Nimevutiwa mno na Jiji la Mwanza

Hot27

JF-Expert Member
Oct 31, 2020
308
422
Habarini za muda huu nduguzangu wa Jamii Forum.
Niende moja kwa moja kwenye Mada kuelezea vile nimepata kujionea utofauti wa jiji la Mwanza tangu siku yangu ya kwanza tu kufika.
Safari ilikuwa ngumu mpaka nikajiuliza nina mkosi maana gari liliharibika mara tatu, hatimaye majira ya saa nane za usiku ndio nikafika Mwanza, Jiji nililokuwa nalisikia tu na kupata sifa nyingi ila sijawahi kufika.
Siku yangu ya kwanza niliona mambo mengi tafauti na Dar es salaam au jiji la Daudi. Watu wa Mwanza ni wakarimu mno ani ukimuuliza anaweza kukujibu vizuri, Makonda na Madereva daladala wako vizuri nilipanda daladala nakaribia kufika kituoni nikasimama akaniambia kaa mpaka gari lisimame ani nilishazoea Dar gari hata halijasimama vizuri utasikia konda anamwambia dereva twende.
Mwanza kuna mandhari nzuri na hali ya hewa safi. Navutiwa zaidi na mawe hasa yaliyo karibu na nyumba, unakuta nyumba imejengwa nyuma kuna bonge la jiwe..

Enewei nina wiki tu jijini Mwanza anayejua maeneo mazuri ya kuvutia maana napenda sana kutalii. Ahsanteni

KichWa bOX
 
Chukua bodaboda hapo ulipo halafu ulizia sehemu za starehe unataka ukaenjoy macho akupeleke boda wanazifahamu halafu nauli buku Kama ni mbali basi buku 2, ukimaliza chukua boda nyingine akubadilishie mandhari
Eti enh! Nilikuwa nasikiaga hifadhi ya Saanane! Nadhani ni muhimu kufika huko pia..

KichWa bOX
 
Habarini za muda huu nduguzangu wa Jamii Forum.
Niende moja kwa moja kwenye Mada kuelezea vile nimepata kujionea utofauti wa jiji la Mwanza tangu siku yangu ya kwanza tu kufika.
Safari ilikuwa ngumu mpaka nikajiuliza nina mkosi maana gari liliharibika mara tatu, hatimaye majira ya saa nane za usiku ndio nikafika Mwanza, Jiji nililokuwa nalisikia tu na kupata sifa nyingi ila sijawahi kufika.
Siku yangu ya kwanza niliona mambo mengi tafauti na Dar es salaam au jiji la Daudi. Watu wa Mwanza ni wakarimu mno ani ukimuuliza anaweza kukujibu vizuri, Makonda na Madereva daladala wako vizuri nilipanda daladala nakaribia kufika kituoni nikasimama akaniambia kaa mpaka gari lisimame ani nilishazoea Dar gari hata halijasimama vizuri utasikia konda anamwambia dereva twende.
Mwanza kuna mandhari nzuri na hali ya hewa safi. Navutiwa zaidi na mawe hasa yaliyo karibu na nyumba, unakuta nyumba imejengwa nyuma kuna bonge la jiwe..

Enewei nina wiki tu jijini Mwanza anayejua maeneo mazuri ya kuvutia maana napenda sana kutalii. Ahsanteni

KichWa bOX
Maeneo mazuri ya "kuvutia"
Nimekuelewa vema hapo Rasta
 
Aisee una Bahati mkuu Villa pub imefunguliwa kilumba pale unapata burudani ya live band na samaki sato mkubwa ana kichwa Cha mtoto.

Ukimaliza request bolt nenda club elevate Malaika pale hutojuta kula hela yako .

Ukiagiza Hennessy inasindikwa na wadada watano wakalii ukimaliza unaondoka nao utajua utawapeleka wapi.

Cask iliungua ila bado Ni ya Moto pale Kuna kila binadam Ni mfuko wako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom