Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Nimeshaomba kazi mara 250, sijabahatika!

Nakushauri uachane na mambo ya ajra kabsa. Tafuta mkopo ufanye biashara yako. Ajira haikutaki
 
better you fall in the good hard hands of God than in the soft hands of the devil.......mwamini Mungu utashinda. Mungu na shetani wote wanakutamani japo mmoja wao ashaanza kukuonesha uzuri wake kwa wazi na mmoja amekuficha uzuri wake japo yupo karibu tu anasubiri maamuzi yako.
Ni mapito ndugu mgeukie Mungu kwa moyo wa toba na kuhitaji sana msaada wake. Mungu akutokezee msaada toka patakatifu pake na aitegemeze miguu na magoti yako yasilegee.
Kumbukumbu la Torati 30:11-16

Asante
 
mdogo wangu naye alisoma kozi kama yako tena huko Udom na mlimaliza pamoja amekaa nyumbani mpaka mitatu mpaka alipopata nafasi Jkt naakapata uhamiaji na Jeshi though hakupendelea jeshi akaenda migration kozi yeny ni nzuri sema inachangamoto sana kwenye ajira
 
Katika MIAKA niliyobahatika kuishi hapa chini ya jua nimejifunza.....mambo makuu mawili ambayo ni ya msingi sana....
1) UVUMILIVU
Wanadamu tunatakiwa tutambue kuwa hatuwezi kupata kila kitu tunavyovitaka au hatuwezi kupata tunavyovitaka kwa wakati tunapovitaka......UVUMILIVU ndio silaha ya mwisho ya mwanadamu katika kuyaelekea mafanikio ya kweli.....

2) SUBIRA
Katika ulimwengu wa subira hakuna linaloshindikana.....hata Muumba aliahidi kuwa pamoja na wale wenye mioyo ya subira....
Na babu zetu wakatuusia kuwa subira huvuta kheri....
 
Mkuu savimbi jr, maisha unayoona kwako ni comedy watu huwa wanapitia katika uhalisia. Msaidie kama una uwezo.
 
= amazing

Wewe ni Kenge Sana,cm yangu nimeweka keyboard automatic neno Amazing kiswaga ni Amaizing najua ni uzee unakusumbua ndio maana swaga za kileo haujui......Peruzi Instagram uone linavyotumika...kenge wahed wewe.
 
Mkuu usiende kwa waganga mwamini Yesu walioenda kwa waganga wameambulia vifo vya ajabu kwa Yesu hupati Leo Ila siku ukipata ndo forever
 
Pole sna.mkuu ! mimi nimemaliza LL.B nimefanya application.zaidi ya 27 sijaitwa hata moja! pole sna Mungu Mkubwa tuko pamoja mkuu
 
Mkuu usiende kwa waganga mwamini Yesu walioenda kwa waganga wameambulia vifo vya ajabu kwa Yesu hupati Leo Ila siku ukipata ndo forever

Mganga ndo kila kitu nawashukuru waganga kwani wamenipa kazi nzuri!
 
Mkuu Sema sas njoo bariadi Kijiji kinaitwa ikongolyabashashi utapata msaada, ukifika ni check
 
Wewe ni Kenge Sana,cm yangu nimeweka keyboard automatic neno Amazing kiswaga ni Amaizing najua ni uzee unakusumbua ndio maana swaga za kileo haujui......Peruzi Instagram uone linavyotumika...kenge wahed wewe.

kwa hayo matusi yako,nadhani itakuchukua zaidi ya miaka 54 kupata kazi.
 
Kwa imani yako tafuta kiongozi wa dini/kiroho mueleze hayo atakusaidia. Hapo naona wingu zito ovu limekufunika.
 
Mimi nina qualification ya shahada ya kwanza ya statiscs na economics toka UDOM 2011.

Niliajiriwa na shirika binafsi kubwa kiasi hivi tokea 7/2011. Nimefanya Kazi kama m&e officer 2 years, program coordinator 2.3 years. Nimeudhuria short courses zaidi ya 20 Tanzania hii kuhusu kilimo, m&e, miradi usimamizi, research, ufugaji, utunzaji mazingira, ukimwi, gender,nk. Sasa mradi umekwisha na mkataba umekwisha pia, nipo kitaa sina Kazi kwa sasa.

Mpaka sasa nimeshatuma maombi zaidi ya 250 kwenye kila sector au shirika iwe wametangaza nafasi au hawakutangaza. Ila sijawahi itwa kwenye interview yeyote ile sijui kwa nini?

Nimewahi kuwekeza kwenye kilimo cha viazi soko lilishuka sana msimu huo nilikulahasara, nikanunua ng'ombe wamaziwa nikamfuga wakati anazaa akafa yeye na kindama chake, nikanunua pikipiki mbili nifanye Bodaboda, moja ikaibiwa na nyingine ikapata ajali, nikafanya utafiti na nikafungua duka kubwa la bidhaa za jumla na rejareja katikati ya mji mwanzoni niliuza sana, competitors wenzangu niliowakuta wakaanza lalamika nachukua wateja wao sikujali, nilifanya biashara miezi 5 tu, mwezi wa 6& 7 mauzo yalishuka toka laki tatu hadi tano na nikawa nauza elfu kumi mpaka 50 tu kwa Siku.

Nikaacha biashara niliendesha kwa hasara. Sasa nipo tu sijui nifanye nini?

Nina mke na mtoto 1. Mke wangu ni mtumishi.Hebu nisaidieni nipate Kazi. Miaka 30 very strong kijana.

Nyongeza: Nimewahi jiunga na biashara ya forever living, nilinunua bidhaa zao nimezunguka nazo usiku na mchana hakuna wateja nikaanza tumia mwenyewe na nyingine nikagawa, nikama nilutapeliwa tu.

Nikakutana na mtu akanishawishi nifuge Kwale wanasoko zuri la mayai na vifaranga, nikafuga Kwale wakaanza taga sana tu, nilizunguka kutafuta wateja wa mayai na vifaranga hakuna kitu.

Pole sana my bro nmeisoma mbk mwsho sometimes unaweza MTU ukafikiria labda umerogwa ukaanza kwenda kwa waganga lakini mi nakuombea ufanikiwe usikate tamaa naamini kuna siku itabaki tu kua stories aya yote
 
Kwani ww ni chama gani?Na ulichagua nani? Masikini Watanzania mmelichagua tena!

Wewe ni bure kabisa....yaani watu wanatoa mawazo na kutafuta muhafaka....mwenzetu unaleta siasa.....inamaana hujui siasa ndo chanzo cha matatizo,hacheni siasa tuishi kama sisi na wao waishi kama wao.
 
Unaonekana ni mtu ambaye huna uvumilivu & unashindwa kutulia eneo moja, ndio maana umejikuta unafanya kila biashara. Nani kakuambia kuwa utapata faida tu bila setback kwa biashara utakayoifanya? Changamoto hutokea, na ndicho kipindi cha kukomaa maana ukivuka hapo next time ikitokea utakuwa na mbinu za kutoka. Lakini kama ukiona changamoto zinatokea, then uka give up na kuanzisha biashara nyingine, itatokea tena na uta give up tena. Mwisho wa siku utakuwa unaona hakuna mafanikio.

Tulia, na anzisha biashara moja na uwe mvumilivu. Mchawi yuko ndani yako mwenyewe. Inuka na umshinde!

sasa mkuu kutoka mauzo laki tatu kwa siku mpaka elfu kumi bado huoni kama jamaa alikomaa sana?.....na hapo kapunguza maelezo vinginevyo angekutajia alivyoplomoka mauzo.....laki mbili....laki...elfu hamsini.nk.....ingejaza uzi mkuu.
 
Huwezi kujaza application form 250 halafu ukakaa nyumbani ukisubiri jibu, ilibidi ufatilie ni bora kwenda mwenyewe na kuongea ana kwa ana kuliko kutuma maombi hilo moja umefeli.
La pili unafanya biashara kwa miezi 6/7 halafu unategemea kupata faida na kuendelea.
Mbona unaonekana msomi halafu hufuati kanuni za biashara hujui kuwa biashara 100 zinazoanzishwa ni chache sana zinavuka miaka miwili zingine hufa kama yako?



. Hilo la pili jombaa si kashasema bihashara ilikufa.....sasa kama bihashara ikifa si unaachana nayo au ulitaka na yeye afe na bihashara yake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom