#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Ninyi ndio Wachawi dhidi ya Umma,mshaurini Mwanamalundi kwa staha ambalo chanjo kwa raia wake
Chanjo bado zipo katika hali ya majaribio kwa wakati huu hatuwezi kusema si salama au kusifu mafanikio ya hizo chanjo,ni mapema bado. Sasa sijui kwanini tunamshinikiza rais aamue kukubali chanjo haraka haraka ikiwa mwenyewe ameona kuna haja kusubiri kwanza. Kwanini uamuzi wake uonekane si sahihi na kuonekana uamuzi ni mmoja tu wa kukubali haraka kuagiza chanjo?
 
Sasa sijui kwanini tunamshinikiza rais aamue kukubali chanjo haraka haraka ikiwa mwenyewe ameona kuna haja kusubiri
Anasubiri nini kweni sisi ni Ng'ombe wake?...sisi ni raia tunaolipa kodi hiyo kodi yetu anunulie chanjo bhana
 
Mimi phase 1 sikuumwa kabisa nadhan nna zaidi ya mwaka sijaumwa kitu( hapa nilikua kama kibarua kwa wahindi vile sikua na muda wa kurelax)..hii ya term hii imenipata coz siutumikishi mwili kbs..ninalala mno nimerelax mno ..mm sitembei kbs ...uvivu ..plus nna pumu ....yaan najuta endelea kuuchosha mwili ..bora nirudie maisha ya nyuma heka heka
Yes nahisi watu wenye maisha yakurelax haka kagonjwa kanawapenda mno..!! Ila kama una pumu ili tatizo..!! Lakini ndo kusema tulioumwa phase 1 tayar tuna herd imunite ya kagonjwa haka au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefanikiwa kupata chanjo ya Corona hapa napoishi na kufanya kazi Dallas, Texas. Nimepata dose mbili za sindano kwenye bega ya kwanza tarehe 5 mwezi wa pili na ya pili tarehe 4 mwezi wa tatu. Nimepata chanjo kutoka kampuni ya Moderna. Nilivimba kidogo kwenye bega kwa mara zote lakini sijapata homa kama watu wengine wanapata homa kwenye sindano ya pili.

Chanjo ni muhimu na zinaokoa maisha hasa kwa wale wenye au ambao waliwahi kuwa na pumu, kisukari, wazee, wenye magojwa ya moyo na wamegundua pia wenye type A ya damu nao wanaumwa sana wakipata corona. Asilimia 90% ya watu wakipata hawazidiwi hivyo inawezekana hata wewe umeshapata Corona bila kujua. Lakini baada ya siku 90 unaweza kupata tena na inaweza kuwa mbaya zaidi maana mwili unakuwa hauna nguvu sana. Kwasababu kirusi cha corona kimekaa zaidi ya mwaka kinabadilika ili kiweze kuingia kirahisi kwenye miili yetu hii kitaalamu wanaita variant. Hivyo mpaka sasa kuna variant ya South Africa, England, Brazil na ili ya China. Ya South Africa ndiyo kali kuliko zote na ndiyo imeingia Tanzania kwa sasa na kusababisha watu kufa na kuumwa sana kulinganisha na ile ya mwanzo.

Kwenye kinga kuna kinga nyingi sana cha maana ni upatikanaji, usalama na chanjo kufanya kazi. Kuna vipimo vikubwa viwili vya kuzingatia cha kwanza ni kinga ya chanjo yaani ambayo inazuia mtu kupata Corona lakini cha pili je mtu akipata corona ambaye ana chanjo ataumwa kiasi cha kulazwa au kuzidiwa?. Hii ya south Africa inaonyesha kinga haifanyi kazi vizuri hasa kwa hii chanjo ambayo nchi za Africa inauziwa za Oxford Astrazenica au AZD1222. Hawajatoa data kuonyesha je mtu akiumwa inakuwaje au kinga inakuwaje. Lakini chanjo ya Johnson and Johnson imeonyesha inakinga ya corona ya south Africa kwa asilimia 57% lakini hata ukipata corona ni karibu 100% hautazidiwa. Lakini mpaka sasa HAKUNA MTU ALIYEPATA CHANJO YEYOTE POPOTE NA KUUMWA NA KUZIDIWA KIASI CHA KULAZWA. Hii ina maana gani ni kwamba inawezekana kinga ikawa ndogo lakini watu nhawatapoteza maisha ambao wana chanjo

Tanzania wanaogopa chanjo kama hii niliyopewa kwasababu inatumia technologia ya mRNA ambayo ni ya DNA na wanaogopa eti DNA zetu wazungu watabadilisha. Wakati nimeenda kupata chanjo kulikuwa na wazungu wengi wamepewa chanjo kama yangu sasa sijui hizi habari ni za wapi?!!!. Lakini kuna chanjo ambazo zina technologia kama chanjo za zamani mfano Sputnik V ambayo ni ya Urusi inatumia technologia ya zamani ya chanjo na sasa wamefanya utafiti unaonyesha inakinga aslimia 90%. Lakini hii ina order nyingi hasa huko South America itachukua muda kuipata.

Hivyo ushauri wangu ni kwa serikali kutumia chanjo yeyote kasoro ile ya China ambayo haina data ambazo watu wamezionana kusema zipo sawa. Lakini hii wenzetu wa Kenya, Nigeria, Ghana wamepata chanjo yenyewe inawezekana kinga ni ndogo kwa hii ya south Africa lakini ukipata chanjo corona itakuwa kama mafua ya kawaida haitakuuwa kama sasa hivi. Hivyo nashauri bado ni bora sana kuliko kukaa na kutokufanya maamuzi yeyote. Tukiweza kuweka order hii ya J&J ni zuri kwasababu ni sindano mmoja na inahitaji jokofu la kawaidia kuifadhi.

Tatizo serikali inaweza kusema wataalamu wanachukungaza lakini mpaka sasa hakuna habari yeyote uchunguzi umefika wapi, nani yupo kwenye hiyo team inawezekana ni maneno tu.
Hakuna haja ya kuendelea kujifukiza
 
Binafsi nafanyia shuhuri zangu kariakoo, Dar es Salaam..!! Kiukweli phase 1 ya Corona ndo niliumwa japo sikupima ila zile dalili niliziona niza Covid..!! Lakini sikufikia hali kama hiyo zaidi mafua tu.. sikuwah kulala kisa nimezidiwa wala sikuwah kuacha kwenda kariakoo kutekeleza majukumu mpaka nilipokuja kupona kwa mchanganyiko wa Tangawizi, Malimao na kitunguu swaumu basi..!!

Phase 2 binafsi sijaumwa..!! Na ata watu wengi wa kariakoo waliumwa phase 1 ila phase 2 ninaowajua sijaona ambae ameumwa Covid.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo phase 1 ulihitimisha vp kuwa ni corona maana hizo dalili hutumika kwa magonjwa mengine pia si corona tu?
 
Same here. Nimechanja ya kwanza ya Pfizer, baada ya wiki tatu nitachanja ya pili. USA.

Sikuumwa kichwa wala kupata homa.

Watanzania wengi waliopo Tanzania wanajazwa ujinga na serikali inayohoji chanjo kwa sababu za kisiasa.

Serikali ingesema tu haina hela za kuwapa wananchi chanjo, watu wangeisaidia.

Ajabu ni kuona watu wanaogopa chanjo halafu wengine wanavaa mpaka chupi za mtumba hawajui zimepakwa nini!

Dawa wanazotumia hawatengenezi wao, maji yanasafishwa na kemikali za ku import, karibu kila kitu tuna import. Na uwezo wetu wa kuhakiki viwango ni mdogo sana.

Halafu mtu anashikia bango chanjo!
Kwa hiyo sasa hivi hamuogopi tena maambukizi ya corona! Yaani hamna haja ya kutumia barakoa wala kunawa mikono kama njiamojawapo ya kujikinga maambukizi haya ya covid19!?

Nasubiri majibu.
 
Mabeberu wanataka kutubadilisha DNA afu tuwe ngombe ili waje kuchimba madini yetu!! Sisi hatuchanji ... ni mwendo wa nyungu mbele kwa mbele.

Afu haya ma chanjo chanjo haya yanaletaniza Corona.

Sasa uwe ngombe mara ya pili inawezekana vipi. Hapo ulipo huna tofauti na huyo ngombe kwa akili hizo
 
Mkuu hiyo phase 1 ulihitimisha vp kuwa ni corona maana hizo dalili hutumika kwa magonjwa mengine pia si corona tu?
Nimeeeleza hapo kuwa japokuwa sikupima ila kwa mafua ya corona yalikuwa tofauti na mafua ya kawaida..!! Yalikuwa mepesi mno, yalikuwa yanatiririka tu na sometime unajihisi hauna mafua ila unakuta yanatoka.. ila shukrani za pekee ziende kwa Mamaangu kwakunipa ushauri wa dawa tajwa hapo pamoja na Mkewangu kuniandalia kila siku bila kuchoka kuhakikisha mumewa nakuwa sawa..!! Pia mamalishe wa Kariakoo nao waliuza sana chai ya tangawizi kipindi kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anasubiri nini kweni sisi ni Ng'ombe wake?...sisi ni raia tunaolipa kodi hiyo kodi yetu anunulie chanjo bhana
Nauliza hivi kwanini wewe unaona uamuzi ni kuagiza haraka haraka hizo chanjo hali ya kuwa bado zipo kwenye majaribio? kwanini umeng'ang'ania hizo chanjo hali ya kuwa bado hazijajulikana hata madhara yake?
 
Nimeeeleza hapo kuwa japokuwa sikupima ila kwa mafua ya corona yalikuwa tofauti na mafua ya kawaida..!! Yalikuwa mepesi mno, yalikuwa yanatiririka tu na sometime unajihisi hauna mafua ila unakuta yanatoka.. ila shukrani za pekee ziende kwa Mamaangu kwakunipa ushauri wa dawa tajwa hapo pamoja na Mkewangu kuniandalia kila siku bila kuchoka kuhakikisha mumewa nakuwa sawa..!! Pia mamalishe wa Kariakoo nao waliuza sana chai ya tangawizi kipindi kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimekuelewa ndio maana nakuuliza kwanini ulifikiria kuwa itakuwa ni corona kwa hizo dalili ambazo zinafanana na magonjwa mengine pia?
 
Back
Top Bottom