Nina maumivu sana jamani, nahitaji msaada wenu

Nina maumivu sana jamani, nahitaji msaada wenu

Mahusiano mazuri hujengwa na mawasiliano mazuri kwa kiasi kikubwa bila hivyo kutakuwa na tofauti baina ya ninyi wawili , nakushauri mtafute akueleze tatizo ni nini linalopelekea kupunguza mawasiliano

Wahenga walisema pata pesa tujue tabia yako ,sijui walimaanisha nini...
Hana haja ya kumtafuta chalii angu, apige kimya tu na asonge mbele.
Hivi mahusiano ya 4 month yanaweza kumtesa mtu hivyo eeeh daaah watu tunatofautiana kabisaaa
Kikubwa muombe Mungu sana akutie nguvu. Ukiona sehemu huwezi usijipe shida, omba Mungu atakushika mkono na kukuvusha. Nenda kasome Isaya 41:10 itakuvusha mahali
 
Virginity mbona halijawa tatizo kama unavodhani? Hujui kwanini hapigi au hapokei simu zako na hujajipa muda kujua ni kwanini, pia hujasema amedumu na tabia hiyo kwa muda gani. Miezi minne katika mapenzi sio muda mrefu sana kukufanya upoteze umakini wa kushughulikia mahusiano yenu. Nnachokiona umempenda saana jamaa na huwezi kukaa mbali nae! Kama ukiweza endelea na shughuli zako za kazi/biashara, socialize na watu au kama mtu wa ibada concentrate huko jifanye kama hayupo na muda utaamua hatima yenu bila maumivu
Good advise
 
Unalilia vihela vyako ama? Miezi minne then unasema mlipendana kwa dhati, ulitumia vigezo gani?
Amka endelea na mambo yako, hakuna upendo hapo na wala haujawahi kuwepo!
Hahahahhahaha watu jmn
 
Huyo hakupend tena ndo ukwel cha msing wew jiondoe tu hapo for good utapata maumivu ya mda bt yataisha kuliko kua na mtu kama huyo utaumia kila siku
 
Dah pole sana lakini hataka maka ulimpenda mtu piga moyo konde achana naye kwa una mpenda zaidi ya mzazi wako na kumbuka mzazi mwenye huwa tunamuacha tunakwenda kuanzisha maisha peke yako sasa wewe achana naye
 
wakati wa Bwana ukifka hakika utamfahamu alie wako lakn pia muombe Mungu akupe maarifa ya kumfaham alie wako
 
kuna misingi ya kupenda ukitaka usilie wala kuumia unavyoachana na mpenzi wako.
1) always sleep wt one eye opend..maanake hata penzi likiwa tamu vipi lazima ujue kuna kuacha na kuachwa.
2) all that glitters s not gold...ukiwa na mpenzi na mapenzi motomoto usijisahau kuona kama ndio mwanzo na mwisho.
3) alikudhamini akiwa hana chochote sasa kapata kazi na hela anakuona hufai...jifunze kusoma alama za nyakati...
4) akufukuzae hakwambii nenda...kama jitahidi zako za kutaka mawasiliano zimegonga mwamba ni ishara upo mahala hutakiwi ten.
5) kumlilia wakati yeye alipo hata hana tone ya chozi ni kujiumiza mwenyewe unajitafutia vidoda na stress.
6) yaonekana anajua ulikufa ukaoza kwake na pengine anajua hilo kwake umefika sasa anachukulia advantage.
7) adui namba moja wa uhusiano wowote ni "kua needy, insecure, predictable"
8) hahistahili chozi lako
 
Hana haja ya kumtafuta chalii angu, apige kimya tu na asonge mbele.
Hivi mahusiano ya 4 month yanaweza kumtesa mtu hivyo eeeh daaah watu tunatofautiana kabisaaa
Kikubwa muombe Mungu sana akutie nguvu. Ukiona sehemu huwezi usijipe shida, omba Mungu atakushika mkono na kukuvusha. Nenda kasome Isaya 41:10 itakuvusha mahali

dadangu jje's mimi nilimwambia amtafute ili ajue source ya tatizo . Lakini pia there are sometimes tunakuwa kwenye bad mood na kupelekea kuwa na maamudhi ya majuto baadae namaanisha huyo jamaa] vivyo basi kwa mtazamu wang apige kimya kama jamaa hatajirudi asonge mbele na maisha yake

Ni rahisi wewe na mimi kusema dada yetu amuache mshkaji kirahisi wakati hatujui ni namna gani dada alimhifadhi jamaa moyoni, jamani mapenzi yanauma asikwambie mtu ndyo maana dada ngumu kwake kirahisi

Kwa kumalizia soma maneno haya ya mtunga zabur 'iTazama ilivyo vema na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja.Ni kama mafuta mazuri kichwani,yashukayo ndevuni,ndevu za Haruni,yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.Kama umande wa Hermoni,ushukao milimani pa sayuni,maana ndiko Bwana alikoamuru baraka,Naam uzima hata milele'
 
Aliekuambia mwanaume anapewa ela nani?? MBITIYAZA eti shoga angu,mpenzi umpe ela???sio mume mpenzi tena wa miezi mi4? Unajiumiza bure tu. Sasa ukilia atapokea simu? Haya maliza kulia ndio ujue kuna maisha baada ya kujiliza liza na tuendelee na mambo yako.
 
Aliekuambia mwanaume anapewa ela nani?? MBITIYAZA eti shoga angu,mpenzi umpe ela???sio mume mpenzi tena wa miezi mi4? Unajiumiza bure tu. Sasa ukilia atapokea simu? Haya maliza kulia ndio ujue kuna maisha baada ya kujiliza liza na tuendelee na mambo yako.



hahahahaha uwiii !msamehe mdada hajajitambua km yeye ni wa thamani !mwee ukijitambua wewe ni ya thaman utajipoenda zaid kuliko yyt yule!
 
Habari zenu

Nilikua na mpenzi ambae tumedumu kwa miezi minne sote tulipendana kwa dhati na kwakipindi hicho yeye ndio alikua ameanza kaz hivyo mshahara alikua hajaanza kupata hivyo kila nilipokua na kidogo sikusita kumpatia.

Kilichonifanya nije hapa jamvini ni kwamba mwanaume huyu amebadilika sana, hapigi cm nikipiga hapokei, nikimtumia jumbe hajibu kiukweli hali hii inaniumiza sana nashindwa hata kula,nimekua mtu wa kulia lia kila mara, tafadhali naombeni msaada wenu maana maji yamenifika shingoni.

Hakukupenda kwa dhati huyo aliamua kuwa na wewe kwa misaada yako kimeeleweka kwake akasepa. Pole sana piga moyo konde atakuja wa ukweli
 
Kwani huyo ndio mwanaume wako wakwanza? Tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom