Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Upo serious kweli, siwahamini sana waganga, sijui utaniaminisha kwa lipi niwaamini.Labda weka namba ya simu ya huyo mtaalamu nimfanyie assement na research ya nguvu.

Sema Sasa, never ever fall on temptation! Unatakiwa ukomae na jambo moja mpaka kieleweke, umejaribu jaribu mno mambo mengi kiasi kwamba hujui nini la kufanya tena. Anzisha tena kamradi kokote then muombe Mungu akufanikishe, achana na mambo ya uganga maana after sometimes unajikuta unarudi pale pale hvo kulazimika kuanza kutoa makafara na mwishowe utajikuta unachanganyikiwa mana huna ulichotarajia. Maombi ni muhim kuliko kwenda kuvuna laana, kwa waganga wanaendaga waliomkatia Mungu tamaa.
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni Kenge Sana,cm yangu nimeweka keyboard automatic neno Amazing kiswaga ni Amaizing najua ni uzee unakusumbua ndio maana swaga za kileo haujui......Peruzi Instagram uone linavyotumika...kenge wahed wewe.
Wewe unamatatizo gani? Mbona matusi gafla kwenye thread yangu hii naomba ushauri na msaada. Sio vizuri
 
. Hilo la pili jombaa si kashasema bihashara ilikufa.....sasa kama bihashara ikifa si unaachana nayo au ulitaka na yeye afe na bihashara yake?

Sorry nimekuelewa namuombea awe na maisha mema na marefu
 
Kuna mashamba ya pamba, pia kuna bibi huku noma kwa matatizo kama yako yule wa gesi aubili sana.
 
Mimi nina qualification ya shahada ya kwanza ya statiscs na economics toka UDOM 2011.

Niliajiriwa na shirika binafsi kubwa kiasi hivi tokea 7/2011. Nimefanya Kazi kama m&e officer 2 years, program coordinator 2.3 years. Nimeudhuria short courses zaidi ya 20 Tanzania hii kuhusu kilimo, m&e, miradi usimamizi, research, ufugaji, utunzaji mazingira, ukimwi, gender,nk. Sasa mradi umekwisha na mkataba umekwisha pia, nipo kitaa sina Kazi kwa sasa.

Mpaka sasa nimeshatuma maombi zaidi ya 250 kwenye kila sector au shirika iwe wametangaza nafasi au hawakutangaza. Ila sijawahi itwa kwenye interview yeyote ile sijui kwa nini?

Nimewahi kuwekeza kwenye kilimo cha viazi soko lilishuka sana msimu huo nilikulahasara, nikanunua ng'ombe wamaziwa nikamfuga wakati anazaa akafa yeye na kindama chake, nikanunua pikipiki mbili nifanye Bodaboda, moja ikaibiwa na nyingine ikapata ajali, nikafanya utafiti na nikafungua duka kubwa la bidhaa za jumla na rejareja katikati ya mji mwanzoni niliuza sana, competitors wenzangu niliowakuta wakaanza lalamika nachukua wateja wao sikujali, nilifanya biashara miezi 5 tu, mwezi wa 6& 7 mauzo yalishuka toka laki tatu hadi tano na nikawa nauza elfu kumi mpaka 50 tu kwa Siku.

Nikaacha biashara niliendesha kwa hasara. Sasa nipo tu sijui nifanye nini?

Nina mke na mtoto 1. Mke wangu ni mtumishi.Hebu nisaidieni nipate Kazi. Miaka 30 very strong kijana.

Nyongeza: Nimewahi jiunga na biashara ya forever living, nilinunua bidhaa zao nimezunguka nazo usiku na mchana hakuna wateja nikaanza tumia mwenyewe na nyingine nikagawa, nikama nilutapeliwa tu.

Nikakutana na mtu akanishawishi nifuge Kwale wanasoko zuri la mayai na vifaranga, nikafuga Kwale wakaanza taga sana tu, nilizunguka kutafuta wateja wa mayai na vifaranga hakuna kitu.

You need deliverance.Muombe Mungu atakusaidia kuvuka.
 
sasa mkuu kutoka mauzo laki tatu kwa siku mpaka elfu kumi bado huoni kama jamaa alikomaa sana?.....na hapo kapunguza maelezo vinginevyo angekutajia alivyoplomoka mauzo.....laki mbili....laki...elfu hamsini.nk.....ingejaza uzi mkuu.

Asante kwa ushauri, mtu anaweza ona kama maigizo lakini ndio halo ilivyo. Ndio naanza amini kwa nini mtu huamua kujinyonga.
 
Sema Sasa, never ever fall on temptation! Unatakiwa ukomae na jambo moja mpaka kieleweke, umejaribu jaribu mno mambo mengi kiasi kwamba hujui nini la kufanya tena. Anzisha tena kamradi kokote then muombe Mungu akufanikishe, achana na mambo ya uganga maana after sometimes unajikuta unarudi pale pale hvo kulazimika kuanza kutoa makafara na mwishowe utajikuta unachanganyikiwa mana huna ulichotarajia. Maombi ni muhim kuliko kwenda kuvuna laana, kwa waganga wanaendaga waliomkatia Mungu tamaa.

Asante Mkuu, nafikiria kuhama mkoa pia
 
Last edited by a moderator:
Da humu hakuna wenye mashirika, makampuni waniajiri. Nipo vizuri kwenye kuandika miradi inayovutia sana, business plan, strategic plan na ni mtaalamu wa data analysis na hata kuandaa research. Shida kwa sasa sina tena mtaji hata kutuma application majanga. Anayetaka kuniokoa ani pm. Kwa waganga wa jadi sitakanyaga kamwe. Sorry for that.
 
sasa mkuu kutoka mauzo laki tatu kwa siku mpaka elfu kumi bado huoni kama jamaa alikomaa sana?.....na hapo kapunguza maelezo vinginevyo angekutajia alivyoplomoka mauzo.....laki mbili....laki...elfu hamsini.nk.....ingejaza uzi mkuu.
Ha ha ha! Inatokea mkuu ... Ndo changamoto za maisha hizo.
 
Chukua " like.
Kuna waganga wako vizuri sana wanaweza kumsaidia, kuna watu watakuwa wameshika nyota yake,

tatizo la hawa wachungaji wetu wa nigeria ukienda kuombewa ndo na nyota yako inapotea,
 
Diamond Platnumz asingekomaa na gemu moja tu ya muziki basi leo angekua amefulia sna.
 
Sema Sasa, never ever fall on temptation! Unatakiwa ukomae na jambo moja mpaka kieleweke, umejaribu jaribu mno mambo mengi kiasi kwamba hujui nini la kufanya tena. Anzisha tena kamradi kokote then muombe Mungu akufanikishe, achana na mambo ya uganga maana after sometimes unajikuta unarudi pale pale hvo kulazimika kuanza kutoa makafara na mwishowe utajikuta unachanganyikiwa mana huna ulichotarajia. Maombi ni muhim kuliko kwenda kuvuna laana, kwa waganga wanaendaga waliomkatia Mungu tamaa.

Au kama vp angeenda kwa gwajima akapigwe na maombi
 
Last edited by a moderator:
Da humu hakuna wenye mashirika, makampuni waniajiri. Nipo vizuri kwenye kuandika miradi inayovutia sana, business plan, strategic plan na ni mtaalamu wa data analysis na hata kuandaa research. Shida kwa sasa sina tena mtaji hata kutuma application majanga. Anayetaka kuniokoa ani pm. Kwa waganga wa jadi sitakanyaga kamwe. Sorry for that.

Kama vp mm nakushauri nenda kwa fundi gwajima ukapigwe maombi mazito ili mambo yakae powa
 
Chukua " like.
Kuna waganga wako vizuri sana wanaweza kumsaidia, kuna watu watakuwa wameshika nyota yake,
mkuu usiende kwa waganga, waganga wanazidiana sana....dawa yao ni mungu pekee omba sana kwa imani, waganga watakuongezea matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom