Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

duh ebhana na wewe umepitia majaribu ya hasara, hila kama mie nimeona kosa pale ulipoacha biashara ya duka instead ulitakiwa uangalie mfumo unaoutumia upya maana kama duka at first lilianza vyema sasa why liliposhuka mauzo na wewe ukakata tamaa badala yakuangalia strategy upya
 
Tafuta pesa kidogo utamfute Mtumishi wa MUNGU utoe sadaka, na akuombee kuvunja roho ya NUKSI
 
Pole sana kijana.Ila kuomba kazi ni kitu kingine kuitwa kwenye usaili "Interview" ni kitu kingine na kupata kazi ni kitu kingine.
Hayumkini umewahi kuitwa kwenye usaili mara kadhaa.Hata kama uneendelea kuomba na kuitwa kwenye usaili bila ya kuji-tathmini na kujua chanzo cha tatizo basi utaendelea kulalamika sana bila ya kupata ufumbuzi wa tatizo.
Naamini na nakupongeza kwa hatua moja uliyochukua ya kuomba msaada.

kwa upande wangu nikiwa kama kijana wa kitanzania ninayejua nini maana ya kuomba kazi mara zote hizo bila mafanikio naahidi nami nitatoa mchango wangu.

ni PM ili niweze kukupatia mafunzo bure ya "Job Interview" ili uweze kujua yafuatayo:
*Jinsi ya kutafuta kazi;
*Jinsi ya kuandika barua za maombi (Application letter&Covering letter;
*Jinsi ya kuandika na kuipangilia CV yako ili unakopeleka iweze kuonekana na kuitwa kwenye usaili;
*Jinsi ya kujiandaa na usaili (JOB INTERVIEW) kabla,wakati wa usaili na baada ya usaili;
*Jinsi ya kujibu maswali ya usaili walao maswali 100 ambayo huulizwa sana katika usaili wa kazi;
*Kujua mabo ya kufanya na ambayo hupaswi kufanya unapoomba kazi na kufanya usaili wa kazi;
*JInsi ya kuuliza maswali unapopewa nafasi ya kuuliza maswali wakati wa usaili wa kazi na
* Jinsi ya kutaja mshahara unapoulizwa wakulipe kiasi gani na mengineo mengi.

Yote haya utayapata bure toka kwangu ila utalazimika kulipia nauli ya kufika tutakapopanga kukutana na walao maji (Tsh 10,000/-nauli na maji) kwa kila appointment zisizopungua tatu kwa mafunzo yote maana hatuwezi kukutana barabarani kisha nikupatie mafunzo hayo.

Naamini kuna mambo mengi ya kuzingatia ili uweze kupata kazi.Hayo hapo juu ni baadhi tu ila yatakusaidia kufikia malengo yako.Nina uzoefu wa miaka 10 na vijana wengi niliowasaidia kama wewe sasa wanakula mshahara makizini waliko.
Kila la Kheri
 
acha kuishi kwa ndoto,chukua akiba yako yote kanywe bia,kesho amka na hamu ya bia tena,kila ukipata hela kidogo peleka bar na utaona mafanikio,naongea kama utani ila kuna siku utanielewa,tatzo lako n mkeo kuwa na ajira,siku akikosa na wote wanakuanglia wewe hutakuja humu kuomba ushauri,
 
acha kuishi kwa ndoto,chukua akiba yako yote kanywe bia,kesho amka na hamu ya bia tena,kila ukipata hela kidogo peleka bar na utaona mafanikio,naongea kama utani ila kuna siku utanielewa,tatzo lako n mkeo kuwa na ajira,siku akikosa na wote wanakuanglia wewe hutakuja humu kuomba ushauri,

maneno makali sana.. ila mwishoni yana ukweli.. watanzania wachache sana waliajiriwa lakini wote wanaishi kwa kujiajiri vitu vidogo vidogo na wengi wao wanatajirika..

sasa kukosa kazi sidhani kama ni jambo la kukufuru... je ungezaliwa kilema?
 
Nakushauri OKOKA, Yaani; mpe Yesu maisha. Anakuhitaji shambani mwake haraka sana
 
Majanga yangu hayatofautiani Sana na yako, lakini Mungu yupo, hapa nilipo nahisi ukichaa unanianza taratibu hata sijui nifanyeje wandugu.usiombe yakukute
 
Dunia na mapito yake hayo. Never give up Bro. Still there is hope.
 
Mkuu embu fuata ushauri wa jamaa mda mwingine wanakuwa wamechukua nyota yako ndo mana chance unapata ila zinabuma so tafuta mganga mana unaweza kuomba sana ukaishia kumlalamikia mungu amekutupa kumbe kuna mtu wako wa karibu anatumia nyota yako ila pole tusikate tamaa ipo siku tutafanikiwa

ndugu mm naona hao wanganga watamaliza hela yako tu kikubwa ni kuoka na kumfuata Yesu yenye ndiye mganga mkuu hata hiyo nyota yako itarudi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom