Nina milioni moja na nusu natafuta gari

Nina milioni moja na nusu natafuta gari

Hahahaha kwa hiyo bei utauziwa vyuma sio gari
 
hahahahha......DAAAH....labda uanze kununua matairi manne afu uchange tena baadaae ununue engine na body
 
Watu hawataki kufa bila kutengeneza historia ya kumiliki magari ktk maisha yao....
 
hahaaaaaa kazi kweli kweli

ukistaajabu ya Frank jb hujayaona ya charger
Nina laki 2 nataka kununua gari.Ushauri unahitajika!!

Started by charger, 31st December 2013 09:26
Utani na masihala hapana.Mwaka ndio unaishia hivo na kiukweli malengo yangu yakukusanya angalau laki 2 nimeyafikisha sina budi kujipongeza kwa hilo.

Sasa nahitaji kausafiri kwani nimechoka kutembea kwa miguu,kuna jamaa anataka kuniuzia hiace na amesema ataniuzia kwa laki 2 na nusu.hiyo gari ya mwaka 1975 haina viti ila si mbaya ntachonga hata vya mbao kwa kuanzia na kama mambo yataenda vizuri ntaifanya daladala.mlango wa abiria haufungi ila nayo si hoja abiria atakae kaa mlangoni ataushikilia na kupata punguzo la nauli.sasa wadau bei hiyo ni sawa au jamaa anataka kunigonga sana?na je route ipi italipa vizuri kwa hapa dar iwapo nitaamua kuifanya daladala?

Ushauri tafadhali!
Ushauri unahitajika sana wandugu....

Started by charger, 21st January 2014 11:31
Hamjambo waungwana?Ukiwa na tatizo vizuri kuwashirikisha wenzako.

Ule mchako wangu wa kupata kausafiri umekamilika.Nimepata land rover kwa laki 2 alhamdulilah na mimi kwenye foleni nimo.wapo watakao sema nimekua freemason etc misijali ni wivu tu.
Ila gari langu lina panya sana jamani. Na za kwenu zipo hivi?.Nikiamka asubuhi humo ndani nakutana na kundi la panya utadhani kuna walsha.Cha ajabu hakuna hata mmoja anaekimbilia nje wote wanapotea humohumo ndani.

Tatizo jingine hili gari haliwaki mpaka kusukuma,hii hali inasababisha nikose marafiki kwani nitakae mpa lift ajiandae kuingia gym anytime.Sasa imefikia hatua mpaka vijana pale mtaani wakiniona na paki wanatawanyika .

Hebu mnishauri nimrudishie huyu jamaa gari lake anipe hela yangu? Au nilikarabati nilifanye kibanda cha chips?.Mawazo ndugu zangu.
 
Njoo nikuuzie jeck, spana, taili spare na radio ya gari. Niliuza gari nikabakisha hivyo kwa pesa yako ndio inatosha hivyo vitu otherwise tembelea wanakokata magari ya wizi utapata mpya.
 
tumia hiyo pesa kula misosi ya nguvu ufuge mwili upate BP halali sio hiyo yako ya magumashi unayoitafuta.
 
Kuna mzee mmoja hapa zoo alikuwa anaitwa mwananyoro, ndinga yake ilikuwa ina viti vya matofali, mafuta hayatokei kwenye tanki bali kwenye kidumu kidogo vha lita tano, breki imefungwa na katani ili isicheze, milango ya gari ina makufuli ya vilo, breki kupiga mpaka ashuke awahi akaweke jiwe mbele..gari lilimzeesha mzee mpaka akapata kibiongo mwishowe akaibukia kuwa fundi makenika hatari saaan pale mwanza.

Try at ur own risk!!
 
najua kuna watakaonibeza na wengine kunikatisha tamaa lakini ukweli ni kwamba nahitaj kununua gari la milioni 1.5, kwa mwenye nayo tuwasiliane kupitia namba 0716 002323, nipo dar.

Mkuu Mimi wa ukweli ongeza ela kidogo tuu. nikuuzie gari. inatembea Hali nzuri ipo Kibaha nitafute 0713139208
 
Kuna mzee mmoja hapa zoo alikuwa anaitwa mwananyoro, ndinga yake ilikuwa ina viti vya matofali, mafuta hayatokei kwenye tanki bali kwenye kidumu kidogo vha lita tano, breki imefungwa na katani ili isicheze, milango ya gari ina makufuli ya vilo, breki kupiga mpaka ashuke awahi akaweke jiwe mbele..gari lilimzeesha mzee mpaka akapata kibiongo mwishowe akaibukia kuwa fundi makenika hatari saaan pale mwanza.

Try at ur own risk!!


Yani nimecheka hadi machoz.
Mweeeeeeh had kama fund
 
Kwa nini usinunue boda B tu kama shida ni usafiri? 1.5M ni hela ya kununulia tairi za gari na balance unalipia road licence!
 
Mkuu Mimi wa ukweli ongeza ela kidogo tuu. nikuuzie gari. inatembea Hali nzuri ipo Kibaha nitafute 0713139208
nitumie picha kwenye namba yangu ya whatsup 0657014137 niweze kuiona!
 
huyo miliona moja na nusu ya kenya au ya tz, kama ni ya kenya iyo ni sawa na million 28-30 ya tz. gari la maana tu mbona. funguka tujue dhamani ya pesa yako
 
Back
Top Bottom