Nilijitoa kufanya naye maisha ila ameniachia wakati mgumu nikiwa na mimba yake

Mfalme Daudi

Senior Member
Dec 23, 2011
110
245
NAANDIKA KWA NIABA YA DADA YANGU MMOJA MUHANGA ANAYEPITIA HILI,NIMEONA NISHEE ILI KUPATA USHAURI WA PAMOJA JINSI YA KUMSAIDIA.

Tulikutana Facebook na ni Mwaka wa nne sasa tangu tufahamiane,alikua akisoma chuo Songea ila kwao ni Dar. Tukaanza urafiki na kuwa wapenzi, akamaliza chuo wakati huo nikiwa nimeajiriwa kwenye hotel Mirerani Manyara. Baada ya kumaliza akawa hana kazi, nikampambania akapata kazi duka moja la nguo akaja Arusha akawa akifanya kazi huku anaishi kwa Uncle wangu.

Akasema ile kazi haiwezi anahitaji kufanya kazi aliyosomea(Alisomea Ualimu). Nikampambania akapata kazi shule fulani iko hapa Arusha nje kidogo ya mji. Akafanya ile kazi kwa mwaka mzima tukawa tuko vizuri kidogo kimaisha,akaondoka kwa uncle akapanga nyumba akaanza kujitegemea, nikawa nikipata nafasi naenda nakaa siku 2, narudi kazini.Kuna Mkopo nilikopa kama laki 8, akaniongezea nikanunua kiwanja huko ngaramtoni nikaandika kwa jina langu mwanzo na la kwake mwisho.

Nikaweka tumaini langu kwake nikiamini ndio mwanaume wa maisha,nikampeleka nyumbani kumtambulisha kwa mama akawa anajulikana,ila mimi skuwahi wajua familia wala ndugu zake aliniahidi siku moja tungesafiri kwenda kwao kunitambulisha.

Tukaanza fanya mambo ya kimaendeleo,sehemu niko hamna umeme Nikamwambia nataka kufunga sola za mkopo akanipa hela nikaenda chukua ya 2M na Laki 6 unalipa kwa mwaka mmoja na nusu nikawa naonesha mpira kwa kutoza kiingilio,nikafungua na mgahawa mdogo nikaacha kazi niliyokua nafanya nikawa nimejiajiri mwenyewe,kiukweli tulikua vizuri.

Mwaka Jana mwezi wa 10 nikapata msiba Mwanza nikasafiri nikakaa kule kama mwezi. Kurudi mwenzangu nikawa kama simuelewi,kabadilika akaniambia ''Mi Nataka Mtoto'',Kwakuwa nilikua nampenda na tulishaanza kufanya maisha nikamwambia hilo halina tatizo sababu nilimwona ni Mwanaume anayejali na sikua na shaka juu ya hilo.

Nikabeba mimba,nilipomwambia akaanza kubadilika kitabia akawa simu anapiga kwa siku mara moja au asipige kabisa. Nikachunguza nikagundua tayari alikua ashapata mwanamke mwingine.

Kuna siku akaja kwangu akaniambia anataka kusafiri aende kwao nikamwambia sawa,kumbe aliiba ile hati ya kiwanja akaenda kukiuza. Akanitumia tu massage ''kanipa zawadi ya mtoto'' nikaanza kumtafuta sikumpata hewani, ile shule aliyokua anafundisha nikaenda wakaniambia alishaacha kazi,mpaka sasa sijui aliko.

Kinachonichanganya zaidi ameniacha na Mimba ya miezi 6 mpaka sasa, nina madeni ya kulipa kuanzia lile la sola nalipa kwa siku 3600/-Tsh na rejesho la ule mkopo wa laki 8, nalipia kila jumatatu 38,000/-Tsh natakiwa kulipa kodi ya chumba nakaa 40,000/Tsh na frem ya ule mgahawa nilifungua Mimba inaenda mwezi wa 7 sasa, sina akiba yoyote ndani,Mama yangu anaumwa na ananitegemea mtaji umekata, Mpaka sasa nimechanganyikiwa nashindwa la kufanya! Naomba ushauri wa kimawazo nifanye nini?
 
Duuh polee sana jitaid kumuomba Mungu kwa ili na punguza gharam za maisha tafuta chumba sehem nyingne kwenye bei chee au rud kwenu tu
Tulikutana Facebook na Ni Mwaka wa nne sasa tangu tufahamiane,alikua akisoma chuo Songea ila kwao ni Dar. Tukaanza urafiki na kuwa wapenzi,akamaliza chuo wakati huo nikiwa nimeajiriwa kwenye hotel Mirerani Manyara.Baada ya kumaliza akawa hana kazi,nikampambania akapata kazi duka moja la nguo akaja Arusha akawa akifanya kazi huku anaishi kwa
 
Kwenye miti hamna wa jenzi ninge kua na mwana mke mpanbanaji kama wewe sasa hivi billionia, ila usijali atarudi kumuona mwanae jipe mwoyo pambana pata mme mgine ila usiwekeze pesa kwake tena hilo liwe somo kwako
 
Mahusiano ya saivi dada ni kuwa na exit plan mapema sana, asikudanganye mwanamme sijui umzalie ndio akuoe, utapigwa na lifatuma kichwani. Mbaya zaidi uko ndani ya mkenge huu ushauri wangu hauwezi kukusaidia.

Cha kufanya ni kupambana tu, jikung'ute vumbi simama songa mbele... Trust me atakuja siku moja akutafute kama anapajua kwenu ipo siku atakuja kukulilia na kusingizia ni shetani alimpitia.

Mimba sio kilema kama wazazi wako wapo wazima wambie hio scenario, wao wameyaona mengi kama hayo watakusaidia tu.

WANAUME TUSIUMIZE WADADA KAMA HAWA WANAOJITOA KWETU NI NADRA KUWAPATA
 
Tulikutana Facebook na ni Mwaka wa nne sasa tangu tufahamiane,alikua akisoma chuo Songea ila kwao ni Dar. Tukaanza urafiki na kuwa wapenzi, akamaliza chuo wakati huo nikiwa nimeajiriwa kwenye hotel Mirerani Manyara. Baada ya kumaliza aka
Kwa hakika Mungu atunusuru, Miaka minne hupajui kwao au unakubakubeba mimbahujui ndugu wa mwenza hata moja!!!
 
Dah kwanza machoz yamenitoka niliposoma hii post.iv sis wanaume tunafel wap umepata mtu mpambanaji namna hii afu unafanya unyama huu iv kweli wewe zinakutosha?.maskini dada wa watu kauweka moyo kwako afu unamfanyia hivi,pole sana aise
 
Tulikutana Facebook na ni Mwaka wa nne sasa tangu tufahamiane,alikua akisoma chuo Songea ila kwao ni Dar. Tukaanza urafiki na kuwa wapenzi, akamaliza chuo wakati huo nikiwa nimeajiriwa kwenye hotel Mirerani Manyara. Baada ya kumaliza
Sola ya Kampuni gani ulikopa? Kama ni Mobisol siku hizi wanajiita Mysoul njoo inbox nikupe ujanja ili uache kulipia,uiuze na hawatakufanya lolote, namaanisha hawana uwezo wa kukushtaki mahali popote
 
Watu wengine wanabahati yakupata wanawake wapambanaji namna hii afu mtu anafanya ujinga.wanasema mpende mwanamke anaekupenda sio unaempenda
Kwenye miti hamna wa jenzi ninge kua na mwana mke mpanbanaji kama wewe sasa hivi billionia, ila usijali atarudi kumuona mwanae jipe mwoyo pambana pata mme mgine ila usiwekeze pesa kwake tena hilo liwe somo kwako
 
Sola ya Kampuni gani ulikopa??kama ni Mobisol siku hizi wanajiita Mysoul njoo inbox nikupe ujanja ili uache kulipia,uiuze na hawatakufanya lolote,namaanisha hawana uwezo wa kukushtaki mahali popote
Aise afazali ulikuepo umpe elimu ili kumpunguzia stress wanaume wengine sijui tunafel wap
 
Mahusiano ya saivi dada ni kuwa na exit plan mapema sana, asikudanganye mwanamme sijui umzalie ndio akuoe, utapigwa na lifatuma kichwani. Mbaya zaidi uko ndani ya mkenge huu ushauri wangu hauwezi kukusaidia.

Cha kufanya ni kupambana tu, jikung'ute vumbi simama songa mbele... Trust me atakuja siku moja akutafute kama anapajua kwenu ipo siku atakuja kukulilia na kusingizia ni shetani alimpitia.

Mimba sio kilema kama wazazi wako wapo wazima wambie hio scenario, wao wameyaona mengi kama hayo watakusaidia tu.

WANAUME TUSIUMIZE WADADA KAMA HAWA WANAOJITOA KWETU NI NADRA KUWAPATA
Kidogo nipasuke kwa kucheka eti 'lifatuma kichwani'! Dah.
 
Back
Top Bottom