Mimi miaka mitatu nyuma nilipona pona kutapeliwa tena na mwanadada akijifanya yeye ni mtoto pekee wa mwenye nyumba - ambaye ndiye mama yake mzazi akidai kwamba anaishi nje ya nchi dubai kwa hiyo tumlipe pesa yeye.
Nyumba ilikuwa nzuri sana na bei wakati ule ilikuwa 400,000 kwa mwezi so nilitakiwa nilipe Tshs. 4.8m pesa ya mwaka. Roho wa Mungu alinitokea na kumwambia yule dada anipe bank account ili nikamwekee pesa!! hapo utata ukaanza kwamba yeye hana account ya benki, nikamwambia basi nimlipe kwa Mpesa pia akadai account yake ina matatizo.
Baada ya kutoelewana kwamba mimi sitoi pesa CASH, wakashauriana na yule dalali kwamba kama sina nia na nyumba niiachie wengine walipie - kwani kulikuwa na wengine nje wakiwa na gari wakisubiri kuiona (nafikiri matapeli wenzao).
Nilivyotoka tu nje na rafiki yangu tukiwa tayari kuondoka, pembeni kidogo akatuita mzee mmoja akatuambia hiyo nyumba ni mali ya jamaa akatutajia jina na hapangishi - wale ni matapeli.
Tulitoka moja kwa moja hadi police, tuliporudi pale hakukukuta mtu na nyumba ilikuwa imefungwa. hapo ndiyo ikawa pona yangu -- I never pay more than 1m Tshs in cash.