#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Duh! Wewe kweli ilikutenda vibaya
Jumamos niliwehuka na jumatatu🤣...leo hii ndo nmeweza kaa sebulen...toka asbh nimekaa nilikua siwez naona makalio yana vichomi sijui miba..mbavu sasa...hom sikuwaambia .nimewaambia jumatano juzi wamepanic mno! Nilikua naongea sentens 1 ya 2 haitok nabak natoa macho
 
Mie natamani sana hao wanaokataa chanjo waugue....huu ugonjwa mie naweza kesha siku nzima nikihadithia jinsi unavyotesa... unanyong'onyeza mno kwa muda mrefu nowonder wazee inawaonda mapema sana..ni mateso makali sana
Utajuaje kama hawajaugua?maana tunaambiwa wanaoumwa na kupona ni wengi kuliko wanaokufa.
 
Jumamos niliwehuka na jumatatu...leo hii ndo nmeweza kaa sebulen...toka asbh nimekaa nilikua siwez naona makalio yana vichomi sijui miba..mbavu sasa...hom sikuwaambia .nimewaambia jumatano juzi wamepanic mno! Nilikua naongea sentens 1 ya 2 haitok nabak natoa macho
Mmmh kweli hii corona ya sasa ni kiboko, wacha tuendelee kuchukua tahadhari tu
 
Nilisema hivyo hivyo....maumiv ya corona ni habari tofauti...umewah jiskia kujisaidia ukashindwa jisaidia wewe...hata kuoga unashindwa...unalia tu kwa maumivu.mie nimepima had uric acid hakuna...hebu toa domo lako hapa...mpk leo misuli ya miguu na shingo vinapasua...
Binafsi nafanyia shuhuri zangu kariakoo, Dar es Salaam..!! Kiukweli phase 1 ya Corona ndo niliumwa japo sikupima ila zile dalili niliziona niza Covid..!! Lakini sikufikia hali kama hiyo zaidi mafua tu.. sikuwah kulala kisa nimezidiwa wala sikuwah kuacha kwenda kariakoo kutekeleza majukumu mpaka nilipokuja kupona kwa mchanganyiko wa Tangawizi, Malimao na kitunguu swaumu basi..!!

Phase 2 binafsi sijaumwa..!! Na ata watu wengi wa kariakoo waliumwa phase 1 ila phase 2 ninaowajua sijaona ambae ameumwa Covid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi nimeacha hata kulala na shemeji yenu kwa hofu kuwa anaweza kuja nao kutoka huko sokoni
Mimi nilijihamisha mwenyewe..nilikua nataka nife asinione mtu😀..nahangaika alone maana maswak meng kwan unaumwa nn? At first day nilihis nimeconceive🤣🤣...shenz...nilikua nyonde mno...sielew nn nataka
 
Nimefanikiwa kupata chanjo ya Corona hapa napoishi na kufanya kazi Dallas, Texas. Nimepata dose mbili za sindano kwenye bega ya kwanza tarehe 5 mwezi wa pili na ya pili tarehe 4 mwezi wa tatu. Nimepata chanjo kutoka kampuni ya Moderna. Nilivimba kidogo kwenye bega kwa mara zote lakini sijapata homa kama watu wengine wanapata homa kwenye sindano ya pili.

Chanjo ni muhimu na zinaokoa maisha hasa kwa wale wenye au ambao waliwahi kuwa na pumu, kisukari, wazee, wenye magojwa ya moyo na wamegundua pia wenye type A ya damu nao wanaumwa sana wakipata corona. Asilimia 90% ya watu wakipata hawazidiwi hivyo inawezekana hata wewe umeshapata Corona bila kujua. Lakini baada ya siku 90 unaweza kupata tena na inaweza kuwa mbaya zaidi maana mwili unakuwa hauna nguvu sana. Kwasababu kirusi cha corona kimekaa zaidi ya mwaka kinabadilika ili kiweze kuingia kirahisi kwenye miili yetu hii kitaalamu wanaita variant. Hivyo mpaka sasa kuna variant ya South Africa, England, Brazil na ili ya China. Ya South Africa ndiyo kali kuliko zote na ndiyo imeingia Tanzania kwa sasa na kusababisha watu kufa na kuumwa sana kulinganisha na ile ya mwanzo.

Kwenye kinga kuna kinga nyingi sana cha maana ni upatikanaji, usalama na chanjo kufanya kazi. Kuna vipimo vikubwa viwili vya kuzingatia cha kwanza ni kinga ya chanjo yaani ambayo inazuia mtu kupata Corona lakini cha pili je mtu akipata corona ambaye ana chanjo ataumwa kiasi cha kulazwa au kuzidiwa?. Hii ya south Africa inaonyesha kinga haifanyi kazi vizuri hasa kwa hii chanjo ambayo nchi za Africa inauziwa za Oxford Astrazenica au AZD1222. Hawajatoa data kuonyesha je mtu akiumwa inakuwaje au kinga inakuwaje. Lakini chanjo ya Johnson and Johnson imeonyesha inakinga ya corona ya south Africa kwa asilimia 57% lakini hata ukipata corona ni karibu 100% hautazidiwa. Lakini mpaka sasa HAKUNA MTU ALIYEPATA CHANJO YEYOTE POPOTE NA KUUMWA NA KUZIDIWA KIASI CHA KULAZWA. Hii ina maana gani ni kwamba inawezekana kinga ikawa ndogo lakini watu nhawatapoteza maisha ambao wana chanjo

Tanzania wanaogopa chanjo kama hii niliyopewa kwasababu inatumia technologia ya mRNA ambayo ni ya DNA na wanaogopa eti DNA zetu wazungu watabadilisha. Wakati nimeenda kupata chanjo kulikuwa na wazungu wengi wamepewa chanjo kama yangu sasa sijui hizi habari ni za wapi?!!!. Lakini kuna chanjo ambazo zina technologia kama chanjo za zamani mfano Sputnik V ambayo ni ya Urusi inatumia technologia ya zamani ya chanjo na sasa wamefanya utafiti unaonyesha inakinga aslimia 90%. Lakini hii ina order nyingi hasa huko South America itachukua muda kuipata.

Hivyo ushauri wangu ni kwa serikali kutumia chanjo yeyote kasoro ile ya China ambayo haina data ambazo watu wamezionana kusema zipo sawa. Lakini hii wenzetu wa Kenya, Nigeria, Ghana wamepata chanjo yenyewe inawezekana kinga ni ndogo kwa hii ya south Africa lakini ukipata chanjo corona itakuwa kama mafua ya kawaida haitakuuwa kama sasa hivi. Hivyo nashauri bado ni bora sana kuliko kukaa na kutokufanya maamuzi yeyote. Tukiweza kuweka order hii ya J&J ni zuri kwasababu ni sindano mmoja na inahitaji jokofu la kawaidia kuifadhi.

Tatizo serikali inaweza kusema wataalamu wanachukungaza lakini mpaka sasa hakuna habari yeyote uchunguzi umefika wapi, nani yupo kwenye hiyo team inawezekana ni maneno tu.
Kwa hiyo mkuu saivi huvai barakoa tena na unaingia kwenye makundi makubwa ya watu kama kawaida.
 
Binafsi nafanyia shuhuri zangu kariakoo, Dar es Salaam..!! Kiukweli phase 1 ya Corona ndo niliumwa japo sikupima ila zile dalili niliziona niza Covid..!! Lakini sikufikia hali kama hiyo zaidi mafua tu.. sikuwah kulala kisa nimezidiwa wala sikuwah kuacha kwenda kariakoo kutekeleza majukumu mpaka nilipokuja kupona kwa mchanganyiko wa Tangawizi, Malimao na kitunguu swaumu basi..!!

Phase 2 binafsi sijaumwa..!! Na ata watu wengi wa kariakoo waliumwa phase 1 ila phase 2 ninaowajua sijaona ambae ameumwa Covid.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi phase 1 sikuumwa kabisa nadhan nna zaidi ya mwaka sijaumwa kitu( hapa nilikua kama kibarua kwa wahindi vile sikua na muda wa kurelax)..hii ya term hii imenipata coz siutumikishi mwili kbs..ninalala mno nimerelax mno ..mm sitembei kbs ...uvivu ..plus nna pumu ....yaan najuta endelea kuuchosha mwili ..bora nirudie maisha ya nyuma heka heka
 
Back
Top Bottom