Nimeweza kuacha pombe. Miaka 4 sasa

Nimeweza kuacha pombe. Miaka 4 sasa

tizo1

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
861
Reaction score
159
Habari wadau.

Nashukuru Kwa wote mlio nijenga juu ya namna ya kuacha pombe nilipoomba USHAURI MWAKA 2022. Naelekea miaka 4 Sasa bila kunywa pombe Nilikuwa mlevi sanaaaaaaaaaaaaaaa wa pombe aina zote za dukani na kienyeji.

Nimelewa Toka 2010 mpaka 2022 nimeacha. Mali zimekwisha ila Mimi nipo hai na salama.

Nimeanza upyaaaaaaaa nikiwa na amani tele.

Asante Sana JamiiForums.
 
AA Prayer

1767299182403.png
 
Hongera mkuu

Binafsi nakumbuka mwaka 2016 kulikuwa na kasherehee flani hivi

Basi bhana mitungi ilikuwa ya kujichotea tu

Ikawa Kila nikinywa sisikii hata dalili ya kulewa basi nikawa naongeza zaidi

Si unajua Tena Raha ya pombe ulewe

Basi nimekunywa pale kama masaa matatu ila bado ni kama sijalewa

Imefika muda wa kuondoka kusimama nashangaa naanza kuyumba yumba nikajisemea hapa kimeshaumana

Tembea hatua tatu mara puuh Niko chini kudondoka siyo kudondoka yaani kama gogo

Kuinuka Sasa hapo ndo mgogoro zaidi

Mtu akisimama mbele Yangu naona maluwe luwe tu mtu mmoja naona kama vile wako wawili nikajua Sasa Leo ndo leo

Bahati nzuri nyumbani hapakuwa mbali japo nilifika nimeshadondoka Si chini ya mara sita

Nimekuja kuamka mwili wote haueleweki mpaka nilipata majeraha

Toka Ile siku nikajiapiza Mimi na pombe basi na kweli nikaacha

Kwa Baadae nilikuja kuokoka sema Tena mambo ya utafutaji ndo yamefanya nimekuwa bize
 
Habari wadau.

Nashukuru Kwa wote mlio nijenga juu ya namna ya kuacha pombe nilipoomba USHAURI MWAKA 2022. Naelekea miaka 4 Sasa bila kunywa pombe Nilikuwa mlevi sanaaaaaaaaaaaaaaa wa pombe aina zote za dukani na kienyeji.

Nimelewa Toka 2010 mpaka 2022 nimeacha. Mali zimekwisha ila Mimi nipo hai na salama.

Nimeanza upyaaaaaaaa nikiwa na amani tele.

Asante Sana JamiiForums.
Hela za pombe sasa utakuwa unaenda kuwatajirisha manabii
 
Back
Top Bottom