Nimevutiwa mno na Jiji la Mwanza

Nimevutiwa mno na Jiji la Mwanza

Mmepasifia sana Mwanza mwezi wa 12 natia timu nikajionee mwenyewe.
Mimi ki asili kabisa wazazi wangu nature yao ni kutoka mikoa mingine tofauti ila walivyokutana hapa na kuanza maisha nikazaliwa hapa hapa Mwanza ila isiwe sababu ila ki ukweli nimefanikiwa sana kufika mikoa mingi hii nchi na baadhi niliweka makazi ya utafutaji ila bado nikaona Mwanza napapenda na inanivutia nikaamua kurudi kuweka kambi rasmi make nlkuaga naja kusalimia ndugu na kuondoka kwenda kutafuta mbali huko..

So KARIBU sana Mwanza ujionee utofauti na Uzalamoni.
 
1.Idara ya maji-Hesawa-Capripoint.

2.Jiwe kuu-Kitangiri-Bwiru (Hapo Jiwe kuu utaziona alama zimetokeza juu ja mawe za mikono,vidole vya mfalme wa kale wa Kisukuma "Ng'wana Malundi".

3.Darajani-Furahisha-Kirumba.

4.Darajani-Mabatini.

5.Bismarck Rock-Kamanga-Nyamagana "utaona nondo zimechomekwa na kuzama ndani ya jiwe".

6.Nyumba juu ya nyumba, Jiwe mbele ya nyumba, nyuma ya nyumba na juu ya nyumba. -SAHARA-Pamba-Mwanza.

7.Bugando Jeshini, Bugando Hospital, Bugando Mission, Bugando Nkali na Bugando Kati [Kata ya Igogo].

8.Isamilo lodge, Mjimwema, Nyashana, na Mbugani.

9.Mwaloni-Magomeni, Kigoto, Ibanda, Bujumbura-Kirumba.

NOTE: KAMA HAUTAFIKA "SAHARA" HAUTAKUWA UMEIFIKIA MWANZA VIZURI, ."SAHARA" INA REKODI ZAKE NA MATUKIO YAKE.
Unaonekana mwenyeji sana sasa nielekeze wapi nikienda napata kitu ugali dona uliopikwa kwa viwango vinavyotakiwa na samaki ambae hakupita kwenye fridge sehemu ambayo nikitoa elfu kumi yangu natoka nijisemea nimekula. Namaanisha smakaki sio kijisamaki samaki hasa sato
 
Ndio mkuu ila naona wana mpango wa kuitoa nyamangana waunde wilaya ya kisesa kama ckosei
Nataka kuweka makaziwanza ila nataka kiwanja kikubwa kidogo eneo zuri haasa baada ya miaka 5 ijayo. Wapi panafaa kati ya Ilalila, Kisesa na Kishiri.
 
LEMME HELP YO ....

1. ARMY J nite club
2.JEMBE NI JEMBE
3. MALAIKA BEACH
4. BLUE SKY LOuNGE
5.SAMANANE .
Hizo zinakutosha , utaenjoi adi uchanga nyikiweh ...

Ovah ....
Msha anza kutaja vi bar..iyo Army J nayo club
 
Nataka kuweka makaziwanza ila nataka kiwanja kikubwa kidogo eneo zuri haasa baada ya miaka 5 ijayo. Wapi panafaa kati ya Ilalila, Kisesa na Kishiri.
Kisesa ni mjii unaokuwa kwa kasi ...nafikur ni sehem nzur ya kuchukua eneo..ila kishir kuna tetesi kuwa itakuwa makao makuu ya wilaya inayoanzishwa kwa hyo ni hot cake pia...sema changamoto ya kishiri ina milima sanaa na uhaba wa maji baadh ya maeneo
 
Na Kisesa naona pameanza kuchangamka sana siku hizi mkuu we unaonaje..?! Igoma na Buhongwa unaweza kusema ni miji midogo ndani ya mji kwa uchangamfu wake.
Buhongwa ina watu wengi kuliko downtown pia pamechangamka sana, pia inakadiriwa buhongwa pekee inawatu 100000 na igoma ina watu 60000.
 
1.Idara ya maji-Hesawa-Capripoint.

2.Jiwe kuu-Kitangiri-Bwiru (Hapo Jiwe kuu utaziona alama zimetokeza juu ja mawe za mikono,vidole vya mfalme wa kale wa Kisukuma "Ng'wana Malundi".

3.Darajani-Furahisha-Kirumba.

4.Darajani-Mabatini.

5.Bismarck Rock-Kamanga-Nyamagana "utaona nondo zimechomekwa na kuzama ndani ya jiwe".

6.Nyumba juu ya nyumba, Jiwe mbele ya nyumba, nyuma ya nyumba na juu ya nyumba. -SAHARA-Pamba-Mwanza.

7.Bugando Jeshini, Bugando Hospital, Bugando Mission, Bugando Nkali na Bugando Kati [Kata ya Igogo].

8.Isamilo lodge, Mjimwema, Nyashana, na Mbugani.

9.Mwaloni-Magomeni, Kigoto, Ibanda, Bujumbura-Kirumba.

NOTE: KAMA HAUTAFIKA "SAHARA" HAUTAKUWA UMEIFIKIA MWANZA VIZURI, ."SAHARA" INA REKODI ZAKE NA MATUKIO YAKE.
Hakuna jipya zaidi ya matukio ya ujambazi.....nikiambiwa nitaje miji iliyoko kanda ya ziwa inayoongoza kwa matukio ya unyang'anyi wa kutumia siraha naanza na mwanza..Geita..hiyo miji miwili wala bata wengi wamejificha kwenye kichaka cha kwamba wanajishughulisha na ishu za madini pamoja na uvuvi.....ukweli ni kuwa wengi ni majambazi.....kituko ni kwamba gereza la butimba huwa halikauki...kila siku linasomba nyomi ya raia...ukiwa mle ndani ni kama sokoni
 
Habarini za muda huu nduguzangu wa Jamii Forum.
Niende moja kwa moja kwenye Mada kuelezea vile nimepata kujionea utofauti wa jiji la Mwanza tangu siku yangu ya kwanza tu kufika.
Safari ilikuwa ngumu mpaka nikajiuliza nina mkosi maana gari liliharibika mara tatu, hatimaye majira ya saa nane za usiku ndio nikafika Mwanza, Jiji nililokuwa nalisikia tu na kupata sifa nyingi ila sijawahi kufika.
Siku yangu ya kwanza niliona mambo mengi tafauti na Dar es salaam au jiji la Daudi. Watu wa Mwanza ni wakarimu mno ani ukimuuliza anaweza kukujibu vizuri, Makonda na Madereva daladala wako vizuri nilipanda daladala nakaribia kufika kituoni nikasimama akaniambia kaa mpaka gari lisimame ani nilishazoea Dar gari hata halijasimama vizuri utasikia konda anamwambia dereva twende.
Mwanza kuna mandhari nzuri na hali ya hewa safi. Navutiwa zaidi na mawe hasa yaliyo karibu na nyumba, unakuta nyumba imejengwa nyuma kuna bonge la jiwe..

Enewei nina wiki tu jijini Mwanza anayejua maeneo mazuri ya kuvutia maana napenda sana kutalii. Ahsanteni

KichWa bOX

Binafsi,,,Mwanza is namba 1 kwa ubora in tanzania and east afrika

Kibiashara,,,
Kuishi,,,
Kutembea,,,
 
Unaonekana mwenyeji sana sasa nielekeze wapi nikienda napata kitu ugali dona uliopikwa kwa viwango vinavyotakiwa na samaki ambae hakupita kwenye fridge sehemu ambayo nikitoa elfu kumi yangu natoka nijisemea nimekula. Namaanisha smakaki sio kijisamaki samaki hasa sato
Mkuu, Nahisi hata wewe si mgeni pale JIJI LA MIAMBA.

Ni Elfu kumi na tatu yaani 13,000=/TSH unampata SATO MKUBWA safi kabisa na UGALI wake safi wa DONA.

Na pale si pengine bali ni ROYAL PUB.
 
Back
Top Bottom