Nimfanyeje huyu mbwa?

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,663
13,488
Ni mbwa wa miezi minne sasa nimemfuga kwa ajili ya ulinzi wa nyumbani. Kinachonishangaza sijawahi kumsikia akibweka zaidi ya siku moja alikuwa anambwekea chura.

Kitu kingine yeye ni rafiki wa kila mtu; mgeni kwa mwenyeji. Nimemfungia weee lakini akipata upenyo wa kukutana na mtu yeyote basi anataka wacheze naye.

Nifanyeje ili awe mkali asiwe na urafiki na kila mtu na awe anabwekea hata mapaka yanayopita usiku?

Yaani alivyo sijui nitamfanya nini zaidi labda ya kumfanya kitoweo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom