Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Pole sana...haya masuala bwana, kafanyiwe tu vipimo dada, kuna sababu nyingi...Hormonal Imbalance,unaweza kuwa una develop kitu kama uvimbe kwenye tumbo la uzazi....nenda tu kwa Gyno, akutazame kwa undani.....!! Nina mwenzangu aliambiwa ana Hormonal Imbalance, akapewa aina fulani ya Contraceptives ika-regulate ile damu baada ya miezi mitatu....! Tafuta kujua tatizo nini kwanza!
 
Dah ila hawa madaktari kila wakipima wanadai hakuna tatizo.SIJUI PA KUANZIA.NATAMANI NINGEPATA DAWA TOKA HUMU JF.NISHAENDA HOSPITAL MPAKA NIMECHOKA
 
ku bleed muda mrefu huo,sio kitu kizuri kabisa.jee umejaribu kwenda ocean road hospital?jaribu na huko
 
Dah ila hawa madaktari kila wakipima wanadai hakuna tatizo.SIJUI PA KUANZIA.NATAMANI NINGEPATA DAWA TOKA HUMU JF.NISHAENDA HOSPITAL MPAKA NIMECHOKA

pole sana dada usikate tamaa kwenda hosp.maana ndo kwenye vipimo vya uhakika kama wengine walivyoshauri kamuone daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama kama ulishakwenda jaribu kwa wengine uone kama jibu litakuwa ni lilelile,vinginevyo ni vigumu kutoa matibabu bila kipimo.hata hivyo naomba kujua je ulikuwa unatumia dawa za uzazi wa mpango na kama ulikuwa unatumia ni kwa muda gani?.
 
Pole Mkuu !
Wakati ukijifikiria fikiria kwenda hospital tena. Tumia contraceptive pills ziitwazo :
LO- FEMENAL AND FERROUS FUMARATE TABLETS
(zenye contents za norgestrel and ethinyl estradiol tablets and ferrous fumarate tablets).
Tumia kwa wiki 3.
(ule mstali wa chini wenye rangi tofauti na mingine usimeze kabisa).
Then angalia matokeo yake baada ya hizo 3 weeks. Kama hamna mabadiliko,
its real kuna tatizo kubwa la kumuona gyno haraka.
 
Kutoka kwa hedhi mfululizo kunaweza kukasababishwa na mambo yafuatayo 1) mabadiliko ya kihomoni 2) matatizo ya kukoma kuganda kwa damu (coagulation defect) 3) uvimbe katika mfuko wa kizazi (myoma) 3) kansa ya shingo ya kizazii (cervical carcinoma)
kitu cha msingi katika kujua tatizo ni kuchukua maelezo ya kina kuhusu ugonjwa wako na maisha yako ya kijamii kama vile kujua umri wako kama una watoto au laa pamoja na idadi yao.kama unavuta sigara au kunywa pombe.ulianza kufanya mapenzi ukiwa na umri gan na kwa ujumla mahusiano yako ya kimapenzi.na pia lazima ijulikane kam dam huwa inatoka muda wote au labda mara baada ya kujamiana na pia kama kuna dalili nyingine zinazoambana na kutoka kwa damu kama tumbo kuuma.na baada ya maelezo basi daktari atakuangalia kwa kukupima ili kujua kama kuna uvimbe au kipi ni chanzo cha tatizo na baada ya hapo basi atakuandikia vipimo.kutibu tatizo lako bila kujua tatizo kunaweza kuleta nafuu kwa muda lakin tatizo lako likarudi.sina uhakika na jinsi madaktari walivyokupima na hawajaona tatizo maana kama tatizo lisipoonekana hiyo inaitwa Dysfunction uterine bleeding (UDB) na kuna jinsi yake ya kutibu,ila mpaka kufikia kufanya diagnosis ya UDB ni lazima kuhakikisha kwa kina kabisa kwamba hakuna tatizo jingine linalosababisha damu kutoka.nakushauri uende muhimbili kuna magynecologist wazuri sana
 
Dada wakati unajipanga kwenda kwa madaktari bingwa wa akina mama ni wazi kwamba kwa sasa damu yako(Hb) ni ndogo sana.Na pia utakua unauambukizo wa bakteria(bacterial infection)
Cha kufanya ni kula vyakula vya kuongeza damu mf maharage,matembele,maini na matunda mf machungwa kwa wingi.
Njia mbadala ni kutumia dawa zifuatazo
1:sylate 500mg tds 5/7
2:primulut N 5mg tds 10/7
3:ferrous +folic capsules 1bd15/7

Kama ndani ya siku tatu hujaweza kuonana na daktari bingwa Basi nenda Pharmacy Kanunue Ceftriaxone injection na uende hospitali au dispensary ya karibu wakuchome 1gm od 5/7 wakupe na flagyl 400mg tds 7/7

Hizo dawa zitasaidia kukata damu kwa muda na kukuongezea damu wakati huo huo zikiua wadudu wanaoweza kuwa wanasababisha uambukizo!

N:B Tumia hizi dawa tu kama wewe si mjamzito na umeshindwa kumwona daktari kwa sababu yoyote haraka
Ni vizuri kwenda kwa madaktari bingwa ili wa rule out kama una uvimbe au imbalance ya vichocheo vya mwili
 
Dada wakati unajipanga kwenda kwa madaktari bingwa wa akina mama ni wazi kwamba kwa sasa damu yako(Hb) ni ndogo sana.Na pia utakua unauambukizo wa bakteria(bacterial infection)
Cha kufanya ni kula vyakula vya kuongeza damu mf maharage,matembele,maini na matunda mf machungwa kwa wingi.
Njia mbadala ni kutumia dawa zifuatazo
1:sylate 500mg tds 5/7
2:primulut N 5mg tds 10/7
3:ferrous +folic capsules 1bd15/7

Kama ndani ya siku tatu hujaweza kuonana na daktari bingwa Basi nenda Pharmacy Kanunue Ceftriaxone injection na uende hospitali au dispensary ya karibu wakuchome 1gm od 5/7 wakupe na flagyl 400mg tds 7/7

Hizo dawa zitasaidia kukata damu kwa muda na kukuongezea damu wakati huo huo zikiua wadudu wanaoweza kuwa wanasababisha uambukizo!

N:B Tumia hizi dawa tu kama wewe si mjamzito na umeshindwa kumwona daktari kwa sababu yoyote haraka
Ni vizuri kwenda kwa madaktari bingwa ili wa rule out kama una uvimbe au imbalance ya vichocheo vya mwili


Akitumia dawa hizo then akafa tutakuona wapi mzee?
 
Akitumia dawa hizo then akafa tutakuona wapi mzee?



Greater Thinker !!!
Jibu la papo kwa papo: Hizo dawa haendi kuchimba porini. Watakaomuuzia kama ni vilaza ndo watakuwa answerable <kama kweli zina madhara na zitathibitika kumfanya a-
sign off kula ugali>.
 
WanaJF, salaam! Mke wangu alijifungua kwa upasuaji nov 2010. Baada ya hapo alikaa kipindi cha mwaka na miezi 3 (miezi 15) bila kuona siku zake (hedhi). Tarehe 31 march mwaka huu, alianza kupata siku zake ambapo ameendelea ku-bleed kwa siku 12 mfululizo na bado anaendelea. (kabla hajajifungua, alikuwa ana-experience siku nne za hedhi). Je, nini ni chanzo? Na matibabu yake ni nini? Ukimwangalia kwa nje, hali yake ni nzuri na anafanya kazi zake kama kawaida. Naombeni msaada
 
Kuna possiblities kubwa mbili>>>
1. Iwapo wakati wa upasuaji kuna mabaki ya placenta ambayo hayasafishwa, yanaweza kusababisha hali hiyo.
2. Inawezekana kuna polyp (kiuvimbe) kimeota ndani au nje ya kizazi.

Nini cha kufanya>
1. Amuone daktari wa akina mama ili pamoja na mambo mengine amuandikie ultrasound.
2. Kizazi kisafishwe.
3. Anaweza kuchomwa sindano ya dawa za kusababisha kizazi kusinyaa na kukamua kilichomo (damu) mfano: Methyergometrine inection.

Nyongeza> Ukisikia damu inatoa harufu mbaya ni dalili ya infection. Ni muhimu mapema sana kupata matibabu ili infection isiharibu kizazi.
 
naukubali ushauri ila natoa Angalizo, uwezekano wa mabaki ya placenta( mf placenta acreta-placenta inayong'ang'ania) ni mdogo kwa sababu yangemletea matatizo mapema kwa sababu yangekuwa km foreign body, uwezekano wa polyp ni mkubwa, pia uvimbe wa tumbo(fibroid), nami nashauri aende hospitalini achukuliwe taarifa/history vizuri na vipimo stahiki, ultrasound muhimu.
Pia afanye haraka kwa sababu kutoka damu kiasi hicho ni hatari kwa afya yake
 
Anaweza kuwa na polysistic ovaries ama fibroids if not just hormones inbalance. Muhimu ni aonane na daktari wa wanawake amuone na kuzungumza nae, atajua vipimo vya kuanzia.

Awahi hospitali na kuachana na ushauri wa mitaani.
 
Ok. Hii imetokea baada ya miezi 10 ya kujifungua. Yaweza sababishwa na lipi kati ya hayo mana hapo awali haijawahi tokea.
 
Back
Top Bottom