Nina hasira na wife, ushauri wenu please

Nina hasira na wife, ushauri wenu please

Wandugu mimi ni mfanyakazi katika taasisi binafsi ya elimu, nna mke na watoto wawili, nimeishi na mke wangu Sasa mwaka wa 4 baada ya kumzalisha baadae nikamchukua awe mke wangu,

Mwaka Jana mwishoni nlilipa mahari kiasi Cha tsh 1.5m na tumeishi maisha ya amani mpaka leo ila Ana matatizo haya ndio yamenifanya niwaone wakuu:

Mosi, huwa anapata wakati mgumu kunijibu ninapomuuliza kitu

Pili, ni muongo, anaweza kukueleza kwamba alikueleza kitu Fulani wakati hakusema kabisaaa

Tatu, amekuwa mvivu kunifulia hasa baada ya Mimi kufanya kufua nguo kipindi akiwa mgonjwa, now anahisi ni wajibu wangu kufua

Nne, Jambo la Mimi kuoga Wala usimuulize, nna Zaidi ya mwezi sijatengewa maji ya kuoga najitengea mwenyewe

Tano, anapenda Sana kunichunguza Kama nachepuka, juzi tumegombana kwa kusachi simu yangu japo hapakuwa na pa kunikamatia ila kuona sms ya mdada kanisalimia ilikuwa Vita.

Na hii ndio shida kuu, ananivizia usiku anasearch simu yangu Sana na sometime anawapigia wadada nilowasave namba zao, KEROOO

NATAMANI SANA AMANI LAKINI NAHISI ANATAFUTA SHIDA

NISHAACHA UJINGA JAPO HATA YEYE NILIMPATIA UJINGANI LAKINI NAHISI ATANIRUDISHA UJINGANI

USHAURI WENU PLEASE...
Matatizo umeyasabisha mwenyewe ameanza kukujaribu taratibu na wewe ukachukulia poa, mpe onyo kama akiendelea kawaeleze wazazi wake tabia za binti yao, ukiona na wao hawachukui hatua ya kumkanya ukiwepo wewe jua hapo umekula ndoano iteme fasta
 
Una madai ya kijinga, unataka akufulie nguo wewe huna mikono, eti akutengee maji wewe ni kiwete, acha uvivu tafuta hela, bila haya wataka ufuliwe maji yako ya kuoga hutaki kubeba mpaka umtese mkeo hujui ulezi ni kazi?
Acha uvivu aisee
kama una mume basi tambua nae unampa shida kama huyu mleta mada anavyoteseka na vitimbi vya mke wake
 
Unalipa mahari 1.5m halafu unaoga maji ya ndoo au beseni. Hauna running water?
 
Huyo mpe psychological tocha, fanya hivi Kama umeshamuonya Mara kibao hasikii.! Nguo zako peleka dry cleaner Kama hazifui ongea pale ambapo Kuna ulazima ...Kama anaona uvivu kukujibu hizo Ni dharau ..... Simu yako ipige password mpya na kamwe usiruhusu mwanamke ashike sim yako Kuwa Mwanaume usikae kizembe Mwanamke usikae nae kimazoea .

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitashika....
 
Unalipa mahari 1.5m halafu unaoga maji ya ndoo au beseni. Hauna running water?
Jamani maana ya kuandaliwa maji ya kuoga sio lazima kuwekewa ndoo bafuni, (au hujui kuwa hata kwa running water mtu huandaliwa?), hata kukaribishwa tu ile mume wangu karibu kuoga hapo ashaandaliwa bukta au kikoi/msuli wa kuvaa baada ya kuoga.

Babu na baba zetu walifaidi sana wallah
 
Jaribu kuchepuka. Pia weka mfanyakazi wa ndani.
 
Una madai ya kijinga, unataka akufulie nguo wewe huna mikono, eti akutengee maji wewe ni kiwete, acha uvivu tafuta hela, bila haya wataka ufuliwe maji yako ya kuoga hutaki kubeba mpaka umtese mkeo hujui ulezi ni kazi?
Acha uvivu aisee
Kuna mdada alikuwa na mtazamo kama wako, alikuwa anaishi na mumewe lakini hakutaka kufanya shughuli yoyote kuhudumia mumewe, rafiki yake mdada alipoona rafiki yake hahudumii mume, alianza kumkaribisha shemejiye kwake, anamuandalia maji, alianza kumnunulia mshakaji nguo nguo, mara amvue viatu, jamaa akazamia kwa rafiki wa mkewe mazimaaa!

Mdada alipoanza kelele rafiki yake akamwambia, "NATAKA KUKUONYESHA NAMNA YA KUMTUNZA MUME" jamaa mpaka leo anaishi na rafiki wa mkewe!

Mke anamtaka mume wake arudi, lakini jamaa amegoma...ameshanogewa na shemeji yake!

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Yani ningekosa hii coment hapa ningedownload upya JF. [emoji16][emoji16]
 
Kuna mdada alikuwa na mtazamo kama wako, alikuwa anaishi na mumewe lakini hakutaka kufanya shughuli yoyote kuhudumia mumewe, rafiki yake mdada alipoona rafiki yake hahudumii mume, alianza kumkaribisha shemejiye kwake, anamuandalia maji, alianza kumnunulia mshakaji nguo nguo, mara amvue viatu, jamaa akazamia kwa rafiki wa mkewe mazimaaa!

Mdada alipoanza kelele rafiki yake akamwambia, "NATAKA KUKUONYESHA NAMNA YA KUMTUNZA MUME" jamaa mpaka leo anaishi na rafiki wa mkewe!

Mke anamtaka mume wake arudi, lakini jamaa amegoma...ameshanogewa na shemeji yake!

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Aishi tu na huyo rafiki kwa kweli maana ingekuwa wangu kanipunguzia mzigo wa dhambi, sitegemei mtu anifuraishe duniani aisee, nafanya ninachojiskia
 
Baby wangu Hana Mambo ya umwinyi na umangi Meza aisee, na tunaelewana
Kama hajakuoa, akuoe haraka please. Wanaume wa aina hiyo ambao wanapika huku mke anachati ni wachache sana. Hata waziri wa Afya Dr. Gwajima naona kaokota mojawapo.
 
Aishi tu na huyo rafiki kwa kweli maana ingekuwa wangu kanipunguzia mzigo wa dhambi, sitegemei mtu anifuraishe duniani aisee, nafanya ninachojiskia
Ukiona umefikia hatua hiyo maana yake umekata tamaa kabisa, haujengi tena future yako na familia yako, umeamua kuwa selfish kwa kiwango cha juu sana

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Rule number 1; Ajue wewe ndo kichwa cha family brigade nzima commandment inatoka kwa mtu mmoja tu ambae ni wewe mwenyewe
Rule number 2;Simu yako ni yako peke yako hatakiwi kuigusa wala usimpe hiyo nafasi kabisa hujamuoa kuangalia hiyo simu
Rule number3; Muweke wazi kabisa kwamba uwepo wake ni wa muhimu lakini hata asipokuwepo hakuna mahali utafeli mkuu.
Rule number 4; Uongo ni mwiko kwenye ndoa ajue vyema kosa hilo linaweza garimu deportation mchana kwasababu mke muongo ni ugonjwa tayari.
Rule number 5;Ni jukumu lake kuhakikisha unakuwa smart maswala ya kufua hii hapana kuna laundry unaweza peleka ikiwa tu hayuko sawa
ni hizo tano tu mkuu wangu mengine yeshasemwa na baraza
 
Kwa staili anakupa mzigo kweli au ndo anakupa uku anaangalia pemben....
 
Back
Top Bottom