Kisa cha kweli cha Nazareth Amulike aliyefungwa miaka 9 jela kwa kosa la kusingiziwa na kuachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
298
608
Katika pita pita zangu YouTube nilikua nimeumiss wimbo wa Ambwene mwasonge "unikumbuke" maana hua navutiwana Melody yake pamoja na ujumbe ndani ya wimbo huo.

Wakati nasikiliza wimbo unao simulia kisa Cha kweli Cha Nazareth nikakutana na mahojiano Kati ya Millard ayo na mhusika mwenyewe "Nazareth".

Jamaa ana simulia, sitasahau nilivyo fungwa jera miaka 9 kuanzia 2006-2014 baada ya kuachiwa huru nilipokutwa Sina hatia. Mm ni akari wa jeshi la wananchi la Tanzania JWT mwaka 2016 kulitokea uvamizi wa gari lililo kua likisafirisha pesa pale ubungo mataa.

Baada ya tukio nchi iliingia kwenye taharuki kidogo serikali ikatangaza kwa watu wasamalia wema endapo Kama wataona watu wanafanya manunuzi yenye gharama kubwa pamoja na kunywa pombe kweny mabaa ma kubwana ukawahisi kua wanahusika na tukio/ mtu yoyote unaye muhisi Basi toa raafika kupitia namba tajwa hizi.

Kwa bahati mbaya zaidi ilikua ni siku ya mwisho wa mwezi, mm na mke wangu sote tulikua ni Askari wa jeshi la wananchi JWTZ, wakati huo ndio mshahara ulikua umetoka Sasa walikua na uhitaji wa viti sofa, na kulikua na mhusika mmoja wa huko masaki alikua anauza zile sofa, mke wangu akanipa taarifa tukaenda kuziona na hatimaye tukazichukua.

Skua na wasiwasi kwakua mm skua mhusika wa tukio lakini kulingana na Aina ya kazi yangu niliamini kua nisinge weza kutiliwa Shaka, bahati mbaya majirani zetu waliona wakati nikizishusha zile sofa viti, asee hapo ndo ukawa mwanzo wa safari yangu ya maisha ya jera, wale majirani walio niona walinilipoti.

Kwa mda ambao skutarajia nilishangaa gari askari police wamefika nyumbani kwangu na kunambia wanataka wakague ndani ya nyumba yangu Kama wangekuta siraha na pesa nilizo hifadhi ndani, niliwaruhusu wakakagua na hawakuona kitu, walituchukua Mimi pamoja na mke wangu na mtoto wetu mdogo wa miezi 7 mpaka kituo Cha police kwa mahojiano.

Tukafika pale kituo Cha police wakatuhoji kwa zamu mm na mke wangu, hasa waliuliza sku ya tukio nilikua wapi, niliwajibu kua nilikua kazini "zamu" na nilirejea nyumbani kwangu.

Na mke wangu pia alieleza uharisia Kama nilivyo waeleza, wao wakadai nibaki kwa maelezo Zaid mm na mke wangu tukawekwa rockup mm ya wanaume huku mke WANGU ya wanawake kule, huu ndo ulikua mwisho wa kukaa na familia yangu.

Nilikaa pale rockup siku ya tatu mke wangu alirejea nyumbani na kuniacha Mimi kituo cha police nikiendelea na upelelezi.

waliniletea wapelelezi wa karibu mkoa mzima lakini wote walisema mbele yangu kua walie nikamata sio mhusika waniachie tu Sasa wakawa bado wanakusanya ushahidi ilia waniachie ukiangalia na nchi ilivo kua kwenye taharuki pamoja na ninyi waandishi wa habari tayari mambo mlikua mmesha yapeleka kwenye jamii kua washukiwa wa ujambazi wakamatwa wengine watambuliwa sura zao. Ilikua kashehe.

Baadae wakaleta mashahidi. moja ya shahidi alikua ni Askari police Alie kua zamu pale mataa, aliletwa kutuangalia aone Kama angeweza kuwafahamu wahusika akatuangaliaa alipo fika kwangu akasema niliona umbo kama hilii. Aaah! tayariii hapohapo nikageuka kua mharifu Sasa nikawa Sina utetezi Tena.

Tulipelekwa mahakamani kwa ajili ya kesi, mke wangu alikua anakuja kuniona mala kwa mala bahati mbaya mke wangu na mwanangu walifariki hapa ni miaka miwili baada ya yeye kukaa rumande.

Anasimulia tukio la mke na mtoto kufariki.

Wakati nipo rumande ndugu zangu walipendekeza mke wangu (familia yangu) ihame ilipo kua ikikaa kwakua tuliona tumezungukwa na maadui tayari. Nililetewa taarifa nami nilibariki familia ikahama, Sasa kule waliko hamia siku ya tukio mke wangu alikua ametoka kazini "zamu" ya mchana karudi kachoka alikua chumbani ana nyonyesha mtoto akapitiwa usingizi.

Dada wa kazi alikua ametoka kidogo alikua kaenda dukani wakati huku nyumbani alikua kaacha mshumaa ukiwaka kwenye kisosi si unajua mambo ya zamani na tule tu visosi, kwa bahati mbaya mshumaa ulidondokea kwenye sofa ukaanza kuwaka.

Wakati dada wakazi anarudi anamuamsha mama Moto ulikua umesha waka sebuleni mama akatoka anakimbia alipofika nje akakumbuka kamuacha mtoto ndani ikambidi amrudie mtoto ndani, wakati anatoka mtoto akadodoka chini kitendo Cha kumuokota tayari Moto ulikua umesha waunguza vibaya, ila walifanikiwa kutoka Basi ikabidi wanachi wampeleke mtoto na mama hospital Kwanza.

Walipo fika mtoto alifariki kesho yake, nikaletewa taarifa nikiwa gerezani ("hapa msimuliaji anasimulia kwa uchungu huku akimeza mate kuzuia chozi la uchungu") nikamshukuru Mungu nikasema Basi Kama Mungu kamruhusu mtoto wetu aondoke Basi tutapata mwingine siku nikitoka gerezani maadamu mke wangu yu hai, baada ya siku mbili aliletewa taarifa pia mke wake afariki.

Kiukweli niuchungu Sana usio elezeka bahati mbaya ukiwa gerezani hupati hata nafasi ya kuhuzuria mazishi, lakini namshukuru Mungu alinitia nguvu.

Baada ya mwaka mmoja ambapo ni miaka mitatu toka awe mahabusu dada yake pia alieye kua akifanya kazi na mke wake JWTZ alifariki kwa mshituko wa moyo hivyo akawa amempoteza mke wake,mtoto wake pomoja na dada yake.

Awali nilikua nalipwa mshahara wangu hatimaye nusu mshahara lakini baada ya dada angu kua amefariki 2009 na pia nilipokea barua ya kuachishwa kazi rasmi na nilipo achishwa kazi mshahara wangu pia ulikoma. Nikiwa gerezani.

Mwandishi ana anamuuliza ni vitu gani hawezi kuvisahau alipo kua gerezani.?..

aaah maisha ya gerezani hapana kwakweli Yale maisha ni mateso Sana nisingependa mtu yoyote aende kule, nilikua nakereka na zile filimbi za gerezani, zilikua zikitokea hasa pale ambapo wamepata taarifa ya uwepo wa mtu mwenye simu gerezani kwasababu Simi ilikua inahatarisha usalama wa nchi na magereza, walikua wakipuliza filimbi basi kila mtu anatakiwa alale chini chali Kisha virungu vinaanza kutembea mpaka mta sema tu.

Kingine maisha ya jera yanachosha, Kuna wakati walikua wanachelewa kutufungulia kutokana na vikao vyao vya wikendi, ashumu umelala saa 9 alasiri mnakuja kufunguliwa kesho yake saa 5 mpaka 6 wakati mwingine, asee nilikua nakerwa Sana.

Bahati nzuri mm nilikua na nizamu ya hali ya juu mpaka ikafika hatua nikaaminiwa kua mkuu wa wanyampala magereza mawili ukonga na segerea ilikua ni zaidi ya wafungwa 1000 Basi kwangu kidogo ilinipa uafadhari.

Anaeleza namna alivo ishi kwa nizamu...

Maisha ya gerezani ni mabaya mno kuna watu hugeuka machizi punde tu wakifikishwa mle asilimia ya wengi kesi niza kusingiziwa Kama Mimi hapa, kule Kuna magojwa na watu hufa Sana Sana hasa wenye magonjwa Yale ambayo yanahitaji uangalizi Kama ukimwi, kisukari n.k

Sasa mimi baada ya kufika mle nilikua na mawazo Sana Sana niliona Sina msaada tofauti na Mungu tu, baada ya kua amekufa mke wangu niliona Sina Tena tumaini nilitamani kufa lakini haikuwezekana.

Nikiwa gerezani nilipata kitabu Cha askofu mmoja kilicho zungumzia habari ya KUSAMEHE NA KUSAHAU, kile kitabu nilikisoma chote hakika kilinijenga Sana Sana niliamua kusamehe kwa dhati mpaka leo, kwahiyo niliamua kuokoka na nilikua na bidii Sana mpaka mchungaji wa gereza aliniomba niwe mchungaji msaidizi hatimaye nikawa mchungaji rasmi baada ya yeye kua na ratiba nyingi za nje akawa haji Tena gerezani.

Ilinibidi niamue kuacha unyampala nimtumikie Mungu tu mle gerezani kidogo utumishi gerezani ulinipa heshima.

Anakazia kwenye msamaha na kusema...
.. hata yule jirani Aliye turipoti na yule Askari trafiki Aliye nifananisha umbo nimesha msamehe, yule jirani Nina mjua maana haiikua Siri Tena Kati yetu na yeye lakini sita msema popote kua ni flani maana nimesha msamehe kabisa.

Hali ya uendeshaji wa kesi ilikia niya taratibu Sana maana walio kua mashahidi baadhi walikua ni Askari police na walipelekwa coz kusoma nje ya nchi kwaio tulikua tunawasubiri wamalize coz ndo waje watoe ushahidi mpaka ilipo fika mwaka 2014 nilipo onekana Sina hatia na kuachiwa huru.

Mwandishi anauliza vipi vilimshangaza huku uraiani baada ya pale alipo ambiwa kaachiwa huru.

Ana simuliaa.. kwakweli nilishangaa nikajiuliza hivi nipo ulaya au Tanzania hapo kumbuka nilifungwa tangu 2006 mpaka 2014 nilishangaa kukuta mji umependeza majengo, magari ni mengi watu wengi mala smart phone mala kile.

Nilipotoka gerezani ilinichukua mda kukaa Sawa ndipo nilipo amini kua nikweli mke na mwanangu walifariki, ila namshukuru Mungu kwasasa nimeoa na tumebarikiwa mtoto mmoja, ilinichukua muda kuamini Kama ningeweza kupata mke ambaye anafanana na mke wangu.

Tangu 2014 nilikua naishi kwa Kaka yangu baadae nikajiona nimekua 2018 nikaondoka rasmi kujitegemea baada ya kua nime kaa Sawa ki saikolojia.

Mwandishi anauliza hatima ya kazi yake.

Anasimulia nilipotoka gerezani nilifatilia.
. niliwaandikia barua makao makuu lakini walijibu kua niliachishwa kazi kwa mujibu wa sheria, lakini sheria inasema kua Askari ataachishwa kazi endapo Kama atakua na utoro/ kuugua kwa mda mrefu lakini mm serikali ndio ilinikamata na ikanikuta Sina hatia.

Nilimwandikia barua mpaka mkuu wa majeshi wa wakati ule alinijibu vile vile ikabidi nimwandike barua hayati magufuli alinijibu na kumwagiza waziri wa ulinzi kua wanishughulikie lakini mpaka leo imekua kimya, Nina mpango wa kumwandikia rais mama Samia naimani kilio changu atakisikia.

Hali yangu ya maisha haijawa Kama ile ya mwanzo ila namshukuru Mungu Nina sehemu inayo nipeleka na jioni Nina Rudi nyumbani nikiwa na chochote kiukweli nalipenda jeshi bado umri wangu una ruhusu kulitumikia, kwanza Mimi bado ni Askari jeshi kwakua Nina viapo vyote vya Siri vya nchi.

Hata hivyo msimliaji anasema kua mahakama iliwahukumu adhabu ya kunyongwa mpaka kufa wahusika tukio Hilo.
 
Dah sijalia siku nyingi zaidi ya miaka minne ila leo namalizia kusoma hiki kisa nusura machozi yanilenge dah hakuna namna ngoja nikapige ka kvant kadogo kwanza sote hatujui siku wala saa ambao jambo lisilotarajiwa litakutokea
 
Dah sijalia siku nyingi zaidi ya miaka minne ila leo namalizia kusima hiki kisa nusura machozi yanilenge dah hakuna namna ngoja nikapige ka kvant kadogo kwanza sotr hatujui siku wala saa ambao jambo lisilotarajiwa litakutokea
Kwakweli nikisa Cha kusisimua bahati mabaya nicha kweli, inaumiza Sana kuona maizingira Kama haya yalimpata binadamu.

Kiukweli inaumiza sana
 
Dunia ina mengi saaana jamani nikisikilizaga huu wimbo nawazaga mengi sana
 
Umasikini wetu husababisha sana haya mambo.

Just imagine sofa zisababishwe mtu aende jela kweli...?
Na wapo wengi kule Gerezani wasio na hatia na wanatumikia kifungo kigumu kweli kweli.
 
Na msimuliaji kalieleza hili Jambo Kuna watu wamefungwa wengi Sana kwa kesi kubwa za kusingiziwa za ubakaji na uuaji lakini ukifatilia uharisia unakuta kumbe walipishana na boss wa kitengo flani eidha kwa kugombania MWANAMKE au mipiaka ya viwanja.
 
Katika pita pita zangu YouTube nilikua nimeumiss wimbo wa Ambwene mwasonge "unikumbuke" maana hua navutiwana Melody yake pamoja na ujumbe ndani ya wimbo huo.

Wakati nasikiliza wimbo unao simulia kisa Cha kweli Cha Nazareth nikakutana na mahojiano Kati ya Millard ayo na mhusika mwenyewe "Nazareth".

Jamaa ana simulia, sitasahau nilivyo fungwa jera miaka 9 kuanzia 2006-2014 baada ya kuachiwa huru nilipokutwa Sina hatia. Mm ni akari wa jeshi la wananchi la Tanzania JWT mwaka 2016 kulitokea uvamizi wa gari lililo kua likisafirisha pesa pale ubungo mataa.

Baada ya tukio nchi iliingia kwenye taharuki kidogo serikali ikatangaza kwa watu wasamalia wema endapo Kama wataona watu wanafanya manunuzi yenye gharama kubwa pamoja na kunywa pombe kweny mabaa ma kubwana ukawahisi kua wanahusika na tukio/ mtu yoyote unaye muhisi Basi toa raafika kupitia namba tajwa hizi.

Kwa bahati mbaya zaidi ilikua ni siku ya mwisho wa mwezi, mm na mke wangu sote tulikua ni Askari wa jeshi la wananchi JWTZ, wakati huo ndio mshahara ulikua umetoka Sasa walikua na uhitaji wa viti sofa, na kulikua na mhusika mmoja wa huko masaki alikua anauza zile sofa, mke wangu akanipa taarifa tukaenda kuziona na hatimaye tukazichukua.

Skua na wasiwasi kwakua mm skua mhusika wa tukio lakini kulingana na Aina ya kazi yangu niliamini kua nisinge weza kutiliwa Shaka, bahati mbaya majirani zetu waliona wakati nikizishusha zile sofa viti, asee hapo ndo ukawa mwanzo wa safari yangu ya maisha ya jera, wale majirani walio niona walinilipoti.

Kwa mda ambao skutarajia nilishangaa gari askari police wamefika nyumbani kwangu na kunambia wanataka wakague ndani ya nyumba yangu Kama wangekuta siraha na pesa nilizo hifadhi ndani, niliwaruhusu wakakagua na hawakuona kitu, walituchukua Mimi pamoja na mke wangu na mtoto wetu mdogo wa miezi 7 mpaka kituo Cha police kwa mahojiano.

Tukafika pale kituo Cha police wakatuhoji kwa zamu mm na mke wangu, hasa waliuliza sku ya tukio nilikua wapi, niliwajibu kua nilikua kazini "zamu" na nilirejea nyumbani kwangu.

Na mke wangu pia alieleza uharisia Kama nilivyo waeleza, wao wakadai nibaki kwa maelezo Zaid mm na mke wangu tukawekwa rockup mm ya wanaume huku mke WANGU ya wanawake kule, huu ndo ulikua mwisho wa kukaa na familia yangu.

Nilikaa pale rockup siku ya tatu mke wangu alirejea nyumbani na kuniacha Mimi kituo cha police nikiendelea na upelelezi.

waliniletea wapelelezi wa karibu mkoa mzima lakini wote walisema mbele yangu kua walie nikamata sio mhusika waniachie tu Sasa wakawa bado wanakusanya ushahidi ilia waniachie ukiangalia na nchi ilivo kua kwenye taharuki pamoja na ninyi waandishi wa habari tayari mambo mlikua mmesha yapeleka kwenye jamii kua washukiwa wa ujambazi wakamatwa wengine watambuliwa sura zao. Ilikua kashehe.

Baadae wakaleta mashahidi. moja ya shahidi alikua ni Askari police Alie kua zamu pale mataa, aliletwa kutuangalia aone Kama angeweza kuwafahamu wahusika akatuangaliaa alipo fika kwangu akasema niliona umbo kama hilii. Aaah! tayariii hapohapo nikageuka kua mharifu Sasa nikawa Sina utetezi Tena.

Tulipelekwa mahakamani kwa ajili ya kesi, mke wangu alikua anakuja kuniona mala kwa mala bahati mbaya mke wangu na mwanangu walifariki hapa ni miaka miwili baada ya yeye kukaa rumande.

Anasimulia tukio la mke na mtoto kufariki.

Wakati nipo rumande ndugu zangu walipendekeza mke wangu (familia yangu) ihame ilipo kua ikikaa kwakua tuliona tumezungukwa na maadui tayari. Nililetewa taarifa nami nilibariki familia ikahama, Sasa kule waliko hamia siku ya tukio mke wangu alikua ametoka kazini "zamu" ya mchana karudi kachoka alikua chumbani ana nyonyesha mtoto akapitiwa usingizi.

Dada wa kazi alikua ametoka kidogo alikua kaenda dukani wakati huku nyumbani alikua kaacha mshumaa ukiwaka kwenye kisosi si unajua mambo ya zamani na tule tu visosi, kwa bahati mbaya mshumaa ulidondokea kwenye sofa ukaanza kuwaka.

Wakati dada wakazi anarudi anamuamsha mama Moto ulikua umesha waka sebuleni mama akatoka anakimbia alipofika nje akakumbuka kamuacha mtoto ndani ikambidi amrudie mtoto ndani, wakati anatoka mtoto akadodoka chini kitendo Cha kumuokota tayari Moto ulikua umesha waunguza vibaya, ila walifanikiwa kutoka Basi ikabidi wanachi wampeleke mtoto na mama hospital Kwanza.

Walipo fika mtoto alifariki kesho yake, nikaletewa taarifa nikiwa gerezani ("hapa msimuliaji anasimulia kwa uchungu huku akimeza mate kuzuia chozi la uchungu") nikamshukuru Mungu nikasema Basi Kama Mungu kamruhusu mtoto wetu aondoke Basi tutapata mwingine siku nikitoka gerezani maadamu mke wangu yu hai, baada ya siku mbili aliletewa taarifa pia mke wake afariki.

Kiukweli niuchungu Sana usio elezeka bahati mbaya ukiwa gerezani hupati hata nafasi ya kuhuzuria mazishi, lakini namshukuru Mungu alinitia nguvu.

Baada ya mwaka mmoja ambapo ni miaka mitatu toka awe mahabusu dada yake pia alieye kua akifanya kazi na mke wake JWTZ alifariki kwa mshituko wa moyo hivyo akawa amempoteza mke wake,mtoto wake pomoja na dada yake.

Awali nilikua nalipwa mshahara wangu hatimaye nusu mshahara lakini baada ya dada angu kua amefariki 2009 na pia nilipokea barua ya kuachishwa kazi rasmi na nilipo achishwa kazi mshahara wangu pia ulikoma. Nikiwa gerezani.

Mwandishi ana anamuuliza ni vitu gani hawezi kuvisahau alipo kua gerezani.?..

aaah maisha ya gerezani hapana kwakweli Yale maisha ni mateso Sana nisingependa mtu yoyote aende kule, nilikua nakereka na zile filimbi za gerezani, zilikua zikitokea hasa pale ambapo wamepata taarifa ya uwepo wa mtu mwenye simu gerezani kwasababu Simi ilikua inahatarisha usalama wa nchi na magereza, walikua wakipuliza filimbi basi kila mtu anatakiwa alale chini chali Kisha virungu vinaanza kutembea mpaka mta sema tu.

Kingine maisha ya jera yanachosha, Kuna wakati walikua wanachelewa kutufungulia kutokana na vikao vyao vya wikendi, ashumu umelala saa 9 alasiri mnakuja kufunguliwa kesho yake saa 5 mpaka 6 wakati mwingine, asee nilikua nakerwa Sana.

Bahati nzuri mm nilikua na nizamu ya hali ya juu mpaka ikafika hatua nikaaminiwa kua mkuu wa wanyampala magereza mawili ukonga na segerea ilikua ni zaidi ya wafungwa 1000 Basi kwangu kidogo ilinipa uafadhari.

Anaeleza namna alivo ishi kwa nizamu...

Maisha ya gerezani ni mabaya mno kuna watu hugeuka machizi punde tu wakifikishwa mle asilimia ya wengi kesi niza kusingiziwa Kama Mimi hapa, kule Kuna magojwa na watu hufa Sana Sana hasa wenye magonjwa Yale ambayo yanahitaji uangalizi Kama ukimwi, kisukari n.k

Sasa mimi baada ya kufika mle nilikua na mawazo Sana Sana niliona Sina msaada tofauti na Mungu tu, baada ya kua amekufa mke wangu niliona Sina Tena tumaini nilitamani kufa lakini haikuwezekana.

Nikiwa gerezani nilipata kitabu Cha askofu mmoja kilicho zungumzia habari ya KUSAMEHE NA KUSAHAU, kile kitabu nilikisoma chote hakika kilinijenga Sana Sana niliamua kusamehe kwa dhati mpaka leo, kwahiyo niliamua kuokoka na nilikua na bidii Sana mpaka mchungaji wa gereza aliniomba niwe mchungaji msaidizi hatimaye nikawa mchungaji rasmi baada ya yeye kua na ratiba nyingi za nje akawa haji Tena gerezani.

Ilinibidi niamue kuacha unyampala nimtumikie Mungu tu mle gerezani kidogo utumishi gerezani ulinipa heshima.

Anakazia kwenye msamaha na kusema...
.. hata yule jirani Aliye turipoti na yule Askari trafiki Aliye nifananisha umbo nimesha msamehe, yule jirani Nina mjua maana haiikua Siri Tena Kati yetu na yeye lakini sita msema popote kua ni flani maana nimesha msamehe kabisa.

Hali ya uendeshaji wa kesi ilikia niya taratibu Sana maana walio kua mashahidi baadhi walikua ni Askari police na walipelekwa coz kusoma nje ya nchi kwaio tulikua tunawasubiri wamalize coz ndo waje watoe ushahidi mpaka ilipo fika mwaka 2014 nilipo onekana Sina hatia na kuachiwa huru.

Mwandishi anauliza vipi vilimshangaza huku uraiani baada ya pale alipo ambiwa kaachiwa huru.

Ana simuliaa.. kwakweli nilishangaa nikajiuliza hivi nipo ulaya au Tanzania hapo kumbuka nilifungwa tangu 2006 mpaka 2014 nilishangaa kukuta mji umependeza majengo, magari ni mengi watu wengi mala smart phone mala kile.

Nilipotoka gerezani ilinichukua mda kukaa Sawa ndipo nilipo amini kua nikweli mke na mwanangu walifariki, ila namshukuru Mungu kwasasa nimeoa na tumebarikiwa mtoto mmoja, ilinichukua muda kuamini Kama ningeweza kupata mke ambaye anafanana na mke wangu.

Tangu 2014 nilikua naishi kwa Kaka yangu baadae nikajiona nimekua 2018 nikaondoka rasmi kujitegemea baada ya kua nime kaa Sawa ki saikolojia.

Mwandishi anauliza hatima ya kazi yake.

Anasimulia nilipotoka gerezani nilifatilia.
. niliwaandikia barua makao makuu lakini walijibu kua niliachishwa kazi kwa mujibu wa sheria, lakini sheria inasema kua Askari ataachishwa kazi endapo Kama atakua na utoro/ kuugua kwa mda mrefu lakini mm serikali ndio ilinikamata na ikanikuta Sina hatia.

Nilimwandikia barua mpaka mkuu wa majeshi wa wakati ule alinijibu vile vile ikabidi nimwandike barua hayati magufuli alinijibu na kumwagiza waziri wa ulinzi kua wanishughulikie lakini mpaka leo imekua kimya, Nina mpango wa kumwandikia rais mama Samia naimani kilio changu atakisikia.

Hali yangu ya maisha haijawa Kama ile ya mwanzo ila namshukuru Mungu Nina sehemu inayo nipeleka na jioni Nina Rudi nyumbani nikiwa na chochote kiukweli nalipenda jeshi bado umri wangu una ruhusu kulitumikia, kwanza Mimi bado ni Askari jeshi kwakua Nina viapo vyote vya Siri vya nchi.

Hata hivyo msimliaji anasema kua mahakama iliwahukumu adhabu ya kunyongwa mpaka kufa wahusika tukio Hilo.
Mapito haya,imeniuma sn
 
Mimi sijui kama ningemsamehe huyo mwamba aliesababisha, labda tu nikose access ya kulipiza.

Askari siwezi mlaumu sana coz alitumia hisia na huenda alikua na hasira, ila huyo jirani ningekula nae sahani moja..
 
Back
Top Bottom