Nina wasiwasi na hii intake ya jkt..hii iko kisiasa zaidi kuliko madhumuni halisi ya kuanzishwa kwa jkt ya mwl. Nyerere.
Nikiwa ni mmoja wapo wa vjiana tuliomalizia jkt ya mwl. Nyerere mwaka 1993, nilipelekwa jkt makutupola nilichokikuta hapo ni kizazaa. Moja wapo la dhumuni kubwa la jkt ni kuleta usawa kwa watanzania wote yaani mtoto wa mkulima,mfanyakazi,rais,waziri,na viongozi wote kwa ujumla kupata mafunzo na treatment sawa. Hapo makutupola tulikuwa na mtoto wa waziri mkuu msuya, wakati sisi watoto wa walalahoi tukila kwa kunyakuwa kwanza yeye alikuwa anakula sgt mess tena bila bugudha....walio kwenda makutu wataongezea. Hapo usawa uko wapi?
Wale waliokuwa ruvu kazi yao kubwa ilikuwa ni kufuga kuku na kulima bustani, jmosi na jpili ukitaka kwenda kula dar es salaam ilikuwa ruksa.....hapo napo je?
Kwa hawa wabunge wanao kwenda jkt ni kiini macho tu kwani watapata matunzo mazuri kuliko wengine na kambi watakazo kuwa wajeshi hawatachakachua vyakula.....
Makamanda wasasa wamejaa upendeleo na kujuana mno kuliko utendaji wa kazi wa kufuata taratibu na miiko ya kazi zilizopo....hivyo kurudisha jkt ni ufujaji wa fedha za walipa kodi tu. Uzalendo hauletwi na kwenda jkt bwana bali ni matendo ya wananchi wenyewe na viongozi wao... Hao waliokula fedha za epa, kagoda nk mbona wote wame kwenda jkt na wala hawana uzalendo? Usalama wa taifa na majeshi mbona wote wana mafunzo lakini ni madudu mtupu?
Tatizo ni kuendekeza u-ccm, mwenzetu nk bila kuweka utanzania mbele..umeona katibu maswi anamsifu bosi wa eura kwa kusaidia ngoma isitoboke wakati nchi ina kwenda gizani....hicho ndo tatizo
kila raheri na unafiki wenu wa kwenda jkt