Nina Noah, ni biashara gani niweze kufanya?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,277
Habar wakuu, kuna gari Aina ya noah zile za zamani, Sasa najiuliza ni biashara gani niweze kufanya ili niweze kupata pesa kwa kutumia hii gari... Kumbuka kwa usafiri kwa hapa Dar es salaam imekatazwa...naombeni mawazo yenu wakuu, na mungu atawabariki.., au kama kuna connection yoyote ile ya namna ya kuitumia hii gari nijulishe. Mimi napatikana hapa Dar, na hiyo gari pia ipo hapa hapa Dar.
 
Unaweza kuuzia bidhaa yaani ukaligeuza kuwa duka linalotembea kufuata wateja walipo au lililosimama kusubiria wateja waje
 
Nenda kimara mwisho pale upige route za kimara goba ..nauli ni 500 ..naoh ina uwezo wa kupakiza watu 7 mpaka tisa ...kikubwa ni upate kibali tuu

Lakini pia km iko katka condition nzur unaweza ukatafuta connections za kupeleka watoto shule na kuwarudisha ...
 
Unaweza kuuzia bidhaa yaani ukaligeuza kuwa duka linalotembea kufuata wateja walipo au lililosimama kusubiria wateja waje
Mkuu nashukuru kwa ushauri huuu.,....je unaweza kunisaidia ni Aina ganiii ya biashara naweza kufanya ikanipa faida, nikapata pesa ya mafuta.
 
1. Wahi kwenye vituo vya daladala asubuhi sana na pakia watu wapeleke wanapokwenda...

2. Igeuze kua duka... Weka bidhaa simamisha sehemu anza kuuza...

Ngoja waje kukupa muongozo...
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri huuu.,....je unaweza kunisaidia ni Aina ganiii ya biashara naweza kufanya ikanipa faida, nikapata pesa ya mafuta.

Kuna jamaa yangu yeye alikua anasambaza maziwa ya tanga fresh kwenye maduka yaliyo mbali kidogo na mjini... sijui ilikua inamlipa vipi ila ilimfanya mpaka akaondoa viti vya nyuma vyote akawa anaweka zile box/pallets za kuhifadhia mzigo mkunwa wa maziwa..

Kwa sasa sijui anaendeleaje maana nilihama mkoa..
 
Habar wakuu, kuna gari Aina ya noah zile za zamani, Sasa najiuliza ni biashara gani niweze kufanya ili niweze kupata pesa kwa kutumia hii gari... Kumbuka kwa usafiri kwa hapa Dar es salaam imekatazwa...naombeni mawazo yenu wakuu, na mungu atawabariki.., au kama kuna connection yoyote ile ya namna ya kuitumia hii gari nijulishe. Mimi napatikana hapa Dar, na hiyo gari pia ipo hapa hapa Dar.
Peleka babati inalipa sana
 
fanya food truck kitu kipya bongo

truck.jpg

truc.jpg

food truck'.jpg
 
Tupia mkoa huko ilete pesa. Ukishindwa nipe mie nikusimamie ila utalamba laki tu kila wiki. Service na matengenezo madogo juu yangu. Maana yake nakuwa msimamizi. Ndio moja ya biashara zangu kwa miaka 7 sasa. Nnaijua vemaaaaaa tena vemaaa...ukiwa tayari sema tuingie mkataba. Matunzo ya gari ni 100%. Inatembea rami tu. Umbali 45km

Haipigwi mstari na haibadilishwi Rangi
 
Back
Top Bottom