Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Jaman polee Ashuraa,but mume wako ndo ufuate ushauri wake haswaaaa...
unamaanisha nini mkuu? Huyu binti anahitaji ushauri wa kitaalam na amekuja ktk jukwaa husika ambalo kuna wataalamu wa matatizo tofauti, ni vipi kama mme wake ni mfanya biashara atampa ushauri gani kuhusu tatizo alilopata? Au wewe ni mtaalam wa kila kitu ktk ulimwengu huu? Hata hospitali pia unaweza kupata ushauri na si kila wakati ni madawa na sindano.
 
Nakuomba kwa Mungu wetu, Yehova Rafa, Mungu atuponyaye, nawe utarudia katika hali yako ya kawaida.
Amini kwamba kuanzia sasa umekuwa mzima katika Jina la YESU, BWANA na MWOKOZI wa DUNIA YOTE. Amin
 
Dr
Hutokea mara nyingi kima mama na wasichana kuwa na kipindi cha msongo wa mawazo pale wanapokosa siku zao na hasa kama hawakutumia njia ya uzazi wa mpango au kinga nyingine ya kushika mimba.

inasemekana Kukosa siku zao sio dalili pekee ya kushika mimba

swali langu ni kuwa "Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama mwanamke hana mimba?" kwa mfano mwanamke kapitiliza labda siku 5 bila kuona hedhi nalo hilo laweza kuwa ni dalili mojawapo ya kuwa na ujauzito?

nipeni majibu wataalam
 
Wakati mwingine hata matumizi ya sindano, vidonge, vipandikizi vya kuzuia mimba yaweza kuwa sababu moja wapo.
 
Hiyo inatokana na mfumo wa vichocheo kubadilika .

Wakati mimba haijatunga vichocheo hufanya kazi ya kitayarisha mirija ya fallopia na nyumba ya uzazi kuanza kuandaliwa kwa ajili ya fertilization (kwenye Fallopian tubes) na kusafiri hadi nyumba ya uzazi(uterus).Mojawapo ya kazi kubwa ya vichocheo ni kuandaa mazingira katika uterus kwa ajili ya kupokea tokeo la fertilization(embryo)kwa ajili ya implantation na kuendelea na hatua zngine za ukuaji hadi miezi 9.

Sasa fertilization isipotokea layer ya damu ambayo iliyoongezeka kwa ajili ya kupokea embryo kwenye uterus hutoka nje kama hedhi.

Kama imetokea ferilization na implantation ,layer ya damu katika uteus haitoki kwa kuwa inahitajika kwa ajili ya ku accomodate embryo ,kwa hivyo huwezi kuona siku za mwezi, hedhi.

Mabadiliko haya husababishwa na vichocheo.
 
Nakushukuru kwa ufafanuzi sasa nimeelewa,ila bado kunakitu kinanisumbua mpaka sasa,kwa mfano unakuta siku mwanamke aliyotegemea kupata hedhi kwa mfano ni tareh 15 lakini inapitiliza labda kwa siku nne mbele ama tano,je kunauwezekano wa kuwa na ujauzito ama ni vichocheo ndio vinasababisha hayo?
 
Kupiliza kwa hedhi katika hali ya kawaida inaweza kusababishwa na huu mfumo wa vichocheo kubadilika.
Mabadilko haya huweza sababishwa na msongo wa mawazo.

Hata hivyo fertization huweza kutokea kama kawaida lakini implantation ikashindika kutokana na sababu kadhaa, mfano matayarisho hafifu ya mji wa mimba(uterus)ambayo pia huweza sababishwa na irritation ktk uterus na baadhi ya contraceptives au infection au upungufu wa vichocheo kwa ajili maintenance ya embryo katika uterus.Yaani ni kama kuna kani mbili ya kwanza inayoifanya embryo ibaki katika uterus na ya pili ni ile inayoing'oa.Kani hizi ni matokeo ya vichocheo.
Sasa kama kani ya pili imezidi basi inatokea spontaneous abortion na embryo huweza kutoka pamoja na damu na hivyo mhusika asigundue kama alishika mimba na imetoka ,lakini anafikiri kuwa hedhi imechelewa
 
Husababishwa na vitu vingi mfano lishe bora,kunywa Maji ya kutosha,mazoezi na msongo wa mawazo. Kama kinga haikutumika wakati wa kujaamiana ni wazi kwamba itakusababishia mawazo na wasiwasi navyo hupelekea kuchelewa kupata period.(Huwa inacheza na saikoloji ya mwanamke) beleave or not
 
Nashukuru kwa kweli,sasa nipo huru kwenda kujibu maswali niliyoulizwa,maana uiengineer na haya mambo ni tofauti ila kwa kuwa ninawataalam hapa jf basi acha nirudishe majibu kwa wahusika
 
Wana JF naomba msaada wenu nina binti yangu ana tatizo la kupata hedhi bila mpangilio, kuna wakati anasimama miezi mitatu bila kuona siku zake, then anapata. Anaweza kubleed hadi siku kumi na moja. anapumzika wiki mbili anableed tena for many days hata week mbili. Kwangu hili limekuwa ni tatizo mno kwani binti anakuwa mgonjwa sana na hata anaonekana kuishiwa damu na pia anasumbuliwa na maumivu ya tumbo na kizunguzungu.
Naomba msaada wenu
 
Ni tatizo la hormones tu, balance ya hormones ni tatizo linalowapata mabinti wengi hasa pindi wanapoanza hedhi na hata wamama wanapokaribia kukoma hedhi. Huwa wanapata unovulatory cycles ambazo huambatana na mzunguko usio wa kawaida (menstrual irregularities) ni vema kwenda kwa wataalamu watamsaidia.
 
Madaktari hamjambo?ni mwezi wa 6 damu ya hedhi inatoka bila kuacha.nini dawa yake.nimeshahangaika hospitali mpaka nimechoka wanasema hawaoni kitu chochote.tafadhali niambeni jina la dawa inayotiau matatizo haya.damu inakuwa nzito kiasi.msaada jamani.hasa wa dawa
 
Sio kila damu itokayo uukeni ni hedhi. Jaribu kufanya kipimo che HORMON ESSAY. Muone Gyenacologist akufanyaie proper examination. Sababu ziko nyingi sana na huwezi mtu akatoa proper diagnosis bila ya proper examination.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom