Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Sema Sasa

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
651
Reaction score
899
Mimi nina qualification ya shahada ya kwanza ya statiscs na economics toka UDOM 2011.

Niliajiriwa na shirika binafsi kubwa kiasi hivi tokea 7/2011. Nimefanya Kazi kama m&e officer 2 years, program coordinator 2.3 years. Nimeudhuria short courses zaidi ya 20 Tanzania hii kuhusu kilimo, m&e, miradi usimamizi, research, ufugaji, utunzaji mazingira, ukimwi, gender,nk. Sasa mradi umekwisha na mkataba umekwisha pia, nipo kitaa sina Kazi kwa sasa.

Mpaka sasa nimeshatuma maombi zaidi ya 250 kwenye kila sector au shirika iwe wametangaza nafasi au hawakutangaza. Ila sijawahi itwa kwenye interview yeyote ile sijui kwa nini?

Nimewahi kuwekeza kwenye kilimo cha viazi soko lilishuka sana msimu huo nilikulahasara, nikanunua ng'ombe wamaziwa nikamfuga wakati anazaa akafa yeye na kindama chake, nikanunua pikipiki mbili nifanye Bodaboda, moja ikaibiwa na nyingine ikapata ajali, nikafanya utafiti na nikafungua duka kubwa la bidhaa za jumla na rejareja katikati ya mji mwanzoni niliuza sana, competitors wenzangu niliowakuta wakaanza lalamika nachukua wateja wao sikujali, nilifanya biashara miezi 5 tu, mwezi wa 6& 7 mauzo yalishuka toka laki tatu hadi tano na nikawa nauza elfu kumi mpaka 50 tu kwa Siku.

Nikaacha biashara niliendesha kwa hasara. Sasa nipo tu sijui nifanye nini?

Nina mke na mtoto 1. Mke wangu ni mtumishi.Hebu nisaidieni nipate Kazi. Miaka 30 very strong kijana.

Nyongeza: Nimewahi jiunga na biashara ya forever living, nilinunua bidhaa zao nimezunguka nazo usiku na mchana hakuna wateja nikaanza tumia mwenyewe na nyingine nikagawa, nikama nilutapeliwa tu.

Nikakutana na mtu akanishawishi nifuge Kwale wanasoko zuri la mayai na vifaranga, nikafuga Kwale wakaanza taga sana tu, nilizunguka kutafuta wateja wa mayai na vifaranga hakuna kitu.
 
Jitahidi na maombi pia...sio hali ya kawaida kwa upande wangu...pole Mungu atakusaidia, usikate tamaa..

Ni mkatoliki haswa, naimba kwaya kanisani. Napenda sana kusali na kuomba. Ila kwa sasa najihisi imani anaanza kupotea taaratibu.
 
Mkuu nakushauri tembea kwa Waganga i don't believe on Players kuna waganga nguli watakusaidia nini maombi bhana workup guys!
 
Kuimba kwaya ni tofauti na kakaa ktk maombi ukiwa umeokoka nikimaanisha kumkiri Yesu kwanza...na kuomba kwa kuamini

Mkuu nakushauri tembea kwa Waganga i don't
believe on Players kuna waganga nguli
watakusaidia nini maombi bhana workup guys!
 
Jitahidi na maombi pia...sio hali ya kawaida kwa upande wangu...pole Mungu atakusaidia, usikate tamaa..

Mkuu nakushauri tembea kwa Waganga i don't
believe on Players kuna waganga nguli
watakusaidia nini maombi bhana workup guys!
 
Kwani ww ni chama gani?Na ulichagua nani? Masikini Watanzania mmelichagua tena!
 
Mkuu nakushauri tembea kwa Waganga i don't believe on Players kuna waganga nguli watakusaidia nini maombi bhana workup guys!

Mh waganga utamjuaje mganga wa kweli na tapeli?!!
 
Kwani ww ni chama gani?Na ulichagua nani? Masikini Watanzania mmelichagua tena!

Kwa sasa sina chama, kwanza maisha yamenikata sana, nawaza cha kufanya sijui. Tuweke chama pembeni nisaidie tu.
 
Mkuu nakushauri tembea kwa Waganga i don't
believe on Players kuna waganga nguli
watakusaidia nini maombi bhana workup guys!

Mkuu embu fuata ushauri wa jamaa mda mwingine wanakuwa wamechukua nyota yako ndo mana chance unapata ila zinabuma so tafuta mganga mana unaweza kuomba sana ukaishia kumlalamikia mungu amekutupa kumbe kuna mtu wako wa karibu anatumia nyota yako ila pole tusikate tamaa ipo siku tutafanikiwa
 
Mbona simple mganga wangu una safiri mpaka huko aliko anakupa dawa ukishafanikiwa ndo unaenda kutoa asante
Upo serious kweli, siwahamini sana waganga, sijui utaniaminisha kwa lipi niwaamini.Labda weka namba ya simu ya huyo mtaalamu nimfanyie assement na research ya nguvu.
 
Upo serious kweli, siwahamini sana waganga, sijui utaniaminisha kwa lipi niwaamini.Labda weka namba ya simu ya huyo mtaalamu nimfanyie assement na research ya nguvu.

Duuhh,, assessment gani tena mkuu
 
Mkuu embu fuata ushauri wa jamaa mda mwingine wanakuwa wamechukua nyota yako ndo mana chance unapata ila zinabuma so tafuta mganga mana unaweza kuomba sana ukaishia kumlalamikia mungu amekutupa kumbe kuna mtu wako wa karibu anatumia nyota yako ila pole tusikate tamaa ipo siku tutafanikiwa

Chukua " like.
Kuna waganga wako vizuri sana wanaweza kumsaidia, kuna watu watakuwa wameshika nyota yake,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom