Nimevamiwa na nyoka aisee ni hatari

Nimevamiwa na nyoka aisee ni hatari

Jamani wanajamvi wazima? Hapa kwangu ninaishi na baadhi ya mifugo,nimewajengea mabanda maalumu uani...

Sasa jana jioni tu kuku wangu alishambuliwa mno,na ndiyo nilikuta nyoka ameshaingia bandani.

Yaani alikuwa ameshamuua jogoo sasa anamnyofoa nyama anakula. Nilikuta kashamla robo tayari na anaendelea kumega mapande ya minofu.

Ama kwa hakika nyoka ni hatari,tulimuua kwa msaada wa kerosene pia.
Mkoani nyoka wengi sana...
Mabaki ya kuku tukayafukia.

Kuweni makini jamani. Na nasikia nyoka aina ya kobra huwa wanatembea mume na mke, mkewe tulishamuua na huyu ni mumewe.

Huwa anaweza kuingia hata kupitia upenyo mdogo wageti.kuweni makini mno

NB:nyoka huyu alikua anatafuna kabisa minofu aliyonyofoa kwenye mwili wa kuku. Hii inaonesha ata mtoto mdogo anaweza kumla. Tuwe makini
Nyoka ananyofoa minofu!?

Nyoka Gani huyo aisee!?

Ebu weka picha ya huyo nyoka
 
Nyoka anatisha bwana

Miaka mingi kidogo nilikaa kwenye kibaraza mbele ya nyumba umeme umekatika, Sina hili wala lile

Ghafla nikahisi kitu chenye joto kinateleza kwenye nyayo zote za miguu, sielewi ilikuwaje ila nilisogeza miguu taratibu sana nikawasha tochi ya simu...Kuangalia nyoka ndio alikuwa anajiweka vizuri pale aiseeee niliruka hatari ile speed sijawahi kuwa nayo tukamuua

Siku tatu mbele nipo bafuni naoga nyoka kama yule yule ukubwa ule ule rangi ile ile namuona pembeni nashukuru nilikuwa sijavua nguo sijui ingekuwajenikatoka mbiiioooo na sikuoga Tena Kwa muda ule

Aiseee mama akaanza kulia wachawi wanamfuata mwanaeeti nyoka yule yule kafufuka..

Siku kadhaa mbele tukaua mwingine ila huyo alionwa na mwingine sio Mimi.

Tukahisi wamezaliwa pale ila hatukuwahi kumuona mama Yao wala baba yao
Alikuwa amemfata nyoka mwenzie anayening'nia Kati kati ya miguu yako
 
Kuna eneo linaitwa Nala, Dodoma. Nilimkanyaga huyu nyoka Dec 31 usiku. Nikagundua kumbe binaadamu tunaweza kupaa basi tu uzembe wetu
Cobra
View attachment 2603894
Angekugusa usingekuwepo leo hii
 
Acha tu yaani niliruka juu height kubwa sana nadhani hata masai niliwashinda.
Lakini hili tukio lilinifanya nigundue Mungu fundi sana kwenye upande wa response towards stimulus/Vichochezi.

Yaani ilinichukua muda wa 0.01second kuchukua hatua ya kuruka juu baada ya kumkanyaga. Nilivyomkanyaga mwili ukasisimka nikajiuliza nini hiki nimekanyaga kilaini hivi nikaruka. Yaani ndani ya muda mfupi sana. Nikawa nimefanya practical ya Topic ya Coordination
Huwa nawashangaa sana wanaosema Mungu hayupo
 
Nilikanyaga nyoka ,bahati nzuri nilikanyaga upande wa kichwani,niligundua alipoanza kujinyonganyonga mwili na kujiviringisha mguuni,akili ya haraka ikanijia kwamba kwakuwa mwili umeshajifunga mguuni nikiinua kuachia kichwa ataning'ata,nikakandamiza kiatu na kubana kichwa ardhini hadi alipojinyoosha kuashiria amekufa ndio nikamuachia,nikamfungua mguuni kwa mkono nikamtupia mbali.

Hii ki Rambo Rambo au Ki Anodi Anodi yaani kisterling sana.
 
Jamani wanajamvi wazima? Hapa kwangu ninaishi na baadhi ya mifugo,nimewajengea mabanda maalumu uani...

Sasa jana jioni tu kuku wangu alishambuliwa mno,na ndiyo nilikuta nyoka ameshaingia bandani.

Yaani alikuwa ameshamuua jogoo sasa anamnyofoa nyama anakula. Nilikuta kashamla robo tayari na anaendelea kumega mapande ya minofu.

Ama kwa hakika nyoka ni hatari,tulimuua kwa msaada wa kerosene pia.
Mkoani nyoka wengi sana...
Mabaki ya kuku tukayafukia.

Kuweni makini jamani. Na nasikia nyoka aina ya kobra huwa wanatembea mume na mke, mkewe tulishamuua na huyu ni mumewe.

Huwa anaweza kuingia hata kupitia upenyo mdogo wageti.kuweni makini mno

NB:nyoka huyu alikua anatafuna kabisa minofu aliyonyofoa kwenye mwili wa kuku. Hii inaonesha ata mtoto mdogo anaweza kumla. Tuwe makini
Chukua oil chafu na uchanganye mafuta ya taa umwagie kwenye vizingiti vya kuingia ndani na kuzunguka mabada ya wanyama.
Next utuwekee na picha
 
Jiandae tu bro mume wake akijua umemuua mke wake utakutana na balaa
 
Nilikanyaga nyoka ,bahati nzuri nilikanyaga upande wa kichwani,niligundua alipoanza kujinyonganyonga mwili na kujiviringisha mguuni,akili ya haraka ikanijia kwamba kwakuwa mwili umeshajifunga mguuni nikiinua kuachia kichwa ataning'ata,nikakandamiza kiatu na kubana kichwa ardhini hadi alipojinyoosha kuashiria amekufa ndio nikamuachia,nikamfungua mguuni kwa mkono nikamtupia mbali.
Noma sana...una akili nzuri sana
 
Huyo nyoka ni wa kidjitali ..ananyofoa minofu na kutafuna na kujipakulia minyamaaa
 
Chief bongo hakuna cobra pia nyoka Hali Kwa kunyofoa yeye ni kumeza tu usingekuta hata manyoya sasa hilo joka lako limemnyonyoa jogoo halifa linanyofoa mapande ya minofu ,niamin mimi mkuu utakua uimkuta mtoto wa fisi bandani kwako
 
Back
Top Bottom