Nini faida kwa mtu kuzaa watoto?

Nini faida kwa mtu kuzaa watoto?

Narudia tena. Binadamu ni wanyama kama wanyama wengine, hatujui kwanini tuko hapa, hatujui kwanini tunazaliana, tupo tuu ili mradi siku ziende nasisi tufe tutoweke. Nje ya hapo ni kujipa moyo na kujifariji
Truth.. Watu wanaoishi na kuyafurahia maisha ni wale wanaoendana nayo.. Wale wasiotafuta maana ya maisha, kuzaa, kuajiriwa vs kujiajiri, starehe gani ni upuuzi na ipi si bora. Yani wale watu wanaoendana na mifumo kwa sababu hupata comfort na furaha

Wengine waliobaki hujawa sonona na emptiness hususani kwa nchi kama Tanzania ambapo kuwa huru kifikra ni kosa. Uzuri pekee wa hili group ndio watu huleta mabadiliko makubwa kwenye dunia, they are thinkers and doors who revolutionize, innovate and invent ili hili group lingine wainjoy. Tatizo la hili group ni mara chache kufanikisha ndoto zao na hivyo hawaipati furaha halisi kwa sababu huitaji kufanikisha greater purposes ambazo kwa nchi kama zetu za wachuuzi ni ngumu mnoo....
 
Kwa nini unataka umasikini wako na kukosa kwako akili na chungu ya matatizo yako hapa duniani umrithishe mwanao asie na hatia yoyote ya raha zako binafsi na mtu wako ?
Ukilalia masiko you gona die poor
 
Kuna mjadala nimeuona Twitter watu wameulizwa hili swali na limekosa majibu ya maana kabisa!
View attachment 3462018
Jibu ni la kisaikolojolia zaidi.

Jiulize ni kwa nini upendo uliumbwa ndani ya nafsi za watu, upendo huo ndiyo husukuma watu kuzaliana.

Wanaozaliwa nao kwa kutumia upendo huo huo ulioumbwa ndani za nafsi zao huwasaidia wazazi wao kutokana na binadamu kuzeeka.

Kwa hiyo, faida ya uzazi kwa mtu ni kunufaika na kutunzwa na mwanaye.

Pia faida ya uzazi iliyo nje ya binadamu, ni mpango wa Mungu kuijaza dunia.
 
Wewe unayatazamaje maisha? Kwa nini unazaa watoto?
Watoto wananipa furaha. Nayatazama maisha kama zawadi yenye changamoto.

Mfano umepata gari zuri halafu kuna saa linapata hitilafu inabidi ulihangaikie ili liwe sawa kisha linakuwa sawa na unaendelea kulifurahia.
 
Kabisa , tupo hapa kuyapa maana maisha.
 
Watoto wananipa furaha. Nayatazama maisha kama zawadi yenye changamoto.

Mfano umepata gari zuri halafu kuna saa linapata hitilafu inabidi ulihangaikie ili liwe sawa kisha linakuwa sawa na unaendelea kulifurahia.
Vipi ukipata mtoto jambazi au shoga?
Furaha ya gari ni tofauti na mtoto kwa sababu ni kitu kinachokuwezesha kusafiri na kupata hadhi/heshima fulani katika jamii, pia unaweza kuuza gari, kulitupa au kuachana nalo ukiona halina faida tofauti na mtoto.
 
Ukaona ushoga tyuuh? nyie watu mkoje kwani?
Mxxxiiiieeeew
 
Back
Top Bottom