Nimetapeliwa Sinza

Nimetapeliwa Sinza

Ukishajua umetapeliwa unatakiwa utulie ujifunze kutokana na kosa wala usijisumbue kuwatafuta matapeli ksbu utaishia kutumia hela nyingi zaidi kuhonga polisi na mahakamani alafu utashindwa kwa aibu. Kabla ujalipa kiasi kikubwa kama hicho ulitakiwa kuwa umefanya homework yako, ina maana ungekua unanunua iyo nyumba ungebeba bulungutu la hela upeleke Makongo!
 
Haki ya nani poleni sana.Mie nina dada yangu ana bonge la jumba Tegeta anahangaika kutafuta mtu wa kuishi humo kwa miaka mitatu maana yeye anaenda kusoma.heeee wengine mnatapeliwa jamani kweli watu tunatofautiana.
Asking price yake ni kiasi gani unajua watu wanatafuta unafuu wa gharama na nyumba ya kawaida ili waishi, sasa ikiwa hilo Jumba ni kubwa (hata usafi pia inasumbua na ni gharama) alafu bei yake ni kubwa sana na location yake sio accessible huenda asipate watu au kama shida ni kuchungiwa nyumba wakati hayupo bora atafute ndugu zake au aweke mlinzi wa kumchungia
 
Mimi sina hamu na matapeli wa sinza nilitapeliwa laki sita kwenda kituo cha polisi kumbe yule tapeli anajulikana sana pale kituoni ila kumkamta ndio inakuwa shida. Hawa jamaa wako makini sana kukanatika sio rahisi. Mimi nilimwachia Mungu ingawa nilikuwa nampangishia demu
 
Nakushauri ukipata tena pesa kana hizo sogea kando ya mji upate kiwanja. Milioni sita unamaliza chumba na kuhamia. Ni pesa ndefu. Achana na kupanga kama kampuni za simu ambazo zinajua tanzania zinapita tu.vyou arwle here to stay for the rest of your life.
Mkuu kweli kwa Dar unapata kiwanja na kujenga kwa kiasi hicho (sijui sababu sikai dar ila navyojua Dar property ipo overpriced)

Pia mkuu mtu anapokaa inategemea na shughuli zake huenda kila siku anahitajika mjini, hivyo akikaa mbali sana huenda gharama za usafiri zikawa ni zaidi kuliko ambavyo angepanga pengine au huenda akashindwa kufanya kazi za watu kwa kutoweza kufika anapotakiwa
 
Haki ya nani poleni sana.Mie nina dada yangu ana bonge la jumba Tegeta anahangaika kutafuta mtu wa kuishi humo kwa miaka mitatu maana yeye anaenda kusoma.heeee wengine mnatapeliwa jamani kweli watu tunatofautiana.

Vipi ungependa akaishi kwa dada yako au....
 
Ndugu zangu tujifunze kwa hili lililompata ndugu yetu. Kama unatafta nyumba ya kupanga au kiwanja kuwa makini sana na hawa madalali kwanza. Pili ukioneshwa mwenye nyumba au kiwanja ebu kuwa mdadisi zaidi ya kupewa funguo. Mimi nilipata nyumba yakupanga na nikamuomba mwenye nyumba anipe at least document inayothibitisha kuwa ile ni nyumba yake. Alinipatia na nikaiona. Pia wakati mna sign lease agreement awepo mtu wa serikali ya mtaa mana huyo atakuwa anawafahamu wakazi wa eneo hilo. Wakati mwingine huwa wanataka kupewa kitu kidogo, ni bora zaidi kumpa hata 50,000 huyo mjumbe kuliko kutapeliwa pesa nyingi kama huyu ndugu yetu.

Binaadamu wa sasa hawaaminiki kabisa, TRUST NOTHING SUSPECT EVERYTHING
 
Pole sana ndugu yetu, na hakuna mtu wa kukulaumu kwani shida ya kupata nyumba hapa dar inaeleweka, ila sasa jaribu kuwa karibu na wenyeji wa sehemu unayokusudia kupanga.
 
mi mweyewe yalitaka kunikuta ila mr mcl
haleyalimcheza na mwenye nyumba anaonekana ni huyo huyo maana na yy alikiwa anaishi kwenye nyumba ya ghorofa makongo juu anaapparyment nyingi tu makongo huko huko niliambiwa anafanya kazi ardhi ni.mchaga
 
pole sana mimi yalinikuta mwaka 2007 sinza delux sitawasahau madalali wa sinza kijiweni
 
Nakushauri ukipata tena pesa kana hizo sogea kando ya mji upate kiwanja. Milioni sita unamaliza chumba na kuhamia. Ni pesa ndefu. Achana na kupanga kama kampuni za simu ambazo zinajua tanzania zinapita tu.vyou arwle here to stay for the rest of your life.
Kila mtu ana chaguo la 'taste' ya maisha anayotaka kuishi. Huko kando ya mji taste yake ni tofauti sana na Sinza.
 
kwani wakati unatoa pesa,hakuna documents zozote mlizoandikishiana?
 
Siku hizi nikinunua shamba or anything nampiga picha dalali, kwenye shamba na mwenyekiti WA mtaa. Na nawataarifu kabisaa kuwa if the deal is a bluff watajikuta magazetini na sura zao wanatabasamu.

pole.
Kuna mdau alinunua nyumba kila kitu fine na alifata procedures zote, matokeo yate wamekuja wanaukoo / ndugu na kudai hawakushilikishwa kwenye hayo mauzo. Huu ni mwaka wa tano Kesi zinapigwa danadana..., ingawa huenda mwisho wa siku atashinda Kesi ila usumbufu na muda aliopoteza anajuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom