Nini kilikufanya ugundue Umri umeenda?

Nini kilikufanya ugundue Umri umeenda?

Ha ha ha niliingia ofisi ya Tanesco wamama ofisi nzima wananiamkia huku wakiwasihi wafanyakazi wengine 'HEBU MSIKILIZENI BABA ANA SHIDA GANI' Yaani mimi nawaona pisi kali wao wananiona baba duh!
šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€Unajiuliza wananiambia mimi au kuna mtu nyumayangu au
 
Pale mama ambapo alinipigia simu, hakuniomba hela ila alinambia....
Emily magnus yaani sina hata chumvi ngoja nikakope....

Nikajua....
 
Siku nyingine nimemsindikiza Rafk angu kutafuta shule ya watoto, Mwalimu wa Taaluma akawa anatukaribisha pale ety "Karibuni ofisini Wazazi " Nikapata shock kua kumbe naonekana kama mzazi šŸ˜€
 
Siku nyingine nimemsindikiza Rafk angu kutafuta shule ya watoto, Mwalimu wa Taaluma akawa anatukaribisha pale ety "Karibuni ofisini Wazazi " Nikapata shock kua kumbe naonekana kama mzazi šŸ˜€
Hahaha ko kuitwa tu mzazi ukaogopa? Kuna wale wanaozaa wakiwa na umri mdogo probably 17 yrs, ko hao wakiitwa wazazi watakuwa wamezeeka
 
Kuna muda mtu unakuwa na mambo mengi hadi unasahau kama upo kwenye "Age go" unaongeza miaka ila ni kama unajiona bado mdogo tu mpaka ukutane na jambo fulani ndio unastuka kumbe umri wangu ushaenda hivyo.

Kuna wengine ongezeko la shikamoo ndio linawastua wengine kuitwa kwneye vikao vya ukoo nk.

Kipi kilikufanya ujue umri ushakutupa mkono?
Ukishafika 35+ jua kabisa maji kupwa ,maji ya jioni ,jua linazama.
 
Hahaha ko kuitwa tu mzazi ukaogopa? Kuna wale wanaozaa wakiwa na umri mdogo probably 17 yrs, ko hao wakiitwa wazazi watakuwa wamezeeka

Kwa sasa kuitwa Mzazi Ni jambo zito kwangu, Kuleta kiumbe Duniani sio Jambo la mchezo.
 
Back
Top Bottom