Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Kalamu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2006
Messages
874
Points
0

Kalamu

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2006
874 0
ES & Mkandara, Kudos! I fully agree, TZ we have millions of excuses. Granted playing field isnt levelled, Incumbency factor, resources na mengineyo..so what? ni wapi..opposition walishawahi kushinda kwa sababu chama tawala kilitaka iwe hivyo especially in Africa? as long as system inaisaidia CCM, forget kupata sheria inayotoa haki sawa kwa wote! Nini kifanyike, operate within and with what you have. It doesnt require new law for me or another JF member kujua kwamba top leaders in CCM ni accomplice wa wizi wa richmond, madini etc! I mean tunaelewa lakini tatizo ni alternative tulizo nazo!

Iam not a politician but Iam very kin with "my secret vote". I always vote my belief and fortunately wengi wetu Tanzania we are slowly coming to terms in dealing with those who tell us on what political values we should believe in. From Senagal to Zambia to Malawi....chama tawala always is strong. waungwana wa chadema et al, we fully appreciate the difficult environment you work in, but hiyo haitoshi..propound policies and try to invest katika uwakilishi wa sauti zetu bungeni, for now dont invest much in presidency maana mkienda bungeni mka-influence mambo, people will trust you more...just saying...
I better call you "Mkuki" - why 'Mikuki?'

I know Mnyika is listening/reading this and internalizing the sense behind it. He is an astute young fellow.

All the Mnyikas in the "Vyama Mbadala" I have a question for you:
Since the last general election (2005), how many of you have gone back and critically evaluated your performances in each of the constituencies where you competed and lost? Have you put in place a better plan for the next election?

This is getting a bit personal, but I've to ask Mnyika specifically - if an election is held today in Ubungo, do you think you stand a better chance than last time? (You don't have to answer this, just keep the answer to yourself). I'm asking because yours was one of the most competitive run. If you have lost ground, ask yourself why, and work hard to reverse the situation; but never be disheartened, because that is the nature of politics.

Now, all of this has to be going on 24/7/52/365/ until the next election, and at the basic level - home by home, and village by village. How else would you expect people to know you exist? I would say, you should forgo the presidency for the moment. Aim at building gradually your parliamentary representation, and the rest will follow in place in due course.

Mzee Es, this topic is another pointer to the very magnifiscent utility of JF. Where else would one find such an insightiful plethora of ideas!
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined
Feb 25, 2006
Messages
3,348
Points
1,250

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined Feb 25, 2006
3,348 1,250
JJ: Good piece.

Kwa utaratibu huu wananchi wataanza kuelewa umuhimu wa vision katika siasa. hawa jamaa wa CCM katika serikali ya leo hawana kabisa habari na mambo ya itikadi wala falsafa; wao wanapuyanga tu, na lugha pekee wanayoijua ni ushindi wa kishindo, yaani hii ndio wamegeuza kuwa itikadi na falsafa yao. If we become firm with policies the odds for the opposition are very good.
 

Kalamu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2006
Messages
874
Points
0

Kalamu

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2006
874 0
Niongeze pia kuwa wakati haya yote yakifanyika vyama vya upinzani pia viibuke na falsafa na sera mbadala. Kwa maana ingine, we have to change the strategy from merely being against something, to being for something! For instance, instead of being against cost sharing in higher education, we can say we are for increased public funding of higher education channelling more resources to public services than to utawala.

Furhermore whatever proposal we make it has to be evidence based. Kwa mfano, inabidi kuonesha kimahesabu kabisa kuwa inawezekana serikali kulipia gharama za elimu ya juu kwa kupunguza gharama za utawala na kuonesha maeneo ya utawala ambayo yangeminywa na idadi ya fedha zitakazopatikana, kama vile ku-phase out wakuu wa wilaya, kuwa na wizara 13 badala ya 30, etc. Nahisi hatujafikia hii hatua na nafikiri ni scenario critical in rebranding the opposition in the eyes of the public.
This it.
I have been wondering why this was not in place all along. I mean, why would you want people to elect you if you are not telling them what you stand for?

People still elect CCM in the erroneuos belief that it still stands for it's lofty ideas of the 60, 70s era. Watu bado wanaamini kuwa inasimamia haki na usawa wa maisha bora kwa waTanzania. Kwa bahati nzuri au mbaya, ni 'slogan' hizi hizi ambazo bado viongozi wa CCM wanazitumia kujipatia kura. Watu bado wanaamini hivyo, ni wajibu wa vyama 'mbadala' kuwafundisha wananchi ili wajue wanahadaiwa tu kwa maneno.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mzee Kalamu,

Maneno mazito hayo, na kwako JJ bado ndugu yangu tunahitaji zaidi kutoka kwako, 2010 sio mbali mkuuu, hebu jaribu kutushawishi zaidi bros, kwa nini tupigie kura Chadema na sio ccm wala vyama vingine, na kwa nini tuipigie kura chadema na sio Freeman as Freeman?
 
B

Brutus

Guest
B

Brutus

Guest
I better call you "Mkuki" - why 'Mikuki?'

I know Mnyika is listening/reading this and internalizing the sense behind it. He is an astute young fellow.

All the Mnyikas in the "Vyama Mbadala" I have a question for you:
Since the last general election (2005), how many of you have gone back and critically evaluated your performances in each of the constituencies where you competed and lost? Have you put in place a better plan for the next election?

This is getting a bit personal, but I've to ask Mnyika specifically - if an election is held today in Ubungo, do you think you stand a better chance than last time? (You don't have to answer this, just keep the answer to yourself). I'm asking because yours was one of the most competitive run. If you have lost ground, ask yourself why, and work hard to reverse the situation; but never be disheartened, because that is the nature of politics.

Now, all of this has to be going on 24/7/52/365/ until the next election, and at the basic level - home by home, and village by village. How else would you expect people to know you exist? I would say, you should forgo the presidency for the moment. Aim at building gradually your parliamentary representation, and the rest will follow in place in due course.

Mzee Es, this topic is another pointer to the very magnifiscent utility of JF. Where else would one find such an insightiful plethora of ideas!

Kudos Kalamu!
Ningekuwa nimegombea ubunge 2005 na kushindwa.. ningefuata ushauri wako Mkuu!

JJ Mnyika.. ushauri wa bure huu!
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Inaendelea........!

Kiongozi wa upinzani Kenya, yaani mtoto wa Kenyatta hivi karibuni alizungumza maneno mazito sana plae TVT, katika kipindi cha "Jambo Tanzania, na Jambo Afrika".

Yeye kama mkuu wa upinzani Kenya, moja ya wajibu wake kisiasa ni kukubali pale serikali inapofanya mazuri tena hadharani, na pia kuyasema mapungufu katika mhmili huo huo. Hapa ametoa fundisho zuri kwa vyama vya upinzani nchini kama kweli vinataka kuaminiwa na wananchi. Yaaani utaratibu wa kukubali na kuyasema bila kificho yale mema ya serikali kabla ya kukosoa, ni utaratibu unaomfanya mwananchi wa kawaida asione kwamba upinzani nia yake ni madaraka tu, na kwamba hausemi ukweli wa hali halisi ilivyo.

Nilichojifunza hapa ni kua wapinzani Tanzania wasipojifunza hili la kuisifu serikali pale inapofanya mazuri, basi watabaki kuonekana kila wasemalo ni uongo mbele ya umma hata kama lina ukweli. Kenyatta alianza kwa kusema yaliyokisibu chama chake hadi kikaondolewa madarakani, mbali ya kwamba ndio chama kilichopata wabunge wengi kuliko NARC. Alisema chama chake kilifikia mahalai kikawasahau wananchi wa kawaida jambo ambalo ndilo lililowaudhi wananchi huko Kenya, ndio maana waliamua kukitosa kwa vile kuna kuna watu wachache waliojiona kuwa ndio chama na wao ndio wenye nchi.

Alipoulizwa kuhusu uchumi, alikiri kuwa serikali ya Kenya imefanya vizuri ingawa alisema mikakati zaidi inatakiwa ili uchumi huo uwanufaishe wananchi wa chini zaidi, kuliko walioko juu kimaisha. Hapa kwetu si rahisi hata siku moja kwa kiongozi wa upinzani kutoa maneno ya kuisifu serikali, kazi yao ni kupinga tuuu, ni vizuri tukajifunza kutoka kwa Kenyatta. Mimi binafsi bado najiuliza, hivi vyama vya upinzani nchini na viongozi wao wanadhani wa-Tanzania hawajui hali ya taifa hili lilikotoka na lilipofikia kiasi cha kuwafanya wananchi waamini ule msemo wao maaarufu waliouzoea, wa " Miaka 45 CCM bado haijafanya kitu!"
Hebu tuangalie mifano ifuatayo na tuone ukweli kama serikali ya CCM haijafanya kitu!


............Itaendelea...........!
 

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Tunasubiri kwa hamu hayo mazuri ya CCM,
Lakini tu kumbuka kitu kimoja mzee wangu, kuzaa mtoto ni kitu kizuri sana na pia ni sifa lakini sifa ya uzazi haikomei ktk kuzaa tu... malezi pia, unaposhindwa kulea mtoto huyo na kumgawa kanisani, sifa zako za uzazi huondoka ama kwa lugha ya hapa kijiweni ndio tunamkoma nyani Gilabu! mawe tu!. heee heee heee!
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,133
Points
1,225

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,133 1,225
Hivi baba akileta mkate nyumbani anapaswa kusifiwa ama ni wajibu wake?
mazuri hayo yana tofauti gani na baba kupeleka mkate nyumbani?
Tambwe amejiandikia makala mbili ameona naye ana sifa za kuwa mjumbe wa NEC hili ni tatizo kubwa.
 

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Mpaka kieleweke,

Unapofanya WAJIBU ndio unastahiri upewe SIFA..matokeo ya wajibu wako ndio tunaweza kuweka mzani wa kungalia mapungufu ktk utekelezaji wake. Huwezi kumpa sifa mntu asiyefanya wajibu, na ikiwa wakibu wa baba ni mkate kila siku, well and good inawezekana mzazi mmojawapo ana uwezo na kipato zaidi na mwenziwe...
Sifa haiji kwa kutofanya usiyowajibika ambayo ni pamoja na utoaji roshwa, hongo ama kitu ambacho sii muhimu kwa mhitaji.
Fikiria kitu chochote kile utakuta ya kwamba wajibu ndio sifa yenyewe!
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mkoloni alipoondooka, alituachia shule takribani za msingi 3,000 zilizokuwa na wanafunzi 486,000,


Leo miaka 45 baada ya mkoloni kuondoka CCM imeanzisha shule za msingi 11,560 zenye wanafunzi millioni 7,957,884.

Serikali imejitahidi kwa kuongeza sekondari kutoka 549 hadi 1,333 katika kipindi kifupi cha mwaka 1995-2004 sawa na ongezeko la aslimia 142.8%, huku serikali ya CCM, awamu ya nne ikiongeza shule kama hizo mpya 480, ambazo hadi mwaka jana zimetuwezesha kama taifa kufikisha shule za sekondari za serikali 1,715 na 640 zisizo za serikali, zote kwa pamoja zikiwa na wanafunzi 700,000.
Katika miaka mitano ijayo serikali ya CCM, inategemea kuongeza na kufikisha taifa kuwa na shule 2,556, ikiwa ni pamoja na kuwa na shule moja katika kila kata, nchini.

Kutokana na uchahe wa shule aliotuachia mkoloni, hadi kufikia mwaka 1985, watoto waliokuwa wanakwenda sekondari walikuwa chini ya aslimia 5%, ya watoto wote wanaofaulu (waliofaulu na sio waliofanya mtihani). Mwaka 1995 tulifikisha asilimia 5.5%, kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya tatu kupitia MMEM na MMES, ziliwezesha mwaka 2005 kufikisha idadi ya vijana waliochaguliwa kuwa asilimia 21%, ya wote waliofaulu.


..........Itaendelea............!
 

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Mzee Es,
Mwaka 1960 Population ya Tanzania ilikuwa 10,026,000 na leo hii ni zaidi ya 36,500,000 Hii ni zaidi ya mara tatu..x3 sasa rudia kutazama shule zilizoongezeka na hesabu ya watu. Ni mara tatu kwa hiyo tumesimama palepale ila tu namba ndizo zimebadilika!

Hivi kweli ulifikiria kuwa Tanzania ingebaki na shule za msingi 3,000 baada ya miaka 45 ya Uhuru... duuuh! hata mtoto wa mlalahoi angekuwa na miaka 45 yaani after 45 years kuna mabadiliko ya Umri na umbile lake. Tunachozungumzia sisi walalahoi ni maendeleo ya masiha yetu! hapa ni hatua za kuondoka ktk umaskini, sii ukubwa wa umri na maumbile!
 

Ilongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2007
Messages
292
Points
0

Ilongo

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2007
292 0
Hizi takwimu ni nzuri sana kwa maana ukizitafakari zinaweza kukupa mwanga kuhusu Watanzania na Tanzania kwa kina zaidi:

Kwanza inaonyesha jinsi gani tulivyojaliwa rutuba ya miili (yaani tunazaana kwa kasi nzuri sana) - jambo ambalo ni zuri maana tunapata nguvu kazi ya Taifa na kuongeza kizazi chenye "fikra mpya za kimaendeleo" (hili sina uhakika nalo sana).

Pili iwapo kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake ipasavyo, hatupaswi kuwa hapa tulipo (ki-maendeleo), kifamilia hadi taifa. Na wajibu wa kwanza kabisa ni wa mzazi kuhakikisha anawatimizia mahitaji ya msingi hao anaowazaa. Je, hili tunalitekelezaje? Ni watoto wangapi wameshindwa kuendelea na elimu ya msingi kwa kukosa sare (uniform) na daftari (achilia mbali vitabu vya kiada na ziada)?

Je, ni kweli huyo baba na mama hawana uwezo wa kumnunulia mtoto wao hivyo vitu? Au ni matatizo yale yale tuliyo nayo ya kutokuwa na "vipaumbele"!!! Ule ufahari wa kuwa na watoto wengi, lakini matunzo hamna bado unatugubika?

Haiwezekani mwanaume uwe na uwezo wa kutafuta mahari na kuilipa kwa wakwe zako ili umpate huyo mkeo, halafu ukishaoa na kuanza kupata watoto mnashindwa (wewe na mkeo) kuwatimizia mahitaji yao ya msingi. Na hapo ndiyo mwanzo wa matatizo yote tuliyo nayo. Kwa maana hata hizo shule zinazotajwa hapo juu, bado hazijawanufaisha walengwa walio wengi. Tumekwama wapi?

Je, ni kwa sababu tumeshindwa kuwajibika katika ngazi ya Familia ndiyo maana tunashindwa kuwajibika hadi ngazi ya Taifa? Tumekwama wapi?

N.B. Kama takwimu hizo za shule za msingi ni sahihi, basi kuna haja ya kujenga shule nyingi zaidi tena haraka sana ama kupanua hizi zilizopo ili kuweza kumudu idadi hii kubwa ya wanafunzi (688 students/school na kama kila darasa linachukua wastani wa wanafunzi 45, tunahitaji madarasa 15 kila shule na madawati yanayoendana na idadi hiyo)
 

Mgumu

Senior Member
Joined
Nov 3, 2006
Messages
112
Points
0

Mgumu

Senior Member
Joined Nov 3, 2006
112 0
Uchambuzi mzuri wa Tambwe Hiza, twaipongeza sisim kwa juhudi za kuongeza shule za msingi na idadi ya wanafunzi.

Kwa upande wa pili wa shilingi sisim imeonyesha udhaifu mkubwa kutokana na takwimu za tambwe, wakati wa mkoloni shule zilikuwa chache, ilikuwa ni fahari kuwa mwalimu na kiwango cha elimu kilikuwa juu.

ongozeko la shule chini ya utawala wa sisim imepelekea kuongeza idadi ya shule, ualimu imeguuka kuwa laana, na kiwango cha elimu kimeporomoka, kuna baadhi ya shule vijijini zenye idadi kubwa ya wanafunzi kuna walimu wawili, imekuwa ni kawaida kwa wahitimu wa darasa la saba kumaliza elimu ya msingi huku akiwa hakui kusoma na kuandika.
 

Ilongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2007
Messages
292
Points
0

Ilongo

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2007
292 0
Uchambuzi mzuri wa Tambwe Hiza, twaipongeza sisim kwa juhudi za kuongeza shule za msingi na idadi ya wanafunzi.

Kwa upande wa pili wa shilingi sisim imeonyesha udhaifu mkubwa kutokana na takwimu za tambwe, wakati wa mkoloni shule zilikuwa chache, ilikuwa ni fahari kuwa mwalimu na kiwango cha elimu kilikuwa juu.

ongozeko la shule chini ya utawala wa sisim imepelekea kuongeza idadi ya shule, ualimu imeguuka kuwa laana, na kiwango cha elimu kimeporomoka, kuna baadhi ya shule vijijini zenye idadi kubwa ya wanafunzi kuna walimu wawili, imekuwa ni kawaida kwa wahitimu wa darasa la saba kumaliza elimu ya msingi huku akiwa hakui kusoma na kuandika.
Mgumu,

Hili la kutokujua kusoma na kuandika linanipa utata sana. Nilibahatika kuwa darasa moja na wanafunzi wawili ambao hadi tunamaliza darasa la saba mpaka leo hii wana wajukuu, lakini bado hawajui kusoma wala kuandika. Na walikuwa ni wahudhuriaji wazuri darasani, wakibeba mikoba iliyojaa madaftari na vitabu vya mazoezi, kalamu n.k. Pia katika shule hiyo hiyo, bado walikuwepo wanafunzi wengine (madarasa tofauti) ambao hawakuweza kujua kusoma na kuandika. Na wataendelea kuwepo (wengine labda wakifanyiwa uchunguzi wa kisayansi, wanayo hitilafu kwenye ubongo ambayo inaweza kuwa inasababisha wasiweze kuelewa wanachofundishwa).

Kwa hiyo kwenda shule, ukakuta kuna walimu wa kukufundisha siyo kigezo pekee cha kukufanya ujue kusoma na kuandika. Wapo wengi ambao walianza darasa la kwanza wakiwa wanajua kusoma na kuandika bila kupitia "tuition" (maana enzi zangu hazikuwepo) wala kupitia "nursery schools" (preparatory), isipokuwa kutokana na mwamko wa wazazi wao katika kumjenga mtoto wao.

Sema tu, katika nyakati hizi ambazo siasa (zilizojaa unafiki na uongo) ndiyo limekuwa kimbilio la kila mtanzania, zimetufanya hadi zile wajibu zetu tunazikana kwa matarajio kwamba fulani afanye kwa niaba yetu, wakati huo huo hatujibidishi kujua maendeleo ya huyo mwanafunzi yakoje!

Nadhani "Siasa za Ujamaa" zilikuwa ni sumu kali kwa Taifa letu. Uvivu (mwenye kujibidisha hana uhuru wa kutumia kile alichotafuta kwa jasho), kutokufikiri independently (zidumu fikra hata kama si sahihi), kutokuwajibika (siasa zikawa ndo zinaongoza kila kitu, chama kushika hatamu) hadi mashirika na viwanda vikawa vinaongozwa na "wanasiasa" wasiokuwa na utaalamu na vitu kama hivyo na wakitoa maamuzi mazito ya "operations and production".

Generally, umenigusa sana na hasa pale unapoongelea kwamba ongezeko la shule na wanafunzi liandane na ongezeko la walimu bora na wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwapa maslahi yaliyo bora. Hawa ndiyo wapishi wenyewe hasa waliotupika sisi tunaojadiliana hapa. Wanafanya kazi ngumu na katika mazingira magumu sana. Lakini, ndiyo hivyo tena mbunge (mwanasiasa) akimaliza miaka yake mitano anachukua more than TShs. 45,000,000/=, wakati hata effect yake ya kuwa bungeni haionekani. Mwalimu aliyenifundisha (na kunifunza) kwa miaka yangu saba hadi nikaiona njia ya kufika hapa nilipo, akistaafu baada ya utumishi wake wa muda mrefu (5yrs x 6 or more) anarushiwa makoko, tena kwa mbinde. Huo mshahara kila mwisho wa mwezi ndiyo kabisa, atausikia kwenye bomba (siku hizi naona labda wanapata, ila sijajua how effective it is; nitafuatilia nione).
 

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,133
Points
1,225

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,133 1,225
Wana JF tusikubali kuyumbishwa na takwimu hizi kwani tunapaswa kuelezwa ni kwa kiasi gani takwimu hizo zimeweza kulinufaisha taifa hili tangu uhuru.

Wakati wa uhuru taifa hili lilikuwa na wasomi wachache ila wazalendo wa kweli, tuhoji hizo shule zimewafanya watanzania kuwa wazalendo ama imewafanya kuwa kama wasiokuwa na uchungu na nchii yao.

kwa mfano ukiangalia takwimu za mkukuta utakuta kuwa wanafunzi wanaojiunga na sekondari ni 13.4% kwa mwaka 2006,wanaofaulu kidato cha nne ni 33.6% kati ya hao ambao ni asilimia 13.tuu.wanaojiunga vyuo vikuu ni 0.24% tuu. hapo unaweza kumwe4lewa Tambwe kwa kuangalia kwa upande huo. na ukiangalia takwimu hizo utaona jinsi ambavyo elimu yetu inaporomoka kwani kwa mwaka 2005 waliofaulu sekondari walikuwa ni 37.8%,na mwaka 2004 ni 38.1%.

hii maana yake ni kuwa shule zinajengwa hakuna waalimu ,vifaa, n.k . na huku Tambwe anawataka wapinzani waone kuwa hili ni jambo jema tena n la kusifiwa na viongozi wa upinzani eti kujenga maboma na ,kuweka vijana ndani yake na kisha kusema kuwa hizo ni shule na zimeongezeka ni aibu kwa Tambwe kutokuliona jambo hilo na kuwataka wapinzanni nao waanze kusifia kwa kina .
 

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Messages
2,721
Points
1,225

Ibrah

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2007
2,721 1,225
Pamoja na mapungufu yao mengi, CCM ina viongozi wengi mno yaani almost kama Brazilian Soccer Team, unaweza kuwapumzisha kikosi kizima cha kwanza na kuiweka team B, na mabo yakawa sawa tu, leo ukimtoa Mrema TLP, basi na siasa imeisha, anyway bado najaribu kuchota elimu nzito kwenye posting zilizopita kwenye hii ishu kabla ya kuja na more!
Mzee ES,

Bila shaka wewe ndiyo Nabii mwenyewe wa CCM! Yaani waniambia CCM ni kama Brazil! Hata hivyo Brazil can not dare to send Team B in the World Cup unless circumstances zote zinawa-favour wao!

Pamoja na hoja zako zenye sehemu ya ukweli; bado bado tunahitaji uwanja sawa wa kuchezea mechi za siasa ili tuweze kujua Vyama gani vya siasa vinaweza kutoa viongozi bora wa siku zijazo. Hebu angalia uwanja wa siasa za Tanzania: Katiba ya Nchi imetungwa na CCM tena kabla ya vyama vingi na bado hiyo hiyo ndo inatumika kwenye mfumo wa vyama vingi! Tume ya Uchaguzi ambayo ni referee has been appointed by CCM!

ES kuweni fair basi ili watazamaji tushuhudie mechi ambayo hatutatabiri mshindi. Kwa uwanja huu- Katiba na NEC, CCM is the winner forever! Si wanasema watatawala milele?

CCM ina viongozi wengi mno! Tunawaona wanavyochukua fomu za NEC ya CCM; watoto wa vigogo wale-wale, wenye mawazo yale-yale, na mlengo ule-ule!

Wapinzani ni vema mlione hilo. Lieni na Katiba Mpya yenye kutoa haki sawa kwa wote na Tume huru ya Uchaguzi; mkipigwa bao kwenye uchaguzi ndo mwaanza kulia! Kwa nini kuingia kwenye mechi ambayo watazamaji tunajua mtapigwa bao?
 

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Messages
2,721
Points
1,225

Ibrah

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2007
2,721 1,225
Mzee ES,

Heshima yako mkuu!

Mkoloni alipoondooka, alituachia shule takribani za msingi 3,000 zilizokuwa na wanafunzi 486,000,

Leo miaka 45 baada ya mkoloni kuondoka CCM imeanzisha shule za msingi 11,560 zenye wanafunzi millioni 7,957,884.

Serikali imejitahidi kwa kuongeza sekondari kutoka 549 hadi 1,333 katika kipindi kifupi cha mwaka 1995-2004 sawa na ongezeko la aslimia 142.8%, huku serikali ya CCM, awamu ya nne ikiongeza shule kama hizo mpya 480, ambazo hadi mwaka jana zimetuwezesha kama taifa kufikisha shule za sekondari za serikali 1,715 na 640 zisizo za serikali, zote kwa pamoja zikiwa na wanafunzi 700,000.
Katika miaka mitano ijayo serikali ya CCM, inategemea kuongeza na kufikisha taifa kuwa na shule 2,556, ikiwa ni pamoja na kuwa na shule moja katika kila kata, nchini.
Naomba ujibu swali hili Mhehiwa ES,

Hivi unakubaliana na utumbo huu wa Tambwe Hiza?

Kama ndiyo, lete takwimu za nchi jirana ztu za Africa Mashariki na hata Kusini kwa kutumia takwimu hizo hizo za Tambwe Hiza ili tuweze kujadili kwa ushahidi.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mzee Ibra,

Heshima yako mkuu, long time bro vipi huko masehemu? Anyway makosa yalifanyika mwanzoni tulipokimbilia kuwa na vyama vingi bila ya kuangalia kwa makini kwamba ni kwa nini tunataka kuwa na upinzani nchini, CCM walijua mapema kuwa wana-deal na viongozi wasioelewa, maana upinzani wangekuwa wanaelewa basi wangeshitukia kuwa CCM kukubali kuanzishwa kwao, ilikuwa ni pressure toka kwa wazungu, kwa hiyo wao ilikuwa ni kuweka mguu chini kuwa lazima katiba pia ibadilike, CCM hawakuwa na choice then kama walivyo nazo sasa!

No, wengi wao, yaani kina Mtei, walikuwa obsessed na ujiko tu kuonekana viongozi wa taifa wa upinzani, Seif amejaribu sana na anahitaji sifa nyingi, lakini kama ninavyosema siku zote watu waliokaa madarakani for the last 45 years, hawatatoa power kwa upinzani kama pipi, au kuuweka uwanja wa siasa uwe fair, historia toka kwenye Biblia inasema kuwa uhuru ulianza na Nabii Musa, alipopambana na Farao uso kwa uso huku akisaidiwa na Mungu ndio uhuru ukapatikana toka kwa Farao, ama sivyo mpaka leo Musa na wana-Israeli wangekuwa bado utumwani Egypt, wakililia uwanja kuwa hauko sawa!

The lesson ni kwamba Kenya, Zambia, na Malawi, uwanja haukuwa sawa lakini wapinzani waliwashawishi wananchi wakawalazimisha watawala, the CCM's likes kutoa uhuru na kuurekebisha uwanja wa siasa ukawa fair, kama bongo tunasubiri CCM siku moja wafurahi na kuamuka asubuhi na kuuufanya uwanja wa siasa kuwa fair, basi huenda tuna muda mrefu sana wa kusubiri!
 

Forum statistics

Threads 1,381,640
Members 526,151
Posts 33,807,096
Top