Nimevutiwa mno na Jiji la Mwanza

Nimevutiwa mno na Jiji la Mwanza

Hakuna jipya zaidi ya matukio ya ujambazi.....nikiambiwa nitaje miji iliyoko kanda ya ziwa inayoongoza kwa matukio ya unyang'anyi wa kutumia siraha naanza na mwanza..Geita..hiyo miji miwili wala bata wengi wamejificha kwenye kichaka cha kwamba wanajishughulisha na ishu za madini pamoja na uvuvi.....ukweli ni kuwa wengi ni majambazi.....kituko ni kwamba gereza la butimba huwa halikauki...kila siku linasomba nyomi ya raia...ukiwa mle ndani ni kama sokoni
Umefanya GENERALIZE mkuu, Umeielewa mada si kwa usahihi.

Ni mkoa upi usio na wafungwa hapa TZ?
Ni mkoa upi usiokuwa na MAGEREZA hapa TZ?

Kuna mahali ambako MAJAMBAZI hawapo hapa TZ?

Taja MIKOA 5 inayoongoza kwa rekodi ya UJAMBAZI hapa TZ tuone kama MWANZA imo katika rekodi hiyo?.

NOTE: Hatukuongelea UGAIDI, UJAMBAZI, wala UHALIFU bali tumeongelea "MAENEO YANAYOVUTIA" au "TULIVU" kwa ajili ya MGENI ku-refresh MIND, KUTALII, N.K
 
Unaonekana mwenyeji sana sasa nielekeze wapi nikienda napata kitu ugali dona uliopikwa kwa viwango vinavyotakiwa na samaki ambae hakupita kwenye fridge sehemu ambayo nikitoa elfu kumi yangu natoka nijisemea nimekula. Namaanisha smakaki sio kijisamaki samaki hasa sato
Punguza kula kula ovyo. Ndio maana limwili minyama minyana ya kizembe kama mcheza sumo[emoji1783][emoji1783]

Sent from my CPH2127 using JamiiForums mobile app
 
Habarini za muda huu nduguzangu wa Jamii Forum.
Niende moja kwa moja kwenye Mada kuelezea vile nimepata kujionea utofauti wa jiji la Mwanza tangu siku yangu ya kwanza tu kufika.
Safari ilikuwa ngumu mpaka nikajiuliza nina mkosi maana gari liliharibika mara tatu, hatimaye majira ya saa nane za usiku ndio nikafika Mwanza, Jiji nililokuwa nalisikia tu na kupata sifa nyingi ila sijawahi kufika.
Siku yangu ya kwanza niliona mambo mengi tafauti na Dar es salaam au jiji la Daudi. Watu wa Mwanza ni wakarimu mno ani ukimuuliza anaweza kukujibu vizuri, Makonda na Madereva daladala wako vizuri nilipanda daladala nakaribia kufika kituoni nikasimama akaniambia kaa mpaka gari lisimame ani nilishazoea Dar gari hata halijasimama vizuri utasikia konda anamwambia dereva twende.
Mwanza kuna mandhari nzuri na hali ya hewa safi. Navutiwa zaidi na mawe hasa yaliyo karibu na nyumba, unakuta nyumba imejengwa nyuma kuna bonge la jiwe..

Enewei nina wiki tu jijini Mwanza anayejua maeneo mazuri ya kuvutia maana napenda sana kutalii. Ahsanteni


KichWa bOX
Kabisa kabisa. Mzee katoka Shinyanga, mama pure mjita, nina ndugu Mwanza, nilipowatembelea 4 yrs ago nami nilifarijika kama wewe, nami mkazi wa Dar, purukshani za jiji hili la bandari ya salama si mchezo, Mwanza palinikosha na ustaarabu wake, kuanzia wakazi wake, wanausafiri, hotelini, bar, mpaka zile sehemu kama kona bar, hata wale wanyama porini nawo walikuwa wastaarabu, hakuna longo longo wala kuibiana, wala kukutosa baada ya misosi na vinywaji, hawana mapepe kama hawa wetu uzaramuni. Hatujaongea swala la samaki, ni kuzuri kwa kweli. Hata usafi wa jiji. Mwanza Oyeeee
 
Ginehe nkoi? Usijali chief, mji utapendeza sana na mazingira yatakuwa safi kutokuwa na machinga.
Kwa hilo ni sawaa mkuu..kuna mitaa kama liberty ilikuwa kero sanàa...ila ukipita ss iv unakuwa comfortable sanaa...kpnd cha nyuma hapo yani ilikuwa ni hatar sanaa kwa usalama wako maana pkpk ilikuwa inakuja kupigia honi kweny miguu bila kuiona
 
Wilaya tarajiwa makao makuu yake ni Fela
Kisesa ni mjii unaokuwa kwa kasi ...nafikur ni sehem nzur ya kuchukua eneo..ila kishir kuna tetesi kuwa itakuwa makao makuu ya wilaya inayoanzishwa kwa hyo ni hot cake pia...sema changamoto ya kishiri ina milima sanaa na uhaba wa maji baadh ya maeneo
 
Buhongwa ni habari nyingine. Ukitaka kujenga nenda Nyashishi au Nyag'homango maana zinaungana na Buhongwa kwa kasi
Buhongwa ina watu wengi kuliko downtown pia pamechangamka sana, pia inakadiriwa buhongwa pekee inawatu 100000 na igoma ina watu 60000.
 
Kesho kutwa naenda kula misamaki Mwanza

Wapi wanapika vizuri, maana samaki asipoiva ni utaharishaa usiku kucha!
 
Back
Top Bottom