Nini tafsiri halisi ya picha ya the last supper?

Nini tafsiri halisi ya picha ya the last supper?

Mbona huyo Mary mwenyewe, anaonekana akiwa BIZE zaidi na Wapambe/Mawaziri/Wanafunzi wa Yesu...!?

Picha inajionesha wazi kuwa Mlengwa/mtajwa (Yesu) as if hausiki na Mary, na yeye wala hajali..!

Da vinci angekuwa hai, maswali ya kumuuliza, ni je...! Mary alivamia kwenye Cabinet au alikuwa ni Mualikwa...?

Na kwa nini kwenye picha ameonesha utovu wa nidhamu, badala ya kuwa beneti na Mr Chairman, ameonekana kuvutiwa na kuwa concetrated na watu upande mwingine...!!

Najaribu kuwaza tu..........huyu Da vinci ameibuni picha hii kutoka wapi...! Kwani naamini miaka hiyo nyuma yeye hakuwepo.

Mawazo na michango iendelee...

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu hiyo picha achana nayo,ina mambo mengi sana yamejificha kuhusu ukristo ndani ya hiyo picha,usiichukulie poa kama uionavyo,hiyo ipo zaidi ya hivyo,kwanza tukianza na LEONARDO DA VINCI,alikuwa ni mbobezi wa masuala ya dini ya ukristo,jamaa alikuwa deep sana kuhusu JESUS,Vatican wanamjua jamaa,kumbuka WARUMI ndio walio`realise BIBLIA kama ulikuwa haujui,na kuna vitabu vingi vipo chini ya mahandaki pale ST.PETER SQUARE,pale chini pana siri nyingi za hii dunia,DA VINCI walimtibua WARUMI,nna akawa ni adui namba moja ndio sababu ya kuanza kuacha jumbe kwa mtindo wa CODES,ikiwemo hii picha ya THE LAST SUPPER,huo muegama wa marry magdalena ulioleta alama ya V kati ya JESUS & MARRY,haikuwa bahati mbaya kwa mchoraji,pia jiulize kwanini vile vikombe vya kanisani navyo vimekaa kwa mtindo wa V zilizogeuziana migongo,unadhani ni urembo,hawa makasisi hasa wa roman kuna vitu vingi sana wanavijua kuliko unavyodhani,unahisi ushoga wa roma umetokea bahati mbaya,una historia ndefu na kanisa linautambua lkn kwa mlango wa nyuma,ila tu ujue una karne nyingi,kibaya zaidi ma`genius wote wa kale walikuwa mashoga,na inasemekana hao hao mashoga ndio watu pekee walioibadirisha dunia kimaendeleo hadi tumefika hapa tulipo leo,including huyo Da vinci,einstein and so so,binafsi kuna mengi sana nayajua,ila nikipata muda takuwa nayaweka hapa,so tusichukulie mambo kirahisi coz tumezaliwa na kuaminishwa hivyo,uhalisia haupo kama macho yetu yaonavyo....ni tofauti kabisa wakuu!
 
Kama alivosema mkuu Eiyer ile picha ni mawazo tu ya mtu binafsi tena mtu aliyekua mpagani na inasemekana alikua gay so alitengwa na dini na ndio maana alitaka sana kupotosha watu katika michoro yake. Lakini pia hii tafsiri ya kua kwenye ile picha kuna mwanamke ni ya Dan Brown mtunzi wa kitabu cha Da Vinci Code ambacho yeye mwenyewe mtunzi mwanzoni kabisa anakiri vingi alivoandika ni fiction (vya kufikirika). Sasa mleta mada naona kaangalia movie au kasoma kitabu na ndio vinamchanganya. Ni sawa na mtu anaeamini story ya movie Titanic ya Leonardo diCaprio (Jack) kua ni ukweli wakati director wa movie James Cameron anasema ni utunzi tu na hakukua na mtu alieitwa Jack kwenye Titanic ya ukweli.
 
Sawa Mkuu...ila kipi bora, tuendelee kuhoji picha ya Da vinci, ama kuitazama picha tu na kujitafakari kimya kimya....!!

Maana naona kama unataka kufunga mjadala...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hiyo picha achana nayo,ina mambo mengi sana yamejificha kuhusu ukristo ndani ya hiyo picha,usiichukulie poa kama uionavyo,hiyo ipo zaidi ya hivyo,
Kwanza hiyo picha inaweza kuwa na mambo mengi kama madai yako yanavyoonesha lakini kusema "ina mambo mengi kuhusu Ukristo" unakuwa hujaeleweka...

Unajua Ukristo ni nini?

Ni wewe tu unayetaka tusiichukulie poa,tena unajisemea tu ukiwa umekaa mahali huku ukinywa juicy ya maembe au ugali na dagaa...

Kwanini isichukuliwe poa?

Au kwa sababu umesema wewe?
kwanza tukianza na LEONARDO DA VINCI,alikuwa ni mbobezi wa masuala ya dini ya ukristo
Leonardo Da Vinci ni nani hadi udhani yupo deep na Ukristo?

Nani amekuambia Ukristo ni dini?

Unajua Ukristo ni nini?
,jamaa alikuwa deep sana kuhusu JESUS,
Unajua Yesu ni nani?

Unajua Leonardo Da Vinci aliishi duniani na kutofautiana na Yesu kwa miaka mingapi?

Ni nini maana ya "kuwa deep" sana?
Vatican wanamjua jamaa,
Una ushahidi wa haya?

Hata kama ikiwa ni kweli,who is Vatican anyway?
kumbuka WARUMI ndio walio`realise BIBLIA kama ulikuwa haujui,
"Ku realise biblia" ndiyo nini?

Biblia ni nini kwa ufahamu wako?
na kuna vitabu vingi vipo chini ya mahandaki pale ST.PETER SQUARE,pale chini pana siri nyingi za hii dunia,DA VINCI walimtibua WARUMI,
Inawezekana vipo hivyo vitabu pale St. Peter's Square,lakini hivyo vitabu ni vitabu gani na vinahusu nini na kwa ushahidi upi?

Kama ni vitabu vya historia ya kanisa?

Kuna siri nyingi duniani,nafahamu hili na inawezekana pale zikawepo,lakini hizo siri zinahusiana vipi na suala hili?

Kutibuliwa kwa Da Vinci na Warumi kuna mahusiano gani na suala hili?

Warumi ni akina nani hapa duniani hadi ukitibuana nao iwe ni jambo la namna hii?
nna akawa ni adui namba moja ndio sababu ya kuanza kuacha jumbe kwa mtindo wa CODES,ikiwemo hii picha ya THE LAST SUPPER,huo muegama wa marry magdalena ulioleta alama ya V kati ya JESUS & MARRY,haikuwa bahati mbaya kwa mchoraji,pia jiulize kwanini vile vikombe vya kanisani navyo vimekaa kwa mtindo wa V zilizogeuziana migongo,unadhani ni urembo,
Alama ya V ina maana gani?

Aliyekuambia yule ni Yesu ni nani?

Nani kakueleza yule ni Maria Magdalene?

Una ushahidi?
hawa makasisi hasa wa roman kuna vitu vingi sana wanavijua kuliko unavyodhani,
Hata mimi na wengine hapa kuna vitu vingu tunavijua,so what?

What so special about "kujua vitu vingi"?

What is "Vitu vingi" anyway?
unahisi ushoga wa roma umetokea bahati mbaya,una historia ndefu na kanisa linautambua lkn kwa mlango wa nyuma,ila tu ujue una karne nyingi,kibaya zaidi ma`genius wote wa kale walikuwa mashoga,
Kwanini unataka unayemuuliza ahisi?

Au hata wewe hujui?

Au na wewe unahisi?

Ushahidi wa nadharia yako hii kuhusiana na ushoga wa kanisa katoliki na ushoga uko wapi?

Genius ni nani na ushahidi wako kuwa walikuwa mashoga uko wapi na kuwa kwao mashoga kunahusiana vipi na kanisa Katoliki?
na inasemekana hao hao mashoga ndio watu pekee walioibadirisha dunia kimaendeleo hadi tumefika hapa tulipo leo,including huyo Da vinci,einstein and so so,binafsi kuna mengi sana nayajua,ila nikipata muda takuwa nayaweka hapa,so tusichukulie mambo kirahisi coz tumezaliwa na kuaminishwa hivyo,uhalisia haupo kama macho yetu yaonavyo....ni tofauti kabisa wakuu!
Kwanza huna uhakika,umejenga hoja zako katika msingi wa kitu ambacho huna uhakika,hili ni tatizo la kwanza kubwa....

Ni vizuri hayo unayojua ukayaweka hapa kuliko kuandika mambo yanayoongeza maswali kuliko majibu...
 
MKUU Eiyer habari yakoo
Nina maswali na malalamiko juu yako please nisikilize.
...malalamiko...
Muda mwingi umekua ukiwa unaelezea kitu umekua ukisema kua hii mada ni ndefu nitaitolea THREAD LAKINI UMEKUA hufanyi hivyo, mkuu hata kama unashughuli nakuomba utimize ahadi yako.

....Maswali...
Mkuu kwa manufaa ya wotee tunaomba ututolea ufafanuzi juu ya Yesu kua na Mtoto na mahusiano na Maria magdalena hili nimeliona wakilijadili pia kwenye chanel ya Discover.
Ahsante...
 
Kwanza mkuu thread ninayotaka kuileta hapa ni ya kiutafiti ambayo itajijenga kwenye hoja na ushahidi hivyo siyo kazi ndogo...

Ninahitaji muda wa kufanyia utafiti kile ambacho ninataka kukileta hapa ili kiwe na nyama za kutosha na siyo kuishia kujisemea tu hiki kiko vile bila kuelezea kwa kina ni kwanini kipo hivyo....

Pamoja na hayo kuna harakati za kimaisha hivyo mkuu muda nao unakuwa mdogo,lakini tuombeane tu uzima na afya tele ili niweze kukamilisha....

Nimefikiria hadi kuandika vitabu lakini bado natafakari sana lakini hapa ni LAZIMA nilete thread iliyoshiba kwanza....

Nikuombe uvumilivu tu mkuu wangu....

....Maswali...
Mkuu kwa manufaa ya wotee tunaomba ututolea ufafanuzi juu ya Yesu kua na Mtoto na mahusiano na Maria magdalena hili nimeliona wakilijadili pia kwenye chanel ya Discover.
Ahsante...
Yesu hajawahi kuwa na mtoto,hizi ni mbinu za Shetani kuendeleza uwongo wake kama alivyofanya pale Eden na hata baada ya hapo....

Discover chanel siyo kituo salama kwa Wakristo na hata wale wanaotaka kujua ukweli wa historia ya dunia hii.Hawana tofauti na CNN au BBC,uwongo mwingi sana kule....

Historia ya kweli ya Yesu imo kwenye biblia.Waandishi waliishi naye na wengine miaka michache baada yake,achana na hawa waliokuja kuishi miaka 1000 na zaidi baadaye kutaka kujidai wanamjua zaidi kuliko wale walioishi naye....

Yote hayo ni uwongo mkuu.....
 
Mkuu Eiyer ahsante sana..
Nakuomba utuvumilie sisi wana jf tusiojua Eng na tusiopenda kujisomea kukugeuza Gogle yetu,
Mkuu kama una muda wa kutosha nakuomba utufafanulie lolote lile unalo faham kuhusu Huo mchoro wa Last Supper iwe ni uongo au ukweli japo nasi tuyafahamu yanayooneshwa kwenye mchoro huo as Code..
Ahsante Mkuu Eiyerpedia Swahili.
 
Kwa haraka haraka....

Kwanza wengi hawafahamu kwamba kuna michoro mingi tu kabla ya huyu Leonardo Da Vinci kuzaliwa ilishachorwa na wachoraji wengine na ilikuwa tofauti na huu mchoro wa Da Vinci.....

Pili,hakuna anayejua kwa hakika kuwa Leonardo Da Vinci alikuwa akimaanisha nini kwenye michoro yake kwasababu hakuwahi kuacha maelezo kuelezea alichokuwa akikimaanisha.Kitu pekee ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Leonardo Da Vinci alibuni mchoro huo kwa namna alivyouona na kufikiri yeye na huenda alikuwa na maana ambayo hakuna ajuaye....

Kwa maana hii,yote yanayohusu mchoro huu ambao ni wa kubuni nayo pia ni ya kubuni kwasababu hayana uhakika.Sijaona sababu ya msingi ya watu kuhangaika na mambo ambayo yamejengwa kutoka mchoro wa kubuni na usio na ukweli wowote...

Kama akija mtu na kusema kuwa huyu Da Vinci alikuwa anamaanisha chochote nje ya masuala ya Yesu huenda akasikilizwa kwa sehemu,lakini akija na kusema kuwa Da Vinci alikuwa anamaanisha chochote kuhusu Yesu hatasikilizwa kwasababu ni uwongo kwasababu Da Vinci hakuishi wakati wa Yesu na kwa maana hiyo alibuni tu huo mchoro,kama alibuni kitakachosemwa chochote kuhusu mchoro huo nacho kitakuwa cha kubuni tu....

Nikija kwenye unachotaka kuhusu mabaya aliyomaanisha Da Vinci kuhusu mchoro huo nitaeleza kwa kifupi kwa sababu sikujiandaa na hili na pia ni jambo ambalo halina uhakika pia kwasababu nilizozieleza hapo juu....

Karibu kwa ufupi..

Leonardo Da Vinci alizaliwa huko Italia tarehe 15 April 1452 na jina lake kamili ni Lionardo di ser Piero da Vinci.Leonardo Da Vinci alijulikana sana kwa taaluma yake ya uchoraji mahiri sana kwa wakati wake.Wakati wa ujana wake,Da Vinci na vijana wengine watatu walishitakiwa kwa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.hii ilikuwa ni mwaka 1476.

Leonardo Da Vinci aliwahi kuwa msaidizi wa anayedaiwa kuwa mtoto wa Papa Alexanda wa 6 mwaka 1502 hadi October 18 1502.Borgia alizaliwa Sept 13,1475,huko Rumi.Wazazi wake wakiwa ni Papa Alexander na mwanamke aliyajulikana kama Vannozza Dei Cattanei....

Inadaiwa kwamba wakati Da Vinci akiwa ni msaidizi wa kijana huyu huko Rome,walianzisha mahusiano ya kingono ya kinyume na maumbile.Inadaiwa kwamba katika kipindi ambacho walikuwa kwenye mapenzi moto moto ndipo Leonardo Da Vinci alichora picha hizi za kubuni na kutokana na mapenzi yake kwa Borgia aliaamua kuchora sura ya Borgia kwenye umbo la mtu aliyebuni kuwa kama Yesu...

Picha hii maarufu inadaiwa kuchorwa kati ya mwaka 1499 na 1503...

Baadhi ya watafiti wanadai kwamba lengo lingine la mchoro wa Leonardo Da Vinci ni kutaka kuonesha kuwa Yesu hakuwa na Uungu wowote bali alikuwa ni mtu tu...

Jambo hili lilionekana kwenye michoro hiyo ambayo alichora michoro yake bila kuwawekea kitu kinachoitwa "Halo"..

Halo ni nini?

Halo ni ule mduara unaoonekana kichwani kwa mtu yoyote anayechukuliwa kuwa ni mtakatifu...

Angalia picha hizi hapa chini....

36AE7ED900000578-3713591-image-a-19_1469741249702.jpg

Mchoro wa Leonardo Da Vinci wa karne ya 15 ukionesha wahusika wa mchoro wakiwa hawana hiyo mizunguko vichwani mwao kuonesha utakatifu....

36AE7F3500000578-3713591-image-m-22_1469741326502.jpg

Mchoro wa karne ya 14 ukionesha karamu ya mwisho kama ulivyobuniwa na mchoraji kipindi hicho.Hapa tunaona wahusika wakiwa na "halo" au round fulani hivi vichwani mwao kuonesha "utakatifu" wao....

36AE7EE100000578-3713591-image-a-24_1469741352055.jpg

Mchoro mwingine wa karamu ya mwisho wa karne ya 14...

Ukiangalia michoro hii inatofautiana,lakini yote ni ya kubuni tu....

Kwa maana hii ni kwamba mchoro wa Da Vinci una maana mbili hasi na ambazo pia hazina uhakika au ushahidi sana au hakuna kabisa ushahidi wowote...

1;Mahali alipoamua kumchora mtu aliyepachikwa kuwa ni Yesu alimchora mtu huyo kwa sura ya Cecare Borgia...

2; Alichora p[icha hizo kuonesha kuwa Yesu hakuwa na Uungu wowote ule...

Ni hayo tu kwa ufupi sana....

Na dhani nimekata kiu yako kwa sehemu....
 
Hapana siyo mimi hii niliisoma kwenye kitabu cha Davinc code
,kina tafsiri ya vitu vingi vingi vinavyotambulika katika ukristo.
Amejaribu kuvidadavua kwa uwazi zaidi.
Ila kikubwa ni kushikilia Imani yako.
Amini unachoamini yeye Da Vinc anaweza asiwe Sahihi ama akawa Sahihi,
Lakini haifai kubadili imani ya mtu.
Leta hizo nukuu za vitabu hapa
 
Asante mkuu
 
Ahsante sana mkuu Eiyer nadhani unao kaa nao ndugu/jamaa wanafaidi sana kupokea nondo kama hizi.
Shukrani ubarikiwe..

Sasa mkuu japo tueleze hizo code za vikombe sijui v na hiyo mikate labda wana suggest alikua analenga kutueleza nini?
 
Back
Top Bottom