Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,208
- 99,953
Maskini dada zetu huko JKT watakoma.......
Hiyo ni semina sio mafunzo ya JKT. Hayo mafunzo yana mtaala wake ambao huwezi kumaliza hata kwa miezi mitatu. Nyie mnatafuta umaarufu wa kisiasa na sio mafunzo ya JKT. Chezea national service weye!
Mafunzo gani mtu unaenda kwa wiki tatu?Kama ni hivyo sioni wanachoenda kujifunza zaidi ya kupata sifa tu kuwa walienda JKTWatafanya miezi sita kwa sasa, ila hawa waHeshimiwa nasikia wanaenda Wiki 3 tu.
Wana JF, salam!
Nategemea kushiriki mafunzo ya JKT yatakayoshirikisha wabunge vijana. Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU.
Nawatakia ujenzi mwema wa taifa kwa kutumia ubao huu/tuition hii ya bure itoayo elimu ya maisha ie JF.
Jeshini kuna kitu kinaitwa daily order na hii inakufanya usitumie akili kwani kila kitu kinakuwa kimepangwa.Huna nafasi ya kutumia akili yako na ndio maana Mwanajeshi anatii amri.Mwigulu Nchemba, tunakutakia kila la heri, nadhani ukirudi kutoka huko Hautapoteza muda wako kuitukana CHADEMA na viongozi wake. Mafunzo ya Jeshi yanachangamsha akili hautabaki kama ulivyokuwa mwanzo...Mungu akusaidie kabisa
Asante kwa taarifa....
Haya kaka kila la heri, labda ukirudi huko utakuwa umejifunza uzalendo sio "KUVAA SCAFU YA BENDERA YA TANZANIA"Wana JF, salam!
Nategemea kushiriki mafunzo ya JKT yatakayoshirikisha wabunge vijana. Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU.
Nawatakia ujenzi mwema wa taifa kwa kutumia ubao huu/tuition hii ya bure itoayo elimu ya maisha ie JF.
Barua imeonesha muda wa kuanza tu ila najua sio mwaka mmoja ni kipindi kisichopungua wiki tatu wala si zaidi ya miezi mitatu
huo 'UCHAMA' wako usije ukaupeleka JKT. Jifunze kuchagua maneno ya kuongea.Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU
Are you serious? Mwigulu?Hapa kuna kitu Mwigulu si kawaida yako kabisa kutushirikisha mambo yako hapa JF. Ila utakuwa mjanja sana, haya kila la heri kiongozi tunashukuru umegundua kama ya maana yote yanapatikana JF