Hekaya za Abunuasi
Senior Member
- Jan 6, 2014
- 166
- 38
Milion sita? Ina maana laki 5 kwa mwezi? Na ulikopa ili upange kifamilia? Au kibiashara? Sinza kwa Remmy? Kweli tunatofautiana sana!
HEKAYA ZA ABUNUASI?? Mimi naomba kutoa pole huku nikipita kimyakimya, maana nimeponea chupu chupu kuporwa simu na kukabwa na wahuni mchana kweupeee maeneo ya mtoni mtongani. halafu begi lilisheheni kila kitu muhimu kwangu. yaani nikikukuta unamtetea mwizi au tapeli nakuua hapo hapo!
Mkuu pole sana, naungana na waliosema utafute vijana wa kazi. Niliwahi kupanga nyumba baada ya kulipa kodi nikaombwa nisubiri ujenzi (wiring) ukamilike, kumbe kijana alokuwa analinda hiyo nyumba katengeneza copy ya funguo. Siku moja nimesafiri, kukacha asubuhi ndani kutupu, wamekomba kila kitu. Kuna jamaa 3 X-vibaka, kazi yao ni kutrace wahalifu na mali zilizoibiwa, gharama yao ni 1/4 ya mali itakayopatikana. Baada ya siku 4, Saa 8 usiku walimleta dogo akiwa hafai, akaeleza wapi vitu vilipelekwa. Tulikuta almost nusu vimeshapigwa bei.
Aliyewahi kuibiwa anajua machungu haya, narudia POLE SANA mkuu HEKAYA.
Sijijui mkuu, halafu mimi huwa sina muda wa kujiangalia kwenye kioo
Pole sana mkuu, ilikuwaje ukalipa pesa bila kukabidhiwa funguo. Nafikiri huu ni wakati wa kuwakataa Mdalali wasiotambulika Kisheria.
Hiyo ID yako inanifanya nishindwe kuchangia hii mada maana kutoa 6ml kwa mtu mkononi tu tena ni nje ya eneo husika napata shida kuelewa.
Nimeandika uzi huu ili watu wajifunze na waelewe kuwa kuna utapeli wa namna hiyo. Na kwa kuwa humu jamvini kuna watu tofauti naweza kupata mawazo nini cha kufanya
Unajua mkuu obwato umefikiria sana kwani hata mimi pia hiyo ID inanifanya nifikirie pengine hata hiki anachotueleza ni kama hadithi za Abunuwasi tu na si kweli. Kwani ktk hali ya kawaida kuikabidhi mil. 6 kirahisirahisi tu bila documents na mashahidi wa kueleweka haiingii akilini
Umeambiwa nani mwenye nyumba halisi?
Bwana hekaya nakushauri kakomae na police watakusaidia muende ktk ile nyumba yule jamaa mpaka mumtie mikononi. Kinyume na hivyo hutopata haki yako