Wana JF, salam!
Nategemea kushiriki mafunzo ya JKT yatakayoshirikisha wabunge vijana. Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU.
Nawatakia ujenzi mwema wa taifa kwa kutumia ubao huu/tuition hii ya bure itoayo elimu ya maisha ie JF.
sikupi hongera mpaka utakapohitimu mafunzo na kupewa force number.
Kule kuna misemo kama hii utaikuta pale main gate tu siku unaripoti:
1. Kuruta hujui kutembea
2. Trankadoso kafike kwenu
3. Kalinyekalinye
4. Songombingo
5. Disko (hapa utapenda maana ni wakati wa kuimba nyimbo za utaifa, kupeana moyo baada ya kazi ngumu ya kutwa nzima)
6. Kichele (sina uhakika kama mtakuwa mnalipwa posho mwisho wa mwezi, tulikuwa tunapata Tsh 300/- those days
7. Kujongomea - Kutoroka, huwezi kumaliza Jeshi bila kutoroka kwa hiyo mh. jiandae kwa hilo vinginevyo unaweza kushusha tani 10 za mahindi toka kwenye Fuso peke yako ukijifanya mlokole na kule hakuna sheria.
8. Usawa wa Gudulia - msosi time, mestine kiunoni (maafande huita appetile yako)
9. Utajibu
ndiyo afande katika kila amri yoyote utakayopewa -- hakuna kuhoji.
Utafanya kazi kubwa na
Kopro's - hawa jamaa ni hatari sana, kwa ufupi tu wana V mbili chini ya bega.
nafikiri ukirudi huko utakuwa umebadilika sana....