Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Discussion in 'JF Doctor' started by Suzzie, Mar 3, 2009.

 1. Suzzie

  Suzzie Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nilichoma sindano ya kuzuia mimba January 13, na ilipofika february 13 nikaanza bleed, kwa kawaida huwa naenda mpaka siku 5, lakini kuanzia tarehe february 13 mpaka hivi sasa bado ninableed. hakika nimechanganyikiwa. naomba ushauri wenu nifanyaje?
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ni vizuri uende hospitali ukaonane na wataalamu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 60,424
  Likes Received: 39,977
  Trophy Points: 280
  Nenda ukawaone madaktari haraka sana. Haya madawa ya kuzuia mimba mengi yana side effects inabidi uzisome kwa uangalifu sana na kuuliza maswali mengi kwa wataalam kabla ya kuamua ni ipi inayofaa kutumia.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,782
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  > Wahi hospitali Dada -- Preferably Marie Stopes -- hawa wana ujuzi na mambo ya birth control.

  > Wengi hapa Jamvini ni Wanasiasa, Wachumi na Wa-IcT, of course na Ma-Engineer. Ma-Gyno ni wachache mno hapa!
   
 5. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sure Mkuu,
  hata mimi niliwahi kuuliza maswali ya kiafya sikupata hata jibu moja. Yaelekea humu wengi ni wanasiasa (of coz kila mmoja ni mwanasiasa) na wahandisi, wahandishi, ... hata wahandisi wenyewe hawataki kujibu maswali ya kihandisi .... ukiuliza kitu cha kitaalamu wanakuingizia siasa mpaka mjadala unabadilika...
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  Hi

  Nadhani hiyo ni kawaida maana hizo dawa huingiliana na hormonal balance, nakushauri uende ukaonane na gynacoelogist otherwise niPM....
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,864
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Mzee KunguruMweupe ndo mtaalamu hapa wa mambo ya kina mama!

  Uko wapi?

  Unahitajika huku!
   
 8. D

  Dotori JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Suzzie,
  Ku-bleed kunasababishwa na mambo mengi ikiwa pamoja na mabadiliko ya hormone (hormonal imbalance).
  Nakushauri uwasiliane na Daktari wa kinamama ili akupime na kukupa matibabu sahihi.
  Lakini kwa majibu ya haraka haraka, tatizo lako linaweza kuwa linatokana na hizo sindano unazotumia.

  Kuhusu kuendelea kutumia sindano hizi au la, daktari anaweza kukupa maelezo mazuri zaidi.

  Natumai maelezo haya yamekusaidia.
   
 9. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbona kuna daktari katoa thread ataka kujibu maswali! https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/9373-leteni-maswali-ya-kiafya-niwasaidie.html

  Na kuna vitu vya kuuliza jf, kama mengine ni obvious unatakiwa upige hodi kituo cha afya- bleeding!
   
 10. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Dada SUZZIE, hiyo ni side effect (SE) ya contraceptive uliiyoitumia (DEPO-PROVERA), mabadiliko ya mentrual cycle ni commonest SE kwa hiyo contraceptive, wengine hawapati kabisa damu kwa kipindi chote wanapotumia hiyo dawa, na wengine kama wewe wanapata prolonged/irregular mentrual bleeding, nakushauri uonane na GYNAECOLOGIST.
   
 11. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Muone daktari (gynaecologist) wa magonjwa ya wanawake haraka. Pole sana.
   
 12. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2009
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kamuone Daktari wa Gynae haraka sana!!! Usipoteze muda hata kidogo.
   
 13. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi si daktari lakini nina uzoefu kidogo kuhusu hilo. Ni suala la kawaida unapoanza kuchoma sindano kwa mara ya kwanza. Kwa wanawake wengi huwa siku unakuwa huziona kabisa. Lakini kwa wachache ndio hivyo tena unakuwa unaziona mfululilizo. Inaweza kuwa mwezi mmoja au miwili halafu inakatika. Hii ni katika miezi mitatu ya kwanza ya kutumia. Baadaye mwili unazoea na unarudi katika hali ya kawaida. Mwaka mmoja baada ya kuzoea kutumia sindano siku huwa zinakuwa chache(mara nyingi moja) na nyepesi kabisa. Hata kwa wale ambao mara ya kwanza ilikuwa mfululizo. Lakini ni vyema ukamuona daktari wako akakupa ushauri zaidi kama mwezi wa pili ukipita na hali ikawa hivyo hivyo. Na hata ukiacha, utarudi kwenye hali ya kawaida baada ya miezi miwili mpaka mitatu mpaka hizo homoni ziishe mwilini. Na kurudi mpaka kuweza kushika ujauzito huchukua miezi 6 mpaka 8; kwa wachache miaka miwili.

  Asha
   
 14. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu utakumbuka kuwa AVATAR ya huyo daktari ilikuwa inatisha na by itself ilizua mjadala ... isitoshe hata yeye nilimwuliza hilo swali hakuwahii kujibu. Unajua hata hizi avatar tunazotumia zinahashiria mhusika ni mtu wa aina gani .... mfano ukicheki ya kwangu utagundua kuwa mimi ni mtu anaependa vitu gani....
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  shekhe
  tupo magnyo hapa wa ndoa za watu mkuu pamoja na mabinti bikra.

  Namshauri Outlier kama yupo dar aende aghakhani watampatia huduma ya fasta maana maria stopes mh! utata mtupu
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,969
  Likes Received: 891
  Trophy Points: 280
  Out of curiosity...what qualications do you have and what assistance were you looking for?
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  HUO UTAFITI UMEUFANYIA WAPI? Mimi ni wa fani gani kama unatabiri?

  Hujamwona `mwanakijiji halisi` humu ndani? Ningekusupport ungesema

  kuwa may be wengi ni Journalists na Kanjanjas. Hahahaaaa!!!!

  Dadaandu, cha kufanya kwa haraka ni kuwahi hospital kama wengi

  walivyosema. Hata wenye fani hiyo watakuwa na msaada mdogo kupitia

  jamvi hili, coz u have to be physically examined of your uteral functioning.
   
 18. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,497
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Forum: JF Doctor 3rd March 2009, 04:06 PM
  Replies: 16 Bleeding: Jamani nisaidieni
  Views: 411 Posted By Suzzie
  Bleeding: Jamani nisaidieni

  Nilichoma sindano ya kuzuia mimba January 13, na ilipofika february 13 nikaanza bleed, kwa kawaida huwa naenda mpaka siku 5, lakini kuanzia tarehe february 13 mpaka hivi sasa bado ninableed. hakika...


  Suzzie, hii hali yako ya bleeding ulii-post tarehe 3 March, sasa embu tuambie kama bado una-bleed mpaka sasa hivi au tatizo limeshakuwa solved.
   
 19. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole Suzie,
  Sio kweli kwamba humu wamejaa Engineers,politiki men etc,mimi nimewahi kusaidiwa sana na Complications kubwa sana,msiwakatishe moyo wanaosaidia. Jamani mtu kama anahitaji msaada si lazima awaulize ndugu zake?hata kama sio ma dakatari watampa ushauri kama wengi hapo juu mlivyofanya? Na wengi wali ni PM.
  Suzie uko wapi kama ni US au Tanzania naweza kukupa ushauri wa haraka.
   
 20. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole Suzie,
  Sio kweli kwamba humu wamejaa Engineers,politiki men etc,mimi nimewahi kusaidiwa sana na Complications kubwa sana,msiwakatishe moyo wanaosaidia. Jamani mtu kama anahitaji msaada si lazima awaulize ndugu zake?hata kama sio ma dakatari watampa ushauri kama wengi hapo juu mlivyofanya? Na wengi wali ni PM.
  Suzie uko wapi kama ni US au Tanzania naweza kukupa ushauri wa haraka.
   
Loading...