya mambo yao ya sirini hapo sawa lakini siyo kukagua michoro yake ya kubuni kama vile ni michoro halisi inayowakilisha maisha ya Yesu....
 
Mkuu Eiyer mimi huwa nakukubali sana kwa kazi yako humu jukwaani.

Mimi nina swali kwako kuwa huyu da vinci kama unavyosema kuwa aliishi kipindi kireefu baada ya Yesu, na mimi sitilii maanani kazi zake za kuchanganya ulimwengu hasa sisi tunaomini katika kristo, lakini mimi najiuliza ni kwanini Wayahudi wamekuwa wakitumiwa sana kuupotosha ukweli wa Neno la Mungu kwa kiasi hiki??????

Pia Huyu da vinci aliyaleta haya ili iweje maana naamini hakuna kitu bila sababu ya hicho kitu huenda unaufaham kidogo kuhusu huyu mtu na mazingira ya kipindi chake alichoishi.

Nipanue ubongo kidogo hapo mkuu.
 
UKRISTO

ALEXANDER,THE GREAT(actually the invader/barbarian)

Alexander,The Great(the barbarian,the invader) aliivamia Kemet(Misri) mwaka 332 BC na kumuondoa mfalme(farao) na yeye kuchukua kiti cha ufalme akiwa hajui chochote kuhusu mila na desturi za Misri.

Aliwalazimisha viongozi wa “dini” iliyokuwa inaabudiwa wamkubali katika dini yao,lakini walimkatalia.Alexander mvamizi alikufa mwaka 323 BC.

Mrithi wa Alexander ,Ptolemy I au Soter(maana ya soter ni mwokozi) naye alikataliwa kuwa sehemu ya “dini” ya wamisri wa kipindi hicho lakini katika mji wa Memphis alipata baadhi ya viongozi wa dini waliosaliti na kumkubali.Walimpa jina la SERAPIS kwa kuunganisha majina Osiris na hepis.Huyu Ptelomy I ndiye aliyetibua misingi ya imani ya wamisri wa kipindi hicho.

Ptolemy I au Soter au Serapis au Christus alijipa cheo cha farao,alitengeneza sanamu ya kichwa yenye sura yake na watu wote walilazimishwa kuabudu lile sanamu.Waliomwabudu serapis walikuwa wanaitwa wakristo(neon la Kigiriki Christus)

SERAPIS 350 BC

ARIUS(256-336 A.D)

Alikuwa mmoja wa viongozi wa dini chini ya utawala wa warumi aliyepaza sauti kuwa kuabudu sanamu la serapis haikuwa sawa hivyo watu wote waache kuliabudu.

MKUTANO WA NICEA 325 A.D(the council of nicea)

Uliwakutanisha viongozi wa juu wa dini chini ya uenyekiti wa mfalme Constantine na ajenda kuu ya kwanza ilikuwa ni kumnyamazisha Arius asiendelee kueneza sumu ya kupinga kumuabudu serapis.Katika kipindi chote kulikuwa hakuna mtu anayeitwa yesu(jesus),aliyeabudiwa alikuwa ni serapis soter au mwokozi kwa Kiswahili.

MAAZIMIO YA MKUTANO WA NICEA 325 A.D

Ambapo ilitolewa “statement” ya imani ya kikristo iliandikwa na makasisi(bishops?) wa kanisa la roma wapatao 318.statement(ambayo ni kanuni ya imani kwenye kanisa katoliki la roma) inasomwa ‘nasadiki kwa mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia,na kwa yesu kristo mwanae wa pekee’(hapa anaongelewa serapis sanamu).

1.Kubadilisha sanamu la serapis na kuweka la yesu

2. Kumfukuza Arius(exile) asiendelee kupinga imani ya warumi
 
Ni kweli kwamba zamani waliabudu masanamu na kitendo hicho kilimchukiza sana Mwenyezi Mungu alichukizwa sana na kisa hiki hata kwenye kitabu cha Kutoka 34:4 amesema mimi ndiyo Mungu wenu msiabudu miungu wengine kwakua mimi Mungu wenu ni mwenye wivu.

Ni kweli Alexandre the Great alitaka kutawala dunia na aliiteka India yote na kitu alichofanikiwa katika utawala wake ni kuchanganya mila ki-Giriki na za mataifa aliyoyateka.

Roman Empire ilikuwa ikiabudu masanamu. Wafuasi wa kwanza wa Yesu Kristo ambao ndiyo wakristu wa kwanza walikuwa mitume wake 12 pamoja na mama yake. Hawa walipigwa vita sana Israel na walikimbilia Siria. Petro ambae aliachwa kuwa mwamba wa kanisa alikufa kwa kusulubiwa na wa Rumi kama Yesu na aliomba wamsulubu kichwa chini kwani hawezi kujilinganisha na Yesu ambae ni mtakatifu sana kwake.
 
Ni kweli kwamba zamani waliabudu masanamu na kitendo hicho kilimchukiza sana Mwenyezi Mungu alichukizwa sana na kisa hiki hata kwenye kitabu cha Kutoka 34:4 amesema mimi ndiyo Mungu wenu msiabudu miungu wengine kwakua mimi Mungu wenu ni mwenye wivu.

Ni kweli Alexandre the Great alitaka kutawala dunia na aliiteka India yote na kitu alichofanikiwa katika utawala wake ni kuchanganya mila ki-Giriki na za mataifa aliyoyateka.

Roman Empire ilikuwa ikiabudu masanamu. Wafuasi wa kwanza wa Yesu Krusto ambao ndiyo wakristu wa kwanza walikuwa mitume wake 12 pamoja na mama yake. Hawa walipigwa vita sana Israel na walikimbilia Siria. Petro ambae aliachwa kuwa mwamba wa kanisa alikufa kwa kusulubiwa na wa Rumi kama Yesu na aliomba wamsulubu kichwa chini kwani hawezi kujilinganisha na Yesu ambae ni mtakatifu sana kwake.
mkuu kwa heshima kubwa niliyonayo kwako i will rest my case😉😀
 
Kutokana na tafsiri za hiyo picha inasemekana miongoni mwa wanafunzi wa Yesu Maria Magdalena naye alikuwemo.
Na alishiriki chakula na Bwana ambaye pia inasemekana alikua ni bwana wake na walizaa mtoto.
Hii nimeisoma kwenye kitabu cha the Davinc Code.
 
Back
Top Bottom