Prof Griff
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,771
- 5,268
Wana JF nimekuwa najaribu kutafakari kuhusu hali ya kisiasa na kiuongozi katika nchi yetu na maswali yanakuwa mengi zaidi ya majibu. Kuna kipindi marehemu Nyerere alisema kama niki-paraphrase kuwa mageuzi au upinzani wa kweli utakuja kutokea CCM, tukiangalia hali ya mambo yanavyokwenda na CCm kuwa na moto mpya wa kuanza kufungua matawi mapya na kutafuta wanachama wapya nchi za nje je hiki kinaashiria lolote lile au wanajaribu kupiga mahesabu ya mbali ambayo hatuelewi. Kampeni ya CCM inayoendelea ni kufungua matawi kadhaa katika miji mingi kwa kadiri itakavyowezekana nje ya nchi na kupata wanachama wapya walioko nje, kwa mfano CCM watakuwa wanafungua tawi jipya Missouri wikiendi hii na pia watakuwa katika miji mingine pia kwa mwezi huu na inayofuatia. Je tutegemee upinzani wa kweli kutokea ndani ya CCM? Je Kuna dalili za kutosha kuwa upinzani tulionao ukishirikiana na wote wanaopenda maendeleo ya kutetea nchi yao katika utaratibu mzuri wa kiuongozi na kuwajibika utatufikisha katika hali bora ya kimaisha?
What a load of crap!!