Nimepata sababu ya kutoacha Pombe...

Nimepata sababu ya kutoacha Pombe...

sasa mtu akiwa anakula chakula, anaitwa na watu mlafi, unafikiri alikuwa anakula hadi kuvimbiwa? na mtu kama alikuwa anakunywa divai, na watu wakasema mlevi, unafikiri alikuwa anakunywa pombe?...hivi kula ni ulafi? na kunywa ni ulevi?....cha maana ni kwamba, Neno la Mungu haliwezi kujipinga, Kuna maeneo mengi mno nitakuletea yanaongelea kuwa pombe ni haramu..na Biblia inasema Yesu hakutenda dhambi hata moja, hivyo kama pombe ni haramu, Yesu hakunywa, angekuwa amekunywa Yesu asingesemwa kuwa hakutenda dhambi...Unaliamini Neno la Mungu kuwa ni amina na kweli? au? hivi wewe ukichukua ule mvinyo mweusi uliotokana na kuchujwa kwa zabibu ukanywa ina maana unakuwa umekunywa pombe?

zaidi ya yote, unachotakiwa kujua ni kwamba, kipindi kile, hakukuwa na chai ama kahawa ama vitu vingine hivi...mtu akila mkate, alikuwa anashushia na divai (isiyolevya), divai ilikuwa kama chai ya sasa, haikuwa inanywewa ile ya kulevya. sasa, watu wote utakaowapotosha hapa kwa maneno yako, damu yao itadaiwa mikononi mwako siku ile ya mwisho...!




Nashindwa kuelewa hivi "Mvinyo" ni kilevi? Nikielewa hapo then ntarudi kuchangia
 
Back
Top Bottom