Nina mfumo dume au yeye ana mfumo jike?

Haleluyah! Amen.
Mi naongezea tu.
We ulipoenda kuoa ulienda tafuta mtumishi au mke. ?? Huyo ni mke sio mjakazi wako. Tena km mimi ni kaka ya huyo mkeo ningekukata zote kumtumikidha dada yangu kila siku. We shs ngapi unamlipa kukupikia. Kukufulia na kusafisha nyumba?? Mbambaf wahedi!

ndo maana mabinti wa siku hizi hamuolewi mnajazwa mimba mkiwa nyumbani mmezidi kiburi
 
Akili za Kiarabu hizo. Msaidie mkeo kazi za nyumbani, hiyo ndio njia bora ya kudumisha mawasiliano na mapenzi yakaimarika. Usifanye moyo wa mkeo ukawa na malalamiko juu yako, ni chukizo mbele za Mungu na kujikosesha baraka.

Na nyie kina wife, nimesema kusaidia. Hiyo haimaanishi uache vyombo vichafu eti ni zamu ya mume kuosha. Mkiwa mnajinadi hapa JF kutafuta waume mnalia mpaka mnalowesha keyboard zenu na machozi, mkishaolewa mnaota mapembe.

Ni tabia mbaya sana mwanamke kubishana na mumeo, inamchukiza Mungu. Wengine wenu mna mapembe kiasi mnataka kuwaongoza wanaume zenu. Nani kawaambia; mara moja mke alipomuongoza mume, lilikuwa chukizo la kwanza mbele za Mungu.
Mwanzo wa dhambi ulitoka katika mwanamke,
na kwa sababu yake sisi sote tunakufa.

Yoshua Bin Sira 25:24
 
Habar za mchana wakuu, ni wiki ya pili sasa mke akinilalamikia ati nina mfumo dume kisa nimekataa kumsaidia kazi za ndani ikwemo kufua na kupika naombeni member akiendelea kung'ang'ania nimpige chini? Mana anaiga mambo ya kizungu ati tusaidiane

msaidie bwana... Kwani utakatika mikono au uume utachomoka?
 
We tigo. Unatakiwa usome uelewe kwanza ndipo utoe hoja. Nimesema km huyo anaetishiwa talaka kwa kukataa kufanya kazi zoote peke yake .angelikuwa dada yangu basi ningemtafuta huyo shemeji uchwara nikakata zote halafu nikafunua na dada yangu nikarudisha nyumbani.
Na kwa ushauri tu. Hii avatar yako ni alama ambayo inafanana na watu wa sodoma na gomora walio laaniwa naomba ubadilishe kabla laana haija kuangukia na wewe.

Kuna kazi za kufanya mwanamke na kuna kazi ya kufanya mwanaume, baadae mtakuja kutetea hata wanaume wawe wananyonyesha watoto sina wana matiti kifuani mwao.
 
Huo kamwe sio mfumo dume mkuu_ila hiyo sio sababu ya kumpiga chini,..wewe komaa tu kumwambia hautaki.

Keep it up_hayo mambo ya kusaidia kazi za ndani(kuosha vyombo,kufua,kupika etc,..etc..)wacha wafanye waliosoma academy_sisi wa kata sio mambo yetu kabisaaaaaaa....labda aumwe...!

Hahahahhaaaaahhaaaa!!!!!!!! Umeniacha hoooiiiii!!!
 
Kuna kazi za kufanya mwanamke na kuna kazi ya kufanya mwanaume, baadae mtakuja kutetea hata wanaume wawe wananyonyesha watoto sina wana matiti kifuani mwao.

Wewe unajitambua na unajua mipaka ya nani afanye nini_hawawezi kutuzingua na mbinu zao za hila eti haki sawa kwa wote....proudly african.
 
Wewe unajitambua na unajua mipaka ya nani afanye nini_hawawezi kutuzingua na mbinu zao za hila eti haki sawa kwa wote....proudly african.

Yaani wanataka walazimishe tamaduni za watu wengine kwenye ndoa za watu, hili haliwezekani nitaendelea kuwa baba wa kiafrika
 
Ya kiafrica ni yale ya kushika remote, kuangalia futbol, kutuma mpaka kitu kilicho mbele yako pia unamuita wife aje akupe mkononi. Wanaume wa kiswahili bwana...!!!

kumbe kumsaidia mwenzio kazi ni mambo ya kizungu?
na yenu waafrica ndo yapi hayo?
 
Kumsaidia sio tatizo hasa inapotokea mara moja moja!the fact is, na yeye ni binadamu sometimes anachoka especially km nayeye ana kazi nyingi.Kwa upande mwingine jiangalie vzr kwasababu wakati mwingine hawa wanawake wanapendaga sana kupima oil kwa kidole so be carefull!!!!!! ila ukiona vp ajiri housegal!!!
 
hayo tu umpige chini na ukimpata wa kukwambia usimuulize katoka wapi anapochelewa kurudi na kurudi usiku umeshalala na kukwambia uwe unamfungulia mlango je utamfanyaje? tatizo lenu nyie wanaume kabla hamjaoa unapokuwa unamtaka mwanamke unakuta ukimtembelea kwake unafanya hayo yote mnakuwa fake (sio wanaume wote naongelea wale wanofanyaga maana nimeshaona). halafu ukioa unasitisha hayo yote na huwezi jua vigezo vya mwenzio kipindi anatafuta mume vilikuwa nini, yawezekana cha kusaidiana kilikuepo, sasa akijaribu kuomba msaada inageuka tatizo. muwe watu halisi ili mtu akukubali ulivyo. km hujui hata kupika chai anakuwa anajua na hata akiugua unakuta mwenyewe tu anawahi kutafuta mtu wa kumsaidia hizo kazi ndogo mpk apone na hamuwezi kugombana kwa ajili ya hayo mambo madogo.
 
Habar za mchana wakuu, ni wiki ya pili sasa mke akinilalamikia ati nina mfumo dume kisa nimekataa kumsaidia kazi za ndani ikwemo kufua na kupika naombeni member akiendelea kung'ang'ania nimpige chini? Mana anaiga mambo ya kizungu ati tusaidiane
msaidie mkeo ebu wacha habari za kizamani
 
Ya kiafrica ni yale ya kushika remote, kuangalia futbol, kutuma mpaka kitu kilicho mbele yako pia unamuita wife aje akupe mkononi. Wanaume wa kiswahili bwana...!!!

kwakweli huo ni uswahili......
 
unaonyesha una roho mbaya sana, hapo kwenye red hayo si maneno ya kuongea, mnatakiwa mkubaliane na msaidiane, ule ni upendo tu, na si vinginevyo, na huo upendo ndiyo unaleta amani kiasi unaweza kufikiria maendeleo na kuweza kufanya kazi vizuri na kuwa na afya njema wewe na familia yako. lakini ukianza kufanya hayo amani ndani ya nyumba inatoweka kiasi inaharibu kila kitu. jiulize unaweza kuwekeza kwenye vita? kana ndiyo hongera. Naomba futa kauli yako hiyo hapo juu tafadhali.

sifuti kauli mmezidi kuwa wajinga.
 
Habar za mchana wakuu, ni wiki ya pili sasa mke akinilalamikia ati nina mfumo dume kisa nimekataa kumsaidia kazi za ndani ikwemo kufua na kupika naombeni member akiendelea kung'ang'ania nimpige chini? Mana anaiga mambo ya kizungu ati tusaidiane

Huyo ni mkeo kweli? Hauko serious kijana!
 
Hamna kitu kama icho, kama na yeye yuko biz na kusaka hera taften house girl. Mtoto wa kiume ucpende kufanya hzo kaz akiwepo maana mwisho wa cku atakuweka kwnye ratiba kabisa!
 
Habar za mchana wakuu, ni wiki ya pili sasa mke akinilalamikia ati nina mfumo dume kisa nimekataa kumsaidia kazi za ndani ikwemo kufua na kupika naombeni member akiendelea kung'ang'ania nimpige chini? Mana anaiga mambo ya kizungu ati tusaidiane

Kukuomba umsaidie tu ndo tayari ushawaza kama umpige chini!ndomana wake zenu wanazaaga na madereva au houseboys....anyways,inategemea na mnavoishi.wewe ndo unafanya kazi na kuleta mahitaji muhimu nyumbani?mkeo ni housewife au mfanyakazi pia?kama mfanyakazi,uelewe kuwa anachoka.kama housewife,ufikirie kuwa mpaka kakuomba basi alibanwa au alichoka pia..kumsaidia mkeo sio uzungu,ni kushirikiana.yani uafrika kazi kweli kweli!hii mentality itatutesa.mfumo jike ni kama angekupanda kichwani kwa kukukosea heshima coz imempasa mke kumheshimu mume.ila kusaidia kazi ndo unatoka povu hivo?halafu hujui tu,inaimarisha ndoa.mi ukinisaidia kupika,ni turn on tosha..usiku lazima nkupongeze in bed.we hujiskii raha japo siku moja tu,mkeo apumzike wewe ushikilie nyumba?hata watoto wanafurahi.sijui unadefine vipi ndoa na mapenzi jamani.umenishangaza!
 
Bila shaka huyo mwanamke atakuwa na either Diploma,degree au masters coz ni vigumu sana kukutana na tabia hii kwa mwanamke aliyemaliza std7 na form4
 
Imenikumbusha Ile story ya m'me alieomba kwa Mungu ageuzwe m'mke kwa kuwa aliona mkewe hana kazi za kumchosha kwa vile yupo nyumbani tuu. Jamaa siku 1 aliomba arudishwe vile vile, bahati mbaya alikua keshabeba ujauzito hivo ilibidi asubiri kwa miezi 9. Hivi wanaume aliewaambia kama kazi za nyumbani ni za wanawake ni nani? Na hata km ivo ndo tulivozoeshwa ktk malezi yetu kuna ubaya gani kumsaidia mwenzako uliemuoa kwa upendo wote? Kwa m'me anaejali Hicho ni kitu cha kawaida tu.
 
Back
Top Bottom