Nimeyatimba: Nimesex na mtu mwenye HIV, ni kipindi kigumu sana maishani mwangu

Aramun

Senior Member
Nov 8, 2023
165
745
IMG_20231104_224035.jpg

Ni single mother mmoja ambaye tulikuwa tunawasiliana naye kwa muda kidogo. Tulishaingiza issues za kusex siku nyingi tuu sema kwenye kukutana ni kama kuna kakitu kanatuzuia.

Siku kadhaa zilizopita siku ikatimia tukaonana na kufanya yetu ya kikubwa. Tulikuwa tumejiandaa kabisa kwamba tutacheki afya zetu hasa HIV kabla hatujafanya chochote. Ila kama mjuavyo penzi la kwanza huwa na nguvu sana, ile tunaingia tuu ndani tumekumbatiana ndo hatukuachiana mpaka kila mmoja alipofika kileleni.

Tumeenda round 2, kisha tukala chakula. Kabla hatujaenda ya 3 ndipo tukakumbuka kupimana. Asalaleeeh!!! Majibu kutoka mwenzangu amewaka, tena amewaka kwelikweli maana hiyo line ya test ilivyo bold siyo mchezo!!!

Kwa kumuangalia mapokeo ya majibu yake ni alikuwa anajua, she knew her status for sure maana chapchap alini-beg nisimpige. Hakujua mimi nina roho ngumu kama paka.

Palepale niliondoka na kwenda hospitali, nikaelezea situation nzima na wakanipa PEP ambazo ndizo napambana nazo mpaka sasa, japo zinazingua kwelikweli lakini hamna namna..

Lengo la kulileta hapa ni ili wana JF wenzangu mjifinze kupitia mimi. Funzo kubwa hapa ni usimuamini yeyote, kabla hamjavuana nguo ni vizuri mkapima kabla, au ikishindikana tumieni njia za ngono salama ili msije mkapitia ninayoyapitia mimi, maana si jambo rahisi.

Funzo la pili mtakalolipata ni matumizi ya PEP kama yanasaidia ama laah. Kwa research zilivyo, PEP zina 80% ya kuzuia maambukizi endapo zinatumiwa inavyopaswa, 20% haziwasaidii na wanapata maambukizi.

Hivyo baada ya kumaliza PEP, itabidi nikae siku 28 ndipo nije nipime. Endapo, nitakuwa NEGATIVE basi nitakuwa nimeangukia kwenye group la 80%, nikiwa POSITIVE basi nitakuwa nimeangukia kwenye group la wale 20%.

Tukutane hapahapa kwenye Next Episode baada ya kumaliza PEP na kupima.
 
Unatakiwa huyo mwanamke umuanike,ni muuzaji kabisa!!

Kumficha ficha hujui ataambukiza wangapi,atapelekea yatima wangapi!!

Unatakiwa umuanike kwa namba zake na ikibidi na picha zake,ni muuzaji!!

Kama mtu anaekutwa na nyama vipande vya swala 12 kafungwa miaka 20+ je huyo muuzaji wa makusudi unamufichia nini?!!
 
Hivyo baada ya kumaliza PEP, itabidi nikae siku 28 ndipo nije nipime. Endapo, nitakuwa NEGATIVE basi nitakuwa nimeangukia kwenye group la 80%, nikiwa POSITIVE basi nitakuwa nimeangukia kwenye group la wale 20%.


Tukutane hapahapa kwenye Next Episode baada ya kumaliza PEP na kupima.[/JUSTIFY]
Tukuweke wimbo gani wa kusindikiza Uzi ndugu mleta mada, Starehe ya Feruzi ft. Prof J au Nimo ya Magwair?

Au ngoja DJ nikuwekee Msinitenge ya Prof J ft. Q Chief tusindikize Uzi
 
Back
Top Bottom