Nini kiliua safari za moja kwa moja za mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines na Lufthansa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Mambo vp jamiiforums.

Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flight) za kuja Tanzania kwa mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines System (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe mwenzao KLM bado anakujaga?
==========
aswsderfdeswqasdfgt.jpg

==========
Jana nikiwa nimepaki gari yangu (Taxi Bubu) hapa kijiweni nilipigiwa simu kwenda kuchukua abiria mmoja pale uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere (JNIA) alikuwa anatokea hukoooo majuu.

Sasa wakati ninasoma vijarida kadhaa pamoja na kupiga stories na abiria pamoja na ndugu waliokuja kupokea wenzako pale sehemu ya kusubiria, nikajifunza mambo yafuatayo.

Kuna njia mbili tu za moja kwa moja kutoka Ulaya hadi Tanzania kwa njia ya ndege. Kwanza kuna KLM (Royal Dutch Airlines) ambayo huruka kila siku kuja Dar es Salaam kutoka Amsterdam nchini Uholanzi.

dfgtgfrty.jpg

Njia ya pili ni kupitia shirika la ndege la Uturuki kutoka Istanbul uwanja wa ndege wa Ataturk. Vinginevyo wasafiri kutoka Ulaya wanaweza kupanda ndege kwenda Nairobi. Halafu Kenya Airways inakujaga karibia kila siku huku Dar/Tanzania.

Mashirika yanayokwenda Nairobi ni pamoja na British Airways kutoka London Heathrow; Air France kutoka Paris; Swiss Air kutoka Zurich; Brussels Airlines kutoka Brussels nchini Ubelgiji; Lufthansa kutoka Frankfurt; na Kenya Airways kutoka London Heathrow au Amsterdam.

Kwa ujumla, Shirika la Ndege la Kenya huchukua chini ya masaa tisa usiku mzima kutoka London hadi Nairobi, ambayo inaunganisha kufika Dar es Salaam.

Ikiwa unataka kuja Dar es Salaam, basi vinginevyo unaweza kuunganisha kupitia Cairo na Egypt Air; kupitia Dubai na Emirates; kupitia Abu Dhabi na Etihad Airways; kupitia Addis Ababa na Shirika la ndege la Ethiopia.

sdededfrdcvf.jpg

Pia abiria anaweza kupitia Muscat na Oman Air; au kupitia Doha na Qatar Airways. Baadhi ya mashirika haya ya ndege pia yana njia zinazoingia Kilimanjaro na Zanzibar.

SWALI LANGU: Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flights) za mashirika ya ndege ya Ulaya kama kama Scandinavian Airlines (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe KLM bado anakuja Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mara nyingi ndege uvunja route kama inaonekana hakuna abiria wa kutosha kwenye hiyo route. Baada ya vulu-vulu zilizotokea hapa katikati hatuna uwekezaji mkubwa kutoka Ulaya na sisi kiwango cha biashara tunachofanya nao ni kdogo sana hivyo kuto-attract movement kubwa ya vitu na watu.

Hapa Tanzania ni watu wachache wanaweza ku-afford products za Ulaya, wengi tunajisalimisha kweye mediocre stuff from Asia. Wazungu wa Ulaya wanaokuja huku sanasana ni utalii ambao pia kwenye destination hiyo bado tunajikongoja, ingawaje Zanzibar wanafanya vizuri ku-attract Wazungu wa Ulaya.
 
Biashara yoyote ni kutokana na mahitaji ya soko kwa kipindi fulani.. Mabadiliko hutokea ambayo huathiri watoa huduma wengine katika soko...

Lufthansa ni shirika walilokuwa wanatoa usafiri kwenda Ujerumani na SAS wanakwenda Geneva, Switzerland.. Sasa hivi wana ushindani mkubwa toka kwa Qatar (Doha) Emirates (Dubai) na Ethiopia Airline (Addis Ababa) hizi nchi zote, zinatoa connection kwa abiria wanaowasili na ndege toka maeneo mbalimbali na kuwapa connection za kwenda Ujerumani, Uswisi, Ulaya, Marekani nk. Kwa maana nyingine haya mashirika yamechukua biashara zao kwa vile sokoni inaonekana ni bora kupitia hizo sehemu. Sasa ukisema uende Geneva na Swiss Air. Mtu anazunguka pasipo sababu wakati anaweza kuunganisha safari kiurahisi toka maeneo hayo.

Vile vile kuna mambo mengine ya kibiashara kama shopping consideration - Dubai / Qatar na hata kiwango fulani Addis Ababa wana duty free shops nzuri, ambazo zinawavutia returning residents wa nchi mbalimbali kupendelea kununua bidhaa katika airports hizo, wakati wakiwa wanarudi nyumbani / makwao sehemu mbalimbali.
 
mara nyingi ndege uvunja route kama inaonekana hakuna abiria wa kutosha kwenye hiyo route. Baada ya vulu-vulu zilizotokea hapa katikati hatuna uwekezaji mkubwa kutoka Ulaya na sisi kiwango cha biashara tunachofanya nao ni kdogo sana hivyo kuto-attract movement kubwa ya vitu na watu.
Very convincing...
 
mara nyingi ndege uvunja route kama inaonekana hakuna abiria wa kutosha kwenye hiyo route. Baada ya vulu-vulu zilizotokea hapa katikati hatuna uwekezaji mkubwa kutoka Ulaya na sisi kiwango cha biashara tunachofanya nao ni kdogo sana hivyo kuto-attract movement kubwa ya vitu na watu.

Hapa Tanzania ni watu wachache wanaweza ku-afford products za Ulaya, wengi tunajisalimisha kweye mediocre stuff from Asia. Wazungu wa Ulaya wanaokuja huku sanasana ni utalii ambao pia kwenye destination hiyo bado tunajikongoja, ingawaje Zanzibar wanafanya vizuri ku-attract Wazungu wa Ulaya.
Hayo mashirika yalivunja safari zake nyingi wakati wa utawala wa Mkapa wala siyo kwa sababu ya vulu-vulu za uwekezaji bali sababu kubwa ilikuwa ni huduma mbovu za uwanja wa JKN. Uchache wa abiria haikuwa factor kubwa kwani BA49 ilikuwa inakuja Dar via Nairobi, na enzi za Lufthansa ilikuwa inajaa sana kutokea Dar kwenda Frankfurt kiasi kuwa haikuwa na tatizo la abiria kabisa.
 
Hii ni orodha ya mashirika yaliyokuwa yanatua Dar na sasa yameacha:
1. PIA (Pakistani International Airlines)
2. SAS (Scandivian Airline Systems)
3. Luthfansa
4. British Airways
5. Aeroflot (Mrusi)
6. Air France (ilikuwa inakuja ile Boeng 747 yenye kigorofa)
7. Gulf Air (Bahrain)
9.
10.
 
Mkuu, kama hii ndio sababu basi tutegemee hayo mashirika kurudi kwa maana sasa kuna TERMINAL III pale JNIA...
Unfortunately kuvunja uhusiano huwa ni rahisi sana lakini kuujenga upya ni kugumu sana.

Uzuri wa uwanja kwa macho ya mashirika ya ndege siyo ule uzuri wa majengo ya terminal, wao wanaangalia mambo kama usalama wa ndege zao na huduma ambazo ndege zao zinapata zinapokuwa pale airport. Mambo hayo hayaletwi na ufunguzi wa jengo la terminal 3. Sababu kubwa ya Lufthansa kusitisha safari zake ilikuwa ni kuwa kuna wakati walikuwa wan-land usiku (alfajiri sana) huku hakuna taa za kutosha uwanjani. Uwanja utakamilika tu utakapokuwa na taa za kutosha na vile vile kuwa na automatic landing system (ALS) infrastructure!!
 
Mambo vp jamiiforums.

Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flight) za kuja Tanzania kwa mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines System (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe mwenzao KLM bado anakujaga?
==========
View attachment 1727879
==========
Jana nikiwa nimepaki gari yangu (Taxi Bubu) hapa kijiweni nilipigiwa simu kwenda kuchukua abiria mmoja pale uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere (JNIA) alikuwa anatokea hukoooo majuu.

Sasa wakati ninasoma vijarida kadhaa pamoja na kupiga stories na abiria pamoja na ndugu waliokuja kupokea wenzako pale sehemu ya kusubiria, nikajifunza mambo yafuatayo.

Kuna njia mbili tu za moja kwa moja kutoka Ulaya hadi Tanzania kwa njia ya ndege. Kwanza kuna KLM (Royal Dutch Airlines) ambayo huruka kila siku kuja Dar es Salaam kutoka Amsterdam nchini Uholanzi.

View attachment 1727881

Njia ya pili ni kupitia shirika la ndege la Uturuki kutoka Istanbul uwanja wa ndege wa Ataturk. Vinginevyo wasafiri kutoka Ulaya wanaweza kupanda ndege kwenda Nairobi. Halafu Kenya Airways inakujaga karibia kila siku huku Dar/Tanzania.

Mashirika yanayokwenda Nairobi ni pamoja na British Airways kutoka London Heathrow; Air France kutoka Paris; Swiss Air kutoka Zurich; Brussels Airlines kutoka Brussels nchini Ubelgiji; Lufthansa kutoka Frankfurt; na Kenya Airways kutoka London Heathrow au Amsterdam.

Kwa ujumla, Shirika la Ndege la Kenya huchukua chini ya masaa tisa usiku mzima kutoka London hadi Nairobi, ambayo inaunganisha kufika Dar es Salaam.

Ikiwa unataka kuja Dar es Salaam, basi vinginevyo unaweza kuunganisha kupitia Cairo na Egypt Air; kupitia Dubai na Emirates; kupitia Abu Dhabi na Etihad Airways; kupitia Addis Ababa na Shirika la ndege la Ethiopia.

View attachment 1727882

Pia abiria anaweza kupitia Muscat na Oman Air; au kupitia Doha na Qatar Airways. Baadhi ya mashirika haya ya ndege pia yana njia zinazoingia Kilimanjaro na Zanzibar.

SWALI LANGU: Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flights) za mashirika ya ndege ya Ulaya kama kama Scandinavian Airlines (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe KLM bado anakuja Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Miaka ya utotoni, baba alikuwa jumapili zingine jioni , alikuwa anatupeleka Uwanja ndege, enzi hizo unaruhusiwa kupanda kule juu
tulikuwa tunakaa mpaka usiku, tunahesabu ndege zinazotua na kupaa

Kufa kwa hizi safari ni kwa sababu ya ushindani kutoka kwa mashirika ya nchi za kiarabu, nauli za ndege za ulaya zilikuwa ni kubwa sana kulinganisha na Gulf Air, Egpty Air, baadae Emirates na Qatar Air hata Oman Air.

Ikawa hata wazungu wenyewe hawapandi ndege zao kuja Africa na Asia, au kwenda Australia, mimi nilikuwa na wazungu kibao kutoka UK kwenda transit za arab country na wanakwambia wanaeenda Thailand au Africa for holiday lakini hawapandi ndege za nchi zao sababu ya nauli kubwa.

Kwa Tanzani ikawa vigumu kwa european country kuleta ndege zao wakati Qatar na Emirates zipo ndege kutoka nchi zao kila siku
Kwa ujumla hizi ndege za Arab country pia zilichangia kufa kwa mashirika makubwa kama SABENA
 
Mkuu hIzo ndege za kiarabu zinatua na kenya pia , na mashirika ya ndege ya ulaya bado yapo.

Sera mbovu za nchi yetu ndio zimepelekea ndege hizi kuacha kuja Tanzania, walilalamika gharama kubwa za airport handling, abiria walipopungua ndo ikawa sababu pia. Kuna muda ilikuwa ni rahisi kupanda ndege Kenya kwenda ulaya kuliko Dar.
 
Miaka ya utotoni, baba alikuwa jumapili zingine jioni , alikuwa anatupeleka Uwanja ndege, enzi hizo unaruhusiwa kupanda kule juu
tulikuwa tunakaa mpaka usiku, tunahesabu ndege zinazotua na kupaa

Kufa kwa hizi safari ni kwa sababu ya ushindani kutoka kwa mashirika ya nchi za kiarabu, nauli za ndege za ulaya zilikuwa ni kubwa sana kulinganisha na Gulf Air, Egpty Air, baadae Emirates na Qatar Air hata Oman Air
ikawa hata wazungu wenyewe hawapandi ndege zao kuja Africa na Asia, au kwenda Australia, mimi nilikuwa na wazungu kibao kutoka UK kwenda transit za arab country na wanakwambia wanaeenda Thailand au Africa for holiday lakini hawapandi ndege za nchi zao sababu ya nauli kubwa.

Kwa Tanzani ikawa vigumu kwa european country kuleta ndege zao wakati Qatar na Emirates zipo ndege kutoka nchi zao kila siku
Kwa ujumla hizi ndege za Arab country pia zilichangia kufa kwa mashirika makubwa kama SABENA
Pia walikuwa wanatuletea madege ya zamani.

Waarabu walipokuja wakawa wanaleta ndege mpya kwa kuwa yalikuwa ni mashirika mapya. Mashirika ya ulaya yakashindwa kushindana, huku wakilalamika ndege za waarabu zinashindana unfairly kwa kuwa wanapata mafuta bure kutoka serikali zao.
 
Mkuu hIzo ndege za kiarabu zinatua na kenya pia , na mashirika ya ndege ya ulaya bado yapo
Sera mbovu za nchi yetu ndio zimepelekea ndege hizi kuacha kuja Tanzania , walilalamika gharama kubwa za airport handling, abiria walipopungua ndo ikawa sababu pia .kuna muda ilikuwa ni rahisi kupanda ndege kenya kwenda ulaya kuliko Dar.
  • Sera mbovu za nchi kama zipi mkuu?
  • Kenya walituzidi kidogo kwa sababu sisi tuliweka uchumi wetu rehani kwa kuwakomboa Waganda wao (Wakenya) hawakuwa na roho hiyo ya upendo.
 
Back
Top Bottom