Nimfanyeje huyu mbwa?

Nimfanyeje huyu mbwa?

Ni mbwa wa miezi minne sasa nimemfuga kwa ajili ya ulinzi wa nyumbani. Kinachonishangaza sijawahi kumsikia akibweka zaidi ya siku moja alikuwa anambwekea chura.

Kitu kingine yeye ni rafiki wa kila mtu; mgeni kwa mwenyeji. Nimemfungia weee lakini akipata upenyo wa kukutana na mtu yeyote basi anataka wacheze naye.

Nifanyeje ili awe mkali asiwe na urafiki na kila mtu na awe anabwekea hata mapaka yanayopita usiku?

Yaani alivyo sijui nitamfanya nini zaidi labda ya kumfanya kitoweo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wahi mpeleke chuo kikuu cha porisi Iringa.
 
Unaweza pia kuwafuatilia wazazi wake kujua kama wao na hawakuwa wakali.

Unawezakuta muda mwingine huyo kiumbe anazuga tu au anataka umaarufu tu-anajisikia raha kujadiliwa na maGREAT THINKERS kama sisi.

Rudi ulipomchukua ulizia wazazi wake,utagundua kama tatizo linatibika au la.
 
Ha ha ha aiss we jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom