Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu dada

Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu dada

Kwa kuwa unaona anakusumbuwa na wewe unasema hujaliwa na boss, sasa kaliwe na boss, akija tena kukuuliza mwambie kuwa wewe umeshaliwa na boss kwa hiyo asikuulize-ulize sana.
Bimkubwa, hapo nilipo Bold ni wewe ndio umeandika hayo au kuna mtu kakuingilia? Bado siamini amini hivi! Unamshauri Fixed point aliwe na boss? Si wewe ndio umetoa hadi mstari wa kitabu kwamba sir god hataki hayo ya uzuinzi!?
 
Hapa nahitaji majibu yale makali kabisa ya kumjibu ili either (i) asije tena kunilalamikia upuuzi anaouendekeza mwenyewe, or (ii) aone clearly kuwa yeye ndo mchochezi mkuu wa hayo mambo kwa hiyo asiendelee kumlaumu baba wa watu.
una uhakika huyo dada si member wa jf??..angalia usije poteza kazi...
 
una uhakika huyo dada si member wa jf??..angalia usije poteza kazi...
ha haa, nina uhakika siyo member.... usiniulize uhakika huo nimeutoa wapi, but 100% siyo member, wewe mwaga tu sumu hapa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
he he heeee, nitaanzia wapi kudanganya namtaka bosi?
hainiingii akilini aisee

Hahahahahaaaa!
If nimekusouma vizuri, umesema unahitaji majibu MAKALI ya kumpa! Aren't you???
...
Wewe hapo hautotoa penzi kwa boss, na badala yake utatoa jibu kali litakalomfanya asikuletee tena hizo habari!!!!!!
What do you think?
 
Ni mara nyingi amekuwa akija kwangu kulalamika jinsi ambavyo baba mmoja anamsumbua sana kumtaka kimapenzi. Bidada hajaolewa lakini ana mchumba. Ila ni mdada mkubwa tu (over 35 years).
Ushauri ambao mara kwa mara nimekuwa nampa ni kujitahidi kuwa mbali na huyo baba. Akutane naye tu kama kuna ulazima wa kufanya hivyo (wanafanya wote kazi) zaidi ya hapo awe mbali naye.
Jana yule dada kanipigia simu kuniuliza kama nitahudhuria workshop ambayo huyo baba kaiandaa (baba ni boss mkuu hapa tulipo, na mimi nafanya kazi nyingi sana na huyo boss). hiyo workshop ni ya nje ya ofisi, kazi yake binafsi, ila alituomba kama tunataka kushiriki kwa njia yoyote ile na ikiwezekana tumsaidie katika maandalizi.
Nikamwambia yule dada kuwa sitahidhuria, akanishangaa kwa nini, nikamwambia kwanza nina kazi nyingi sana lakini pia haikuwa lazima, na kwa nilivyobanwa nisingeweza kujitolea. huyo dada kwanza hafanyi kazi chini ya huyo baba, ingawa tupo idara moja, yeye ana bosi wake. lakini alipoona ile email aliamua kujitolea kumsaidia. kwa vile hafanyi kazi tunazozifanya, kwa hiyo kajitolea kumsaidia logistics wakati wa workshop.......
Hebu naomba mniambie huyu mdada anataka nini? nina uhakika wakitoka huko workshop (maana wanalala huko huko hotel) atakuja kunilalamikia jinsi alivyosumbuliwa.
Hapa nahitaji majibu yale makali kabisa ya kumjibu ili either (i) asije tena kunilalamikia upuuzi anaouendekeza mwenyewe, or (ii) aone clearly kuwa yeye ndo mchochezi mkuu wa hayo mambo kwa hiyo asiendelee kumlaumu baba wa watu.

Mwambie wamalizane kikubwa!
 
......Hebu naomba mniambie huyu mdada anataka nini? nina uhakika wakitoka huko workshop (maana wanalala huko huko hotel) atakuja kunilalamikia jinsi alivyosumbuliwa.
Hapa nahitaji majibu yale makali kabisa ya kumjibu ili either (i) asije tena kunilalamikia upuuzi anaouendekeza mwenyewe, or (ii) aone clearly kuwa yeye ndo mchochezi mkuu wa hayo mambo kwa hiyo asiendelee kumlaumu baba wa watu.

...... AshaDii keshachangia uzi huu?...
Huyo mdada ni mfano halisi wa wale wanao "mark" territory!....aka .....kuudhibiti Uzio!
 
Last edited by a moderator:
...... AshaDii keshachangia uzi huu?...
Huyo mdada ni mfano halisi wa wale wanao "mark" territory!....aka .....kuudhibiti Uzio!
na mimi namsubiri kwa hamu huyo uliyeniitia.....
ngoja atuletee nondo hapa....
kuna majibu pia nayasubiri kutoka kwa Kongosho, King'asti na snowhite......
mdogo wangu cacico sijui yupo!
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaaaa!
If nimekusouma vizuri, umesema unahitaji majibu MAKALI ya kumpa! Aren't you???
...
Wewe hapo hautotoa penzi kwa boss, na badala yake utatoa jibu kali litakalomfanya asikuletee tena hizo habari!!!!!!
What do you think?
ha haaa, asije akaamini halafu akamwambia bosi kumbe ulimtaka na fulani!
si nitafukuzwa kabisa na kazi
 
Mtani Fixed Point naomba tu nisikufundishe namna ya kumjibu huyo mdada maana naweza kuishia kupata BAN tu hapa...na hapa nina mihasira ya timu yetu ya Taifa kufungwa ndio kabisaaaa siwezi andika...
 
Last edited by a moderator:
He he he he, FP, utakua lini? Huyo dada ni wapenzi na bosi, hapo anakuja kumchunguza kuku wake kuona kama anakula na wengine.


Kuna info anaitafuta toka kwako, na hapo hapo ana mark teritory yake kwako, labda huwa anaona mko karibu kikazi basi anakosa raha.

na mimi namsubiri kwa hamu huyo uliyeniitia.....
ngoja atuletee nondo hapa....
kuna majibu pia nayasubiri kutoka kwa Kongosho, King'asti na snowhite......
mdogo wangu cacico sijui yupo!
 
Huyo dada hajitambui, hana msimamo, na namwomnea huruma sana huyo mchumba wake.

Huko kusumbuliwa kwake na huyo bosi ni yeye huyo dada ndo anakusababisha.

Kama kweli angekuwa hataki basi isingekuwa vigumu kwake kuziwekea 'kibosh' hizo advances za jamaa.

Sasa huenda huyo dada ni glutton for attention na hivyo anafurahia kinachoendelea au ni mmoja ya wale ambao hwajui kusema 'hapana'.

Vyovyote vile, huyo mchumba wake kala hasara hapo. Ni bora awekeze kwenye mambo mengine kuliko kuwekeza kwa huyo dada.

Wanawake (hata wanaume) wenye maadili, misimamo, heshima, na ambao hawachiti ni tunu.
 
We mkaushie wmle mzigo kwanza kisha ndo aje na kishombo shombo chake na kuanza kujisemesha semesha kwako. heshima ya mtu kama huyo ni kuliwa kabang kwanza ya nguvu kisha ndo atanyooka.
 
Fixed Point huyo mdada inawezekana humjui vizuri au unamjua lkn kuna mambo mengi yanyomhusu huyajui yote. Hivyo basi wewe akikusimulia anayokumbana nayo nayo toka kwa huyo bwana mkubwa msikilize na kisha muulize yeye anaona nini. Baada ya hapo badili story endeleeni na mambo mengine maisha yasonge. Yawezekana hana nia mbaya anapokusimulia hayo bali inatokana na uwezo wake kichwani wa kuchuja mambo.

Yaelekea ameshampenda boss wake so ukiweza msaidie ili aweze kuyaona madhara ya michanganyo na mwisho wa yote yeye ndiye dereva wa nafsi yake na maisha yake. Mkanye kama ndugu na asipokusikiliza mwache.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom