Nimepata sababu ya kutoacha Pombe... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimepata sababu ya kutoacha Pombe...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Asprin, Jul 16, 2010.

 1. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Hapo awali msimamo wangu ulikuwa kwamba nitaacha pombe endapo tu:

  1. Nimeshauriwa na daktari kwa manufaa ya afya yangu.
  2: Nimeishiwa kiasi kwamba kununua bia unakuwa mzigo mkubwa

  Nilishawishiwa na baadhi ya watumishi wa Mungu kuwa niache pombe, kwa kuwa eti pombe ni dhambi (imagine, eti bia ni dhambi?). Aisee walikaribia kufanikiwa mpaka nilipokutana na Neno Hili Takatifu toka katika kitabu Kitakatifu Cha Mungu. Hapa aliandika Mtakatifu Matayo katika Sura ya 11 ya Injili yake:
  16"To what can I compare this generation? They are like children sitting in the marketplaces and calling out to others: 17" 'We played the flute for you, and you did not dance; we sang a dirge and you did not mourn.' 18For John came neither eating nor drinking, and they say, 'He has a demon.' 19The Son of Man came eating and drinking, and they say, 'Here is a glutton and a drunkard, a friend of tax collectors and "sinners." ' But wisdom is proved right by her actions."

  HILO NDILO NENO LA MUNGU!

  Leo ntakunywa bia kwa raha sana.

  Ahsanteni na wikiendi njema!!!!
   
 2. RR

  RR JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Shinda na usilegee.....
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Lazima tumuenzi Bwana Yesu..
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Hahahaha! nimeona na hii:

  Beer helps u get un-sober!
   
 5. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  ha ha subili watumishi wa Mungu waje wakubishie mpaka kesho hawatakubali na kukupa laana juu. lkn ukweli ni kwamba Mheshimiwa alikuwa anaonja kinywaji japo wanasema hakikuchachishwa mi sijui.
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Labda kama watabishana na Neno La Mungu.

  Bwana Mkubwa alikuwa anakunywa hii kitu, kwanini nisifuate nyayo zake?
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asprin unatakiwa usome Biblia yote na kuichambua sio kipengele kimoja tu unajihalalisha kunywa pombe.
  Kwanini ukinywa pombe kina eliza woote unawaona warembo wakati kabla ya hapo ulikuwa unawaona wa kawaida?
  Pombe inachochea maasi ..
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Labda uniambie kama nimeongeza kitu kwenye hayo maandiko.

  Ukweli ni kwamba chochote ukikitumia vibaya kinasababisha kutenda dhambi. Kisu ukikitumia vibaya si unaua? Kwa hiyo kisu kikatazwe kutumika?
   
 9. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hahaha, rafiki yangu, Yohana alikuwa anakula asali na nzige/senene bila shaka. hicho ndo kilikuwa chakula chake. Yohana alikuwa hali mikate kama Yesu, wala alikuwa hanywi divai kama Yesu. Cha kuelewa hapa ni kwamba, si divai zote ni kilevi, kuna divai ya kulevya na divai isiyolevya. na hiyo ndiyo ilikuwa served kwenye meza wakati ule. watu wengi wamepotea kwa kufikiri Yesu alikuwa kilevi, hapana. ninaenda kujipanga afu muda wowote nitakuibukia na mistari ili niueleweshe ulimwengu wenye imani kama yako...hii ilichanganya watu wengi kwasababu Yesu alikuwa anaingia na kula hata kwenye nyumba za wenye dhambi, lakini hakuna sehemu yoyote wamesema likuwa anakunywa kilevi...bali mvinyo madunda ya zabibu ambazo hata wewe unakunywa ili kuongeza damu..si ile inayolevya.

  zaidi ya yote, kwasababu Yesu alijua watu wagumu kumuelewa, ametutumia Roho Mt, ambaye Yesu alisema atatutia kwenye kweli yote. Ukiwa umejazwa Roho Mt. hauna haja ya kuuliza maswali yote haya, hauna haya ya kuhangaika na mambo ya kwenda kimwili haya...Roho Mt. atakuambia kitu gani ni halali na kipi si halali...nakushauri uokoke ili umpate Roho Mtakatifu aliyeahidiwa kwa wote watakaomwamini Yesu na kuokoka....hauhitaji maswali yoyote yale...atakuambia kipi ni halali.atakutia kwenye kweli yote wakati anapokuwa anakuongoza...na Roho Mtakatifu wa Mungu amethibitisha kabisa kwenye mioyo yetu kuwa pombe ni dhambi and it damns the soul.

  tatizo kubwa, watu wengi kwenye dini nyingi kuanzia za kikristo etc, wanaabudu Mungu kimwili, hawamwendei Mungu kiroho. Mungu ni Roho nao wamwabuduo lazima wamwabudu ktk Roho na kweli..that means, ktka abudu yako, imba yako, maombi yako, mahubiri yako etc, lazima Roho mt. ahusishwe,,,kama hatakuwepo Roho Mt.basi roho chafu itakuja na kuhubiri pale na kupotosha, watu watalishwa mawe na kande kama hizo...ukiona unasali kwenye kanisa lisiloamini ujazo wa Roho Mt. kimbia, hapo hapana Mungu na hautahudumiwa na Mungu ktk mahubiri etc. Talk to you soon!
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo, hebu soma hii:

  18For John came neither eating nor drinking, and they say, 'He has a demon.' 19The Son of Man came eating and drinking, and they say, 'Here is a glutton and a drunkard,

  How come mtu anywe divai isiyolewesha halafu aitwe mlevi???? Isitoshe maneno hayo alikuwa anayasema Yesu mwenyewe kuwa amekuja anakula na kunywa watu wakamwita mlafi tena mlevi. Asingeweza kusema nimekunywa divai isiyolewesha mkanisingizia mlevi?
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahaha
  mpwa mtu ambae hata kupa senksi hapa ni MCHAWI
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  The Following 2 Users Say Thank You to Asprin For This Useful Post:

  MZIGOMZIGO (Today), Teamo (Today) ​
  Ahsanteni wanachama wenzangu kwa kulitii neno na Mungu.
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Preventive is better than cure ...Kisu hakiwezi kukukata kama una akili zako timamu na umefata sheria zote za kiusalama wakati wa kukitumia.
  Lakini Pombe ..Dah ukilewa kupita kiasi unaweza hata kukojoa mbele ya mkweo ..ndo nini hiyo bana Asprin...
  Unakuwa huru kuwatongoza tongoza kina Eliza akipita umeshika kiuno ,mala umepapasa nyonyo ,mala aaaaaaaaaaaaaaaaaaggh..
   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Si umeona? Same applies to ulabu. Kama nimepiga bia zangu mbili nikajirudia zangu home kucheza na watoto kuna ubaya wowote hapo na Mungu?
   
 15. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sasa mtu akiwa anakula chakula, anaitwa na watu mlafi, unafikiri alikuwa anakula hadi kuvimbiwa? na mtu kama alikuwa anakunywa divai, na watu wakasema mlevi, unafikiri alikuwa anakunywa pombe?...hivi kula ni ulafi? na kunywa ni ulevi?....cha maana ni kwamba, Neno la Mungu haliwezi kujipinga, Kuna maeneo mengi mno nitakuletea yanaongelea kuwa pombe ni haramu..na Biblia inasema Yesu hakutenda dhambi hata moja, hivyo kama pombe ni haramu, Yesu hakunywa, angekuwa amekunywa Yesu asingesemwa kuwa hakutenda dhambi...Unaliamini Neno la Mungu kuwa ni amina na kweli? au? hivi wewe ukichukua ule mvinyo mweusi uliotokana na kuchujwa kwa zabibu ukanywa ina maana unakuwa umekunywa pombe?

  zaidi ya yote, unachotakiwa kujua ni kwamba, kipindi kile, hakukuwa na chai ama kahawa ama vitu vingine hivi...mtu akila mkate, alikuwa anashushia na divai (isiyolevya), divai ilikuwa kama chai ya sasa, haikuwa inanywewa ile ya kulevya. sasa, watu wote utakaowapotosha hapa kwa maneno yako, damu yao itadaiwa mikononi mwako siku ile ya mwisho...!
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  Hivi Asprin na Teamo hizi bear or something yenye kilevi haina madhara kwenye afya ya binadamu kama mimi???
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Andiko lako haliendani kabisa na defence yako. Ningekuwa jaji nawe ni mshitakiwa ningekuhukumu vibao kwanza hapo hapo mahakamani. inaonekana umezoea kukariri maandiko tu. Hata kiingereza kidogo kama hicho unashindwa kuelewa? and you call yourself a great thinker??

  Mwanzoni nilidhani unaquote andiko linalosema..."mpe maskini kilevi asahau shida zake" na hilo sikwambii liko wapi.

  Ila kumbuka pombe huharibu fikra ikishatumiwa na kumfanya mtu kutenda mabaya mbele za watu na Mungu.
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,760
  Trophy Points: 280
  Divai ilikuwa haileweshi? Kuna maandiko nimesahau vifungu (damn beer). Lutu (Sijui Nuhu?) alinyweshwa divai na mabinti zake akalewa mabinti zake wakalala naye.. Unaijua?

  Sina nia ya kupotosha watu hapa mkuu. Nimetoa kifungu ambacho Yesu mwenyewe anasema watu walimwita mlevi, kwa maana alikuwa anakunywa. (Haikuelezwa kama alikuwa anakunywa divai isiyolewesha, sijui wewe ulijuaje) Isitoshe katika biblia pia kuna vifungu vinahalalisha watu kula ulabu; "Mpe maskini kileo, anywe alewe asahau shida zake" umeshawahi kuiona hii?
   
 19. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hivi wale jamaa wa Alshabab wa somalia - waasi wa serikali ya Somalia (kama ipo) nao wanakunywa sana pombe eehh!! au maasi unayongelea ni asprin kumuona Eliza mzuri baada ya bia ya saba na valuu mbili?
   
 20. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  enzi zote pombe ni haram. kizazi cha kanaani kililaaniwa kwasababu ya pombe pale Nuhu babu yao alipolewa na Ham akauona uchi wa babake. unakumbuka Lutu alilewa binti zake wakalala naye na wakapatikana kizazi cha waamoni na wamoabu watu ambao kwasasa ni raia wa Jordan na maeneo ya syria and around that area. Biblia inasema kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu na kuwa waasherati, wazinzi na walevi hawataurithi ufalme wa Mungu. Pombe ni shetani, maeneo yote yanayouzwa pombe yana harufu kabisa ya shetani na vitu vyote vya kishetani vinapatikana pale, kuanzia kupapasapapasa wanawake/uzinzi,kuibiana kufanya kila kitu. JAMANI, NURU NA GIZA VIKO WAZI MNO, NI DHAHIRI HAVIHITAJI KUJIULIZA MASWALI...hili mbona liko wazi, pombe ni giza na siku zote wanywaji wa pombe wanaogopa mwanga...Neno la Mungu,,,hata kama hawatakwambia lakini roho zao huwa zinawasuta muda wote kwamba wanatenda dhambi. Mungu awasaidie.
   
Loading...