#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Kwa hiyo sasa hivi hamuogopi tena maambukizi ya corona! Yaani hamna haja ya kutumia barakoa wala kunawa mikono kama njiamojawapo ya kujikinga maambukizi haya ya covid19!?

Nasubiri majibu.
Kwani ukitumia condoam kujikinga na UKIMWI halafu ukaenda hospitali ikatakiwa upewe damu utasema hiyo damu wasiipime UKIMWI kwa sababu umevaa condom?
 
serikali inaendelea na utafiti kuhusu hiz chanjo,wewe ulitaka itoe majibu ya haraka haraka bila analysis ya kutosha!? kumbuka haya Mambo sio upatu,ni science inahitaji muda wa kutosha kufanya analysis juu ya hiz chanjo.hatutaki kukimbilia chanjo ambayo bado Ina walakini kwenye ufanisi.hongera kwa kuchanja pia mkuu,Ila reaction na impact ya chanjo sio ya miez 2 au 3,u can't be sure abt the doses u took.
 
Dah pole sana. Mungu aendelee Kutunusuru na haya Maradhi mhh inatisha maumivu uliopitia
 
Nauliza hivi kwanini wewe unaona uamuzi ni kuagiza haraka haraka hizo chanjo hali ya kuwa bado zipo kwenye majaribio? kwanini umeng'ang'ania hizo chanjo hali ya kuwa bado hazijajulikana hata madhara yake?
Mataifa yote yanazigombania tena yake yenye akili sisi huku kajamba nani tusijitie wajuwaji
 
Huyu kakariri sayansi ya kwenye kitabu hataki kwenda na wakati.
Tena ni kitabu cha mwalimu wake, tena leo anaanza kumpinga mwalimu wake kisa eti katumia formula ambayo yy haijui!!

Ni bora chanjo ipelekwe kwa ngiri wanaokaa kenya, ug, rwanda na kwingineko!

Na kwamba binadam wa tz sio watu wamchezo mchezo!
Yaani....basi tu!
 
Hili jibu linathibitisha kuwa hizo chanjo hata ninyi mliodungwa mna wasiwasi! Yawezekana ni kwa shinikizo mmedungwa vinginevyo msingekubali! Poleni na mvumilie. Sisi tunawaombea zisiwazuru hizo chanjo! Kwani mkidhulika watengenezaji na wasambazaji wa chanjo hizo hawatahusika kwa namna yoyote ile kisheria.
 
Dah pole sana. Mungu aendelee Kutunusuru na haya Maradhi mhh inatisha maumivu uliopitia
Haielezeki...imenidhalilisha sana..maana hata nguo za muhimu nilishindwa vaa .nikapangiwa sindano za diclofenac ..sisahau akili kuwa za kuruka ruka siwez sahau
 
Mataifa yote yanazigombania tena yake yenye akili sisi huku kajamba nani tusijitie wajuwaji
Sawa ila nachosema mimi kutoharakisha kuagiza hizo chanjo pia ni uamuzi kama ambavyo hao wengine wao wameamua kuharakisha kuagiza hizo chanjo,hapo hakuna mjinga wala mjanja kwa sababu chanjo bado zipo majaribu.

Katika hayo mataifa yenye akili kuna ambayo raia zake wamekufa sana kwa corona na sababu moja wapo ni kwamba tunaambiwa walifanya uzembe wa kuchelewa kuchukua tahadhari mapema.
 
Kuna jamaa alisema unavaa barakoa halafu unang'atwa na mbu!
Asilimia kubwa ya makabila ya tz ni walevi mbwa, kitaifa ndo sekta inayochangia pakubwa kwenye pato la taifa.

Sasa mlevi na barakoa wapi na wapi!?
 
Waswahili walisema, mbio za sakafuni, huishia ukingoni.
 
Logical non sequitur.

Wasiwasi ni nini? Unaupimaje? Kwani nani alikwambia kuna chanjo iliyo 100% efficient?

Na kama hamna chanjo iliyo 100% efficient, hilo linamaanisha hakuna chanjo inayofaa?

Wewe unapopanda gari unajua kwamba hilo gari halitapata ajali siku hiyo?

Kitu gani kinakufanya ukubali kupanda gari hata kama hujui siku hiyo itaishaje?
 
Mbona kama mnateseka kuhusu sisi na chanjo??

Maisha ni yetu,,afya yetu sasa kipi kinawauma?

Maralia inayomaliza watu africa miaka na miaka mbona wazungu hawajawahi kuona hili ni tatizo kw africa wakalivalia njuga??
 
Nikilazimika nitachanja, kama silazimiki sichanji. Simple as that.
Sasa utaipata wapi mjomba au unadhani chanjo inauzwa kama Condom zinavyouzwa huko kwenu Buza kwa Mpalange.. Chanjo inaagiza nchi na Mwenye nchi kasema haleti kwa wala usiahangaike kushupaza shingo. Nyau we
 
Mbona kama mnateseka kuhusu sisi na chanjo??

Maisha ni yetu,,afya yetu sasa kipi kinawauma?

Maralia inayomaliza watu africa miaka na miaka mbona wazungu hawajawahi kuona hili ni tatizo kw africa wakalivalia njuga??
Kwenye sisi kuna wazazi wangu au
 
Mbona kama mnateseka kuhusu sisi na chanjo??

Maisha ni yetu,,afya yetu sasa kipi kinawauma?

Maralia inayomaliza watu africa miaka na miaka mbona wazungu hawajawahi kuona hili ni tatizo kw africa wakalivalia njuga??
Wewe na nani, maisha yenu na nani. Isemee familia yako sisi wengine tunataka. Ujinga na ushamba wenu msitulazimishe wote. Nyau we
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…