Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Mzee Jasusi,

Wananchi tulishachoka na hayo maneno, dalili hazionyeshi kuwa mbele kuna mwanga bro! I mean I have a feeling kuwa it won't happen in our life time, labda kikzazi kijacho, lakini bado ni worhty kuendelea kupiga kelel hapa forum!
 
Mzee Es,
Bustani zetu ziko mbioni kubinafsishwa, sijaona makala inayopinga kitendo hicho toka viongozi wapinzani. Wanasubiri kitu gani hasa ikiwa baadhi yao hapa JF ndio kijiwe chao?....
Hata ukitazama scandal zote walizowahi kuanzisha zimekufa kabisa! sidhani kama kuna mtu anafuatilia tena Richmond, IPTL, Rada, NBC na mengine kibao ambayo kauli ya rais tu ilifunga mjadala wa kitaifa. JK anahitaji kuwekewa kaa la moto kutowapa hifadhi wabadhilifu. Msukumo wenu kuleta mageuzi ni ushindi mkubwa kwenu machoni pa wananchi. Kama tunavyoipa sifa JF ktk baadhi ya maswala.
Kusubiri CCM watoe mwanya na nafasi sawa ya upinzani ni ndoto!..
 
Kwa nini upinzani hawanielewi, na hawana positive na serikali ya awamu ya nne?

.......coming up next......!
 
Nawashukuru wote waliosoma makala yangu iliyopita, walionipongeza na wale walionitusi kupitia ujumbe mfupi wa Simu zao na barua pepe. Wote wamenifanya niendelee kuelewa na kujifunza zaidi mawazo ya wananchi wenzangu. Ni changamoto nzuri kwangu, lakini napenda pia ieleweke kuwa, yote niliyoyaandika katika makala yangu, ni mawazo yangu binafsi na hayahusiani na chama changu cha mapinduzi CCM.

......Coming Up Next......



Fundisho La Uhuru wa Kenya!............!
 
Mkandara:

Hilo la bustani uchambuzi wake umenipita. Nipe link.


Mzee Es:

Hizo makala ya Tambwe Hiza si uziweke kwa ukamilifu wake? Binafsi nimezisoma, zimesheheni hoja tenge ambazo najua hapa JF hoja zitajibiwa kwa hoja. Pumba na mchele vitatenganishwa. Sidhani kama sina-deserve kuwekwa vipisi vipisi vya coming soon or to be continued kama zilivyo hard facts unazozitoa kule kwenye mjadala wa Richmond.

To all:

Ur all right. We need level field(kwa maana ya mfumo) but we also need strong oppossition parties. They all have to be addressed kwa pamoja. Ila la muhimu zaidi ni kujenga vyama vyenye nguvu vya upinzani. Hii inahitaji pia mwamko wa kifikra toka kwa wananchi. Je, ni kazi ya upinzani pekee kuwaamsha wananchi kifikra? Anyway, suala hili linahitaji mjadala mpana; kuna uhusiano wa CAUSALITY hapa!

Tazama DINI, VYOMBO VYA HABARI, AZISE/AZAKI, VYAMA VYA WAFANYAKAZI nk, utajua kama taifa tunafanya kazi chini ya mfumo gani. Inahitaji uthabiti na kuleta mabadiliko chini ya mfumo huu wa udhibiti. Tunajitahidi, Inshallah tutafika-na si mbali!

JJ
 
J.J Mnyika,

Habari za gardens zetu nimezipata toka humu:-
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2993

We need level field(kwa maana ya mfumo) but we also need strong oppossition parties. They all have to be addressed kwa pamoja.

hapa mjomba sikubaliani kabisa!... hata mimi huu ni mtazamo wangu isije chukuliwa kama ndio mawazo ya kila mtu. Nitasema kwa nini nafikiri Mzee Es amewasakama.

J.J Mnyika, Mnashindwa kutenganisha vitu viwili muhimu hapa. Navyo ni kwamba nchi yenye demokrasia ya kweli ni ile yenye kutoa nafasi sawa kwa vyama - (Equal field level) ktk Kutangaza siasa zake. Sasa kama Tanzania hakuna ina maana hatuna haja kabisa ya kuwa na vyama vya Upinzani ktk mtazamo wa demokrasia (chama mbadala). Kila kunapokucha kazi za vyama vyetu ni kugombania nafasi sawa jambo ambalo CCM imewahakikishia kuwa haiwezekani sawa na serikali ya mkoloni ilivyokuwa ikitawala. Na bahati mbaya mnaendelea kupigania haki yenu ya demokrasia ambayo kwa mlalahoi hawezi kabisa kuelewa mnapigania kitu gani hali nchi yetu iko huru na kama ni demokrasia sii hiyo mnayo?..
First, wengi wetu hatuelewi nini demokrasia na inafanya kazi vipi ktk mazingira yapi - tunachofahamu zaidi ni kuisoma hiyo demokrasia ktk magazetini, kama vile fiction.

Kwa hiyo hapa nafasi ipo tu ktk upinzani kuchagua ni mbinu gani itangulie. Kama ni kutafuta Demokrasia, basi hakuna haja ya vyama kujiunga na uchaguzi wa aina yeyote na kuweka madai yenu ktk kutafuta hiyo level. Hapa viongozi hamhitaji chama hata kidogo kwa sababu kuwepo kwa chama na kushiriki kwake ni sababu moja tosha kuwepo kwa level sawa ya demokrasia (quote n qoute) huko nje. Ikiwa hampewi nafasi sawa dawa yake ni kutoshiriki...
Mapambano yenu yanakuwa ktk kuwaelemisha wananchi kama walivyofanya akina MLK, Malcom na kadhalika yaani vyama vya UPINZANI..

Nafikiri leo inabidi nikupe wazi msemo wako mwenyewe kuwa Chadema sio chama cha UPINZANI ila ni Chama MBADALA. Na hupendi kabisa watu wanapokiita Chadema chama cha Upinzani.
This is where mawazo yenu na ya wananchi yanapopishana.
J.J Mnyika, huwezi kuwa chama mbadala ktk mfumo ambao hauna leve field sawa. Huwezi kuwa chama Mbadala hali madai yako mengi yatakuwa yakikwamishwa na katiba iliyopo ambayo inakumbatia chama kimoja. Hapa mnakuwa hamna mwelekeo kwa sababu wananchi wanashindwa kufahamu hasa vyama hivi vinapigania kitu gani!. Kibaya kuliko yote ni kwamba mnajaribu kuyafanya yote kwa pamoja..

1. Kutafuta uwanja sawa huku mkiwa bado ndani ya ligi...
2. Mnacheza mechi hali mnafahamu marefa, linesmen wote ni vibaraka wa timu mnayocheza against!..huku mkitegemea kwa baraka zake Mungu labda kutatokea muujiza wa ushindi!... heeeeelll No haiwezekani hata kidogo.
Kisha baada ya mechi mnataka wananchi wafahamu kuwa mlishindwa kwa sababu... blaaa blaaa blaa! lakini kwa nini mmejiunga na ligi? hali mnafahamu toka mwanzo ligi hii ni feki?.. inapangwa kama mechi za boxing za mzee Don King! unless nanyi ni washiriki wazuri ktk mchezo huu kutafuta ngawila!...
That is Mzee Es point. kama kweli mnataka kuwakilisha wananchi mnatakiwa chama cha UPINZANI na mfanye kazi zenu kama Wapinzani. Madongo tuuuuuu kila kukicha!.. Wananchi watakuja kuona mwanga na ndio siku CCM wataweka uwanja sawa na pengine mnaweza kuchukua imani za wananchi ktk Upinzani kuliko ktk mfumo mliokuwa nao leo....Ati vyama mbadala ktk mfumo usiokuwa na haki.
 
Kaka Mkandara:

Nilichomaanisha ni kuwa huwezi kuwa na uwanja sawa wa kisiasa kama huna vyama vya upinzani vyenye nguvu na huwezi kuwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu kama huna uwanja sawa wa kisiasa; na kinyume chake. Kwa maneno mengine ni kama hidaya ya kuku na yai kipi kitangulie!

Kama vyama vinataka kususia uchaguzi(kitu ambacho tumeshaanza kukijadili) lazima viwe na uwezo wa kuleta kishindo cha kususia uchaguzi(ndio maana tunaendelea kuijenga CHADEMA mpaka vijijini kupitia Mpango wa CHADEMA ni Msingi ambao tunakwenda kwa awamu wilaya kwa wilaya). Ndio maana wakati tumeanza kudai katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi wakati huo huo tunapaswa kujenga mtandao/netiweki ya chama na asasi za chama(kwa maana ya kujenga chama taasisi) na wakati huo huo tunapaswa kuendelea kuwatumikia wananchi(kwa maana ya kuwatetea na kuchochea uwajibikaji ikiwemo kukusoa serikali iliyoko madarakani) na kuhamasisha mwamko wa wananachi(kwa maana ya kupanua uwekelewa wa kisiasa).

Sasa uchaguzi utakapo karibia tutafanya tathmini: Je, tumefanikiwa kwa kiasi gani katika nyanja zote mbili? Je kuna sababu ya kushiriki uchaguzi? Je, tushiriki namna gani?

Ndio maana nikasema nyote mko sawa- "its is a glass is half full, no its half empty scenerio!"

JJ
 
Kaka Mkandara:


Ndio maana wakati tumeanza kudai katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi wakati huo huo tunapaswa kujenga mtandao/netiweki ya chama na asasi za chama(kwa maana ya kujenga chama taasisi) na wakati huo huo tunapaswa kuendelea kuwatumikia wananchi(kwa maana ya kuwatetea na kuchochea uwajibikaji ikiwemo kukusoa serikali iliyoko madarakani) na kuhamasisha mwamko wa wananachi(kwa maana ya kupanua uwekelewa wa kisiasa).

Sasa uchaguzi utakapo karibia tutafanya tathmini: Je, tumefanikiwa kwa kiasi gani katika nyanja zote mbili? Je kuna sababu ya kushiriki uchaguzi? Je, tushiriki namna gani?


JJ

Niongeze pia kuwa wakati haya yote yakifanyika vyama vya upinzani pia viibuke na falsafa na sera mbadala. Kwa maana ingine, we have to change the strategy from merely being against something, to being for something! For instance, instead of being against cost sharing in higher education, we can say we are for increased public funding of higher education channelling more resources to public services than to utawala.

Furhermore whatever proposal we make it has to be evidence based. Kwa mfano, inabidi kuonesha kimahesabu kabisa kuwa inawezekana serikali kulipia gharama za elimu ya juu kwa kupunguza gharama za utawala na kuonesha maeneo ya utawala ambayo yangeminywa na idadi ya fedha zitakazopatikana, kama vile ku-phase out wakuu wa wilaya, kuwa na wizara 13 badala ya 30, etc. Nahisi hatujafikia hii hatua na nafikiri ni scenario critical in rebranding the opposition in the eyes of the public.
 
J.J Mnyika,
Nilichomaanisha ni kuwa huwezi kuwa na uwanja sawa wa kisiasa kama huna vyama vya upinzani vyenye nguvu na huwezi kuwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu kama huna uwanja sawa wa kisiasa; na kinyume chake. Kwa maneno mengine ni kama hidaya ya kuku na yai kipi kitangulie

Safi kabisa!..
Sasa ikiwa hakuna kilichotangulia sisi akina yakhe tunajiuliza why waste kutafuta kilichotangulia hali vitu vyote tayari vipi?.na watu wanazidi kufa na njaa.

Je, sii jukumu letu kuamua kuwa wafugaji wa Kuku ama Mayai?..
Tatizo lenu mnataka kufuga vitu vyote wakati vifaranga ni marufuku kuingizwa nchini ila kwa kupitia taasisi ambayo ni mpinzani mkubwa wa biashara yenu?...In all cases lazima uwe na vifaranga maanake kuku hawa wa siku hizi hupati kuku wala mayai bila chanzo chake ambacho ni vifaranga - Demokrasia! demokrasia yetu ipo kwa tafsiri ya CCM!
Interesting haaaa!... kwi kwii kwiii!..ngoma zangu hizi uncle!
 
Kaka Mkandara:

Teh teh teh teh! U know how to dance with words....


Kitila Mkumbo:

habari za siku kaka! Kumbe na wewe upo humu....

Nakubaliana kabisa na mawazo yako-ila changamoto ni kuwa hawa jamaa wana-mess up kila siku mpaka na sisi tunaingia mkenge wa kuwa faya brigades.

Kuna wakati tunasema alternative policy positions ila in the middle of the crisis watu(hususani waandishi) huwa wana-pick zaidi juicy issues(matatizo of the day, na short term solutions-in the case of crisis in higher learning, kwa maana ya wanafunzi kurudishwa shuleni). Debates kuhusu long term policy solution zinakuwa evaded.

kwa hiyo ni vyema tukawa pro active wakati wa majira ya kawaida, kukisubiri kuuza sera wakati wa reactions tutaendelea kusukumwa na upepo.

We need to adjust the sails and set the agenda...

Hata hapa JF tunaugonjwa huo wa MBC-angalia issue ya cost sharing iliyolala sasa, huu ndio ulikuwa wakati mwafaka wakuendelea kupiga mawe wakati tunapoelekea kwenye bunge la bajeti.....

JJ
 
Wazee wote hapo juu heshima mbele, mawazo mazito na elimu kali kwa kuongezea tu ninasema kwamba pia upinzani uachane na tabia ya one man show, kwa hiyo field haiko levelled kwenye taifa tu, bali hata ndani ya vyama vya upinzani pia nako hakuna uwanja sawa kwa viongozi wao, leo Chadema ni Freeman, it used to be Mtei, na baadaye Makani,

Pamoja na mapungufu yao mengi, CCM ina viongozi wengi mno yaani almost kama Brazilian Soccer Team, unaweza kuwapumzisha kikosi kizima cha kwanza na kuiweka team B, na mabo yakawa sawa tu, leo ukimtoa Mrema TLP, basi na siasa imeisha, anyway bado najaribu kuchota elimu nzito kwenye posting zilizopita kwenye hii ishu kabla ya kuja na more!
 
JJ: true indeed, lakini tukumbuke hawa jamaa watatupeleka hivi hivi hadi wakati wa uchaguzi halafu wasema wapinzani hawana sera kazi yao ni kupinga. So, we have to do both in a parallel fashion, striking and at the same time advancing. Nitafurahi siku moja nikisikia kulifanyika seminar na waandishi wa habari kuzindua consultation process kuhusu mwelekeo wa sera ya elimu, afya, uchumi, etc za chadema in the next 5, 10, 15 or so years. Hiyo tutakuwa tumepiga hatua moja muhimu sana mbele.
 
Kitila:

Nakubaliana nawe kabisa. Lazima tuanze kutangaza sera kuanzia sasa.


Mzee Es:

Si vyama vyote vya upinzani ni one man show. CHADEMA ni zaidi ya mtu mmoja. CHADEMA si Mbowe ingawa Mbowe ni CHADEMA. Ndio maana CHADEMA inaendelea na harakati zake za kisiasa pamoja na kuwa Mbowe yuko masomoni.

Unaweza kutaja majina ya viongozi wengine katika CHADEMA, na nakwambia hata ukimuondoa Mbowe leo CHADEMA kama taasisi itaendelea na harakati zake za kisiasa. Tunaongozwa na Mpango Mkakati wa kudumu!

Lakini siwezi kukata kwamba Mbowe ana nafasi ya pekee kwenye CHADEMA kama Mwenyekiti wa Taifa.

Na hii si CHADEMA tu, hata CCM- huwezi kupuuza nafasi ya Kikwete na Malecela katika CCM; hebu jaribu kujiuliza watu hawa wakitoka ghafla (ni wazi system ya chama chenu itatikisika kabla ya kurudi katika hali yake ya kawaida).

Lakini sisemi kwamba CHADEMA ni taasisi iliyokamilika katika kila kona-bado tunaendelea na jitihada ya KUJENGA CHAMA TAASISI badala ya chama uchaguzi ama chama mtu!

karibu

JJ
 
Tanzania, CHADEMA, CCM na mjadala wa falsafa na itikadi; lipi ni jibu? - Sehemu ya kwanza

Na John Mnyika

Mjadala kuhusu falsafa na itikadi umeibuka tena rasmi. Nimesoma mahojiano ya mwanasiasa kijana David Kafulila akizungumzia CHADEMA ni Msingi na makala ya mchambuzi mahiri Prince Bagenda aliyoyapa kichwa "Itikadi ya Mrengo wa Kati si jibu. Nimesoma pia makala ya Mwenyekiti wangu-Freeman Mbowe kuhusu suala hili. Ni dhahiri mjadala umefumuka rasmi. Suala la falsafa na itikadi si la wanasiasa na vyama tu, ni suala la kitaifa; tulijadili. Katika makala yake Prince Bagenda kimsingi, amebeza itikadi ya mrengo wa kati. Si lengo la sehemu hii ya kwanza kujibu hoja kwa hoja uchambuzi wa Bagenda kuhusu mrengo wa kati. Lengo la makala ya leo ni kueleza ni nini hasa itikadi ya mrengo wa kati. Katika makala yake Freeman Mbowe amebainisha hoja mbili kubwa- Mosi, kwamba CCM haifuati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa vitendo kama inavyotangaza kwa maneno na nyaraka zake(kwa maneno mengine CCM inakiuka katiba ya nchi). Pili; kwamba kitendo cha serikali ya CCM kuweka kwenye katiba ya nchi kwamba Tanzania ni nchi ya itikadi ya siasa na ujamaa na kujitegemea ni kinyume na dhana ya demokrasia ya vyama vingi ambayo inataka uhuru wa fikra na kiitikadi. Nitachangia kwa kiasi hoja hizi(kwa maana nyingine vyama vyenye itikadi tofauti na ujamaa na kujitegemea vinakiuka katiba ya nchi). Nitajadili!

Kwa tafsiri rahisi, falsafa ni fikra na mtazamo wakati itikadi ni imani. Maneno haya mawili ni muhimu sana katika medani ya siasa na maendeleo kwa ujumla. Nimewahi kupitia katiba za vyama mbalimbali vya siasa nchini, nimewahi kupitia Azimio la Arusha, nimewahi kusoma maamuzi ya Zanzibar(ambayo wengi huyaita Azimio la Arusha) na ninayo kama rejea ya msingi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukipitia nyaraka zote hizi utaona kwamba mjadala kuhusu falsafa na itikadi ni suala lisiloepukika.


Mwaka 1991 Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi wakati huo alijitokeza na kutoa hotuba ndefu akitetea maamuzi ya Zanzibar na kusisitiza kwamba CCM inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, namnukuu: " Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo, tokea mwanzao, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi). Haikugeuka wala hatutazamii kuigeuza. Kwa hali yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatutaigeuza Siasa hii. (Makofi) . Kule Zanzibar tulizungumza mambo mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao."


Lakini miaka kadhaa baadaye, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitamka wazi kwamba CCM haifuati siasa ya ujamaa na kujitegemea, nikinukuu kitabu chake cha uongozi wetu na hatma ya Tanzania : Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi.Na walikuwa na haki ya kufanya hivyo, maana sera ni yao, ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na hadi sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea.' Haya ni maneno ya kiongozi ambaye alishiriki moja kwa moja kuandika Azimio la Arusha na misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2000, mwaka mmoja tu baada ya baba wa Taifa kufariki, serikali ikapeleka bungeni mabadiliko ya Katiba na kuweka tafsiri finyu ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2006, Agrey Mwanri-Mbunge wa CCM akichangia katika Bunge la Kwanza la Bajeti alijenga hoja nzito kwamba nchi hii haina itikadi, kinachoendelea hapa ni shughuli tupu. Mwaka 2007, Agrey Mwanri huyo huyo, baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alijenga hoja kinzani wakati wa kuchangia mjadala kuhusu muswada wa rushwa; kwamba nchi yetu bado inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na kwamba bila siasa hii; mustakabali wa taifa utakuwa mashakani. Hapa ndipo tulipofika! Je, mustakabali wetu hauko shakani?


Kauli hizi zinahitaji kujadiliwa. Inaweza kuonekana hili ni suala dogo. Lakini hilo ndio chanzo ya matatizo ya watanzania. CCM inafuata sera ya Ubepari uliokubuhu na mfumo wa soko holela. Ndio maana leo wageni na wawekezaji kutoka nje wanapewa kipaumbele zaidi. Ukuaji wa uchumi unawanufaisha wachache na matabaka katika jamii yanazidi kuongezeka, Uzalishaji umepungua na tumegeuzwa wachuuzi wa bidhaa toka nje.Kwa upande mwingine mzigo wa huduma za kijamii katika sekta za elimu na afya unazidi kuwa mzigo kwa watanzania maskini.Chama tawala kinapokosa itikadi maana yake kimekosa dira. Chama kinapokosa itikadi yake hakiwezi kuandaa sera na kutoa mwelekeo wa Taifa!.


Niweke pia bayana kwamba ujamaa ni neno tamu; ni tamu linapobeba dhana ya undugu na usawa. Lakini inapochukua sura ya dola kufanya uzalishaji wa moja kwa moja hapa hupoteza maana. Kujitegemea ni suala zuri. Hasa linapotekelezwa kwa vitendo bila kuegemea wahisani. Hata hivyo maneno haya yanapotumiwa hivyo sivyo na vyama visivyo na dira wala mwelekeo dhana hizi zinapoteza dhima na maana yake!


Bagenda amejenga hoja kwamba vyama vya upinzani nchini vinaiga itikadi za kimagharibi na ameshambulia moja kwa moja itikadi ya CHADEMA ya Mrengo wa kati. Anasahau kwamba CHADEMA ni chama hakijatoka nchi ya misingi yake ya asili. Wakati wa mabadiliko ya Katiba ya CHADEMA mwaka 2006, ambayo yalihusisha mchakato wa kutuma timu za kukusanya maoni ya wanachama toka ngazi ya wilaya, nilikuwa mjumbe katika kamati ya itikadi. Kamati hii iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mwesiga Baregu-Profesa wa siasa na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Kamati hii iliratibu mchakato wa kuweka bayana itikadi ya chama katika katiba. Hapo nyuma tulisema CHADEMA inaamini katika falsafa na itikadi ya nguvu na mamlaka ya umma. Sasa tumeamua kuweka bayana falsafa yetu na itikadi yetu. CHADEMA tunaendelea kuwa na falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma. Huu ni msimamo wetu wa asili: Kwamba falsafa ya CHADEMA ni kuamini katika "nguvu na Mamlaka ya Umma"(People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni na kuendeleza mawazo, raslimali, uchumi na siasa za nchi. Aidha, falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa kwa dola ya nchi na kuwa umma ndio wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatma ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni....hivyo basi, falsafa ya "nguvu na mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vinavyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na haki. Hii ni falsafa tuliyokuwa nayo ambayo tunaiendeleza.


Kwa upande mwingine tulipitia madhumuni ya kuanzishwa kwa CHADEMA pamoja na sera za chama. Tumejitafakari kiitikadi na kuona tutamke bayana katika katiba yetu tuko wapi. Mkutano mkuu uliamua kwa kauli moja kwamba CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI(center party). Kwangu mimi itikadi ni imani. Ni imani inayotuunganisha. Ni imani inayotuongoza. Ni imani inayotuelekeza. Ni imani tunayoielekea. Dhana ya "Mrengo wa kati" pengine itaeleweka vyema kama nitasimulia kisa cha dola moja ya kifalme kama ifuatavyo.


"Katika ufalme huo palikuwa na baraza ambalo lilikuwa na wajumbe wa makundi matatu. Kundi moja lilikuwa upande wa kulia: Hili lilikuwa ni kundi la watawala, wakati wote lilitetea utawala, nidhamu ya kijamii na maslahi ya watu binafsi. Kundi la pili lilikaa upande wa kushoto: Hili lilikuwa likitetea umuhimu wa dola kuhudumia wananchi ikiwemo umiliki wa pamoja wa njia zote za uzalishaji mali na kuweka mkazo katika haki za matabaka. Kundi la tatu lilikaa katikati: Hili lilikuwa likitetea umuhimu zaidi wa dola kuwawezesha wananchi, likiweka mkazo katika uhuru na uwezekano wa kuboresha maisha ya mwanadamu na jamii. Kundi hili la tatu ndio asili ya itikadi ya mrengo wa kati.


CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati kwa mujibu wa madhumuni yake na sera zake. Mathalani, ukipitia madhumuni ya kiuchumi ya CHADEMA, utabaini kuwa ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao. CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru ama soko la kijamii, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti. Tunaamini katika soko huru sio soko holela. CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.


Pia CHADEMA kinayo misingi muhimu katika sera na ajenda zake inayokiweka chama katika Mrengo wa Kati. Tunaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri. Tunaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo nzuri. Tunaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa. Tunaamini katika umuhimu wa dini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola. Tunaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu. Tunaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake. Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya CHADEMA kuwa chama cha mrengo wa kati.


Hatahivyo, hatuamini kwamba itikadi ni suluhisho pekee la matatizo katika taifa. Tutaendelea na utamaduni wetu wa kuwa na itikadi laini (relaxed ideology) badala ya itikadi iliyojibana (restrictive ideology). Tutaendelea na msimamo wetu wa kutaka mabadiliko kwa vitendo (pragmatism). Hiyo ni imani, matumaini na mwelekeo wetu. Tunahitaji vyama viwe na falsafa na itikadi ili wananchi wachague ni chama gani kiwaongoze katika wakati gani. Lakini hatuhitaji itikadi ya chama kimoja ndio iwe itikadi ya taifa lote kikatiba. Ingawa tunahitaji mjadala wa kitaifa. Ili tuwe na misingi ambayo tutakubaliana kwa pamoja kama taifa katika katiba mpya, misingi hii kila chama kitaonyesha ubunifu na umahiri wa kuizingati, kuitafsiri na kuitekeleza kupitia falsafa, itikadi, sera na shughuli zake. Nawasilisha hoja hizi kuendeleza mjadala tujiulize- Tanzania, CCM, CHADEMA na mjadala wa falsafa na itikadi;lipi ni jibu?



Mwandishi wa makala hii ni mwanaharakati na mwanasiasa kijana anayepatikana kupitia 0754 694 553, mnyika@yahoo.com na www.chadema.net
 
Wazee wote hapo juu heshima mbele, mawazo mazito na elimu kali kwa kuongezea tu ninasema kwamba pia upinzani uachane na tabia ya one man show, kwa hiyo field haiko levelled kwenye taifa tu, bali hata ndani ya vyama vya upinzani pia nako hakuna uwanja sawa kwa viongozi wao, leo Chadema ni Freeman, it used to be Mtei, na baadaye Makani,

Pamoja na mapungufu yao mengi, CCM ina viongozi wengi mno yaani almost kama Brazilian Soccer Team, unaweza kuwapumzisha kikosi kizima cha kwanza na kuiweka team B, na mabo yakawa sawa tu, leo ukimtoa Mrema TLP, basi na siasa imeisha, anyway bado najaribu kuchota elimu nzito kwenye posting zilizopita kwenye hii ishu kabla ya kuja na more!

Sidhani kwamba ukipumzisha kikosi cha kwanza cha CCM mambo yatakuwa sawa tu kwa sababu kikosi hicho hicho cha kwanza kinaboronga mambo beyond belief! Sasa uweke kikosi cha pili si ndio itakuwa kiama kabisa.....Tanzania kuna leadership crisis ambayo haina suluhu kwa sasa....
 
JJ nilikuwa ninamaana kuwa mwenyekiti alipokuwa na Helikopta anazunguka kwneye kampeni, ilichukua karibu hela zote za kampeni za chama mpaka ikabidi baadhi wabunge wa Chadema kukosa hela za kampeni, na kujitoa kwenye uchaguzi huo, sasa mimi nilidhani huo ni mfano tosha wa how one show inakuwa built in a system ya chama cha siasa, na nilifikiri kuwa mtindo wa namna hiyo haufai katika kujenga nguvu za upinzani za kweli na kuwepo katika taifa zima badala tu ya Darisalama, na mwenyekiti.

Huko CCM, hata Muuugwana na JM, wakitoka sidhani kama kutakuwa na tatizo at all, maana sasa kina Mangula ndio kwanza wanaanza kugombea ueneyekiti wa mkoa huko Iringa, kina Salmin wako pembeni huko Visiwani, kina Sumaye ndio kwanza wanatafuta ujumbe wa NEC, kwa hiyo kwenye hili sidhani kama kuna comparison,

Lakini, pia nimekusikia mkuuuu!
 
Nyani Ngabu,
nadhani Mzee Es alikuwa na maana ushindi wa CCM ktk uchaguzi na sio ktk kuongoza nchi.
 
(JOKE):

Teh teh teh

Nyani Ngabu:

Nimependa hoja yako. Kwamba CCM ikipumzisha kikosi cha kwanza wakikaa 'watoto wao' itakuwa dhahama zaidi!

CHADEMA je, wakipumzika wakina Mbowe wakaingia wakina Mnyika itakuwaje?

There is a solution to Tanzania's leadership crisis!

JJ
 
Mzee Es:

Hujanisikia!

Suala la Helikopta nimeshalizungumza sana, rejea makabrasha. Haukuwa uamuzi wa kumjenga Mbowe kama mtu ulikuwa uamuzi wa kumtumia mgombea urais kujenga chama kwa ujumla wake.

Nilichambua kwa kina gharama ngapi zilitumika na ngapi zilitumika kwa ubunge na kwanini.

Na nilieleza kwa nini wagombea wengine walijitoa na kwani nini wengine hatukujitoa.

Soma! Soma! Halafu ndio SEMA, SEMA!

Hata ukija wewe Mzee Es kugombea urais tutatumia helikopta- Soma tamko la CHADEMA kuhusu mipango ya uchaguzi 2010.

Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa tutawekeza rasilimali za chama ngazi ya ubunge kwenye target seats!

Nashukuru sasa umenisikia

JJ
 
Wakiingia kina Mnyika & Co. there's a high probability watakuwa kama predecessor counterparts wao kwa vile bado wana njaa....Mnyika naye atataka kufikia Waldorf Astoria kila akija New York, Mnyika naye atataka kuvaa suti za dola 5,000, kuvaa mashati ya Brooks Brothers, Mnyika naye atataka kuendeshwa kwenye Maybach ya dola 300,000, atataka kuruka na Gulfstream.......huku asilimia kubwa ya watu wakiishi kwa chini ya dola moja kwa siku, hawana maji safi, umeme wa uhakika, n.k., n.k........acha tu bwana......madaraka yana utamu na raha yake.
 
Back
Top Bottom