Nimepiga block ombaomba wote mpaka baba na mama

Nimepiga block ombaomba wote mpaka baba na mama

Wewe ukizikwa hata na taifa zima.
Viongozi, wachungaji na masheikh au hata na Malaika nini kitabadilika au utamzidi nini yule aliyetupwa jalalani?
Kuna Watu mnafikiri kwa namna ya kuchekesha sana.

Duuh inashangaza kama mzee kama wewe unafikiri namna hii basi iko shida mahali hivi ni kweli mnaamini kuzika so muhimu tena anyway things a changing
 
Mzee unaishi kama umedondoka na parachute kisiwani, ukimsaidia mtu sio kwaajili yake, sababu shida za watu haziwezi kuisha, ni kwaajili yako wewe mwenyewe kama binadamu mwenye utimamu.

Jifunze kusema hapana kama huna, jifunze kusema sina hiyo uliyoomba naweza nikakupa robo yake etc.

Binafsi raha yangu ni kutumia hela yangu na niwapendae. Hela tamu sana, tamu zaidi nikishare na wamuhimu.

Kikubwa tutafute hela, umasikini unaleta roho mbaya.
 
Niliwahi fanya hivyo kwa ndugu zangu ila sio kwa kiblock namba zao ila tu nilivunja line na kusajili nyingine.
Sababu ilikuwa ni baada ya kupata shida mzazi wangu akakataa kunisaidia( nilimwomba anikope sh laki 5 ili nikatangulize kwa mdeni wangu mzazi alikataa kunikopesa alikataa kwa sababu nililiona salio lake bank alikuwa na milion kumi na mbili.
Kuninyima sawa pengine ana matumizi nayo ila klichoniuma zaidi ni yeye kuanza kufurahia matatizo yaliyonikuta huku akisema acha nikome)
Ndugu zangu nao hakuna aliyenisaidia zaidi na wao kuniombea mabaya..
Nilikamatwa na kuwekwa ndani siku mbili siku ya kwanza mama yangu alipopata taarifa kauli ni ile ile acha nikome kwani mimi sio wa kwanza kufungwa na pia swala la mdhamini nitajijua labda mwajiri wangu ndio atanitolea dhamana..
Baada ya kutoko lockup nilibadili line zangu zote

Ila baada ya mwaka mmoja nilimtafuta mzazi wangu nikamchana ukwli kuwa alivyonifanyia sio poa
Naye sijui yalimuingia maneno alinikatia milion mbili akanipa na ndugu zangu baadhi niliendelea kuwasiliana nao wengine mpka leo wameumute..

NB kwa kitendo alichonifanyia mzazi nakili mpka leo niliakbulia presha na vidonda vya tumbo vitu vinavyonitesa hadi leo..

Ila nashukuru kwa kuwa nimejifunza kitu kuwa usimtegemee mtu too much na usijitoe kwa mtu too much maana siku yakikukuta hutoamini majibu yao..

Nilimsamehe mzazi wangu ila kiukweli sina imani naye tena..
Nikipata shida yoyote mzazi wangu atakuwa wa mwisho kuijua na ataijua pale nitakapokuwa nimekosa mtu wa kunisaidia na hata nikimwambia ni ile tu ngoja nijaribu..

Sababu ya kukamatwa ni madeni ya mashine za ushuru wa serikali.
Nakumbuka muda wowte siku yoyte mzazi alikuwa akiniomba pesa(anaweza omba sh 10000 nikatuma 20000, akaomba 30000 nikatuma 60000 n.k) na pesa hizo nilikuwa namega kwenye pesa ya mashine ya ushuru..
Mwaka 2019/2020 kulikuwa na ukame nilimnunulia mchele jumla ya gunia tatu nikamtumia kwa nyakati tofaut ili kunusuru hali ya njaa yote haya niliyafanya kwa pesa ya mashine ya ushuru..
Siku mahesabu yangu yameenda kombo ndo alivyonifanyia kama nilivyoeleza hapo juu..


USHAURI KWA MTOA MADA.
usimblock mtu yoyote bila sababu ya msingi tena hasa mzazi na ndugu kwa kuwa sio kila ukiombwa kitu lazima utoe.
Mafano ukiombwa pesa na hauna usiibe et umtumie pesa au usilale njaa kisa umtumie pesa mtu.
Mwambie huna tu au muahidi utampa netx tym..

Shida hazina fomula wala muda wa kukuijia na hujui itakuja shida gani na kwa muda gani..

Shida ni dude la ajabu huwa lina tabia ya kukupeleka kwa uliowakana ili waitatue.
Mkuu pole saana ila Kaa kimya Kwa yaliyonikuta lako dogo. Sukukurupuka kuandika huu uzi
 
Wengine tunatamani tuwe na kipato kikubwa tusaidie wazazi wetu maana umri wao umeenda hata nguvu zao za kufanya kazi zimepungua hawana msaada zaidi ya Mimi ila wewe unawakataa? Kweli binadamu tunatofautiana
 
Mimi mara nyingi baba au mama akinipigia simu kuhitaji hela hua sijiulizi mara mbili kama kaomba 50k Nampa 100k, mabro itategemea na alivonielekeza [emoji848]wengn itategemea tupoje mm na ww, wanaume hua tuanasaka Kwa namna ngumu ila hatuli pekee yetu
Nakazia hapa, kwa wazee wangu ntajitahidi kiasi chake...
 
Mnambembeleza mtu ambaye kasha jichokea na maisha.Mpaka kafika hapo kala vya wazazi ama walezi vingapi harafu sasa hivi kakua kapata vijisenti ananyea kambi wapuuzi km hawa unawaacha tu majibu hayachelewi l..Ww unamblock mzazi kisa kaomba hela [emoji3064].Ww wablock sana hata simu usiwapigie majibu utakuja kuyapata hapa hapa duniani.
Nakazia hapa..
 
Haya maisha ukizaa usitake umperekeshe mtoto wako, kama hukujipanga ukiwa kijana ni wewe mwenyewe na ujuha wako

Mtu yoyote akisema tu nisaidie kitu flani nakata simu na block juuu, elewa neno mtu yoyote hata kama ni kaka, dada, baba au mama napiga block kila mtu afanye maisha yake sitaki upuuzi wa kuharibiana bajeti apaa

N. B. laana ni neno la kutengezezwa tu Wala hakuna kitu laana kama inavyohisiwa
Huenda ukawa na laana, au unaelekea kupata laana.
 
kunanguvu kubwa kwenye utoaji unaozingatia bajeti yako
Kama nafasi yakutoa ipo toa kama haipo sidhambi kusema sina ila kuwablock wazazi au wakuombao ni lack of confidence
 
Back
Top Bottom