Madhara ya chanjo ya Corona yamefikia hatua gani kwa waliochanjwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Ikiwa ni takribani miaka minne tangu watu waanze kupata chanjo ya Corona kuna mtu yeyote aliyegeuka zombi tangu achomwe chanjo ya Corona kama wapinga chanjo wengi mfano Gwajima walivyokuwa wakitabiri?

Kwa mliowahi kuchomwa chanjo ya Corona mmpetawa na hali gani hasa mbaya ambayo mnaihusisha na chanjo hiyo?
 
Muda ni jibu sahihi chanjo inaishi miaka na miaka mwilini majibu yapo watu waliopararaiz wamekuwa wengi sana
 
Unauhakika kwani hata wasiopata chanjo ya corona pia wengi wanaparalaiz kwa maradhi mengi,mimi na wengine wengi hapa kjijini tuliopata hiyo chanjo tupo fiti tunadunda. Gwajima ni mwongo sijawahi kumwamini
 
Muda ni jibu sahihi chanjo inaishi miaka na miaka mwilini majibu yapo watu waliopararaiz wamekuwa wengi sana
Kuna mtu unayemfahamu aliyethibitika kuparalaizi kutokana na chanjo ya Corona?
 
Ikiwa ni takribani miaka minne tangu watu waanze kupata chanjo ya Corona kuna mtu yeyote aliyegeuka zombi tangu achomwe chanjo ya Corona kama wapinga chanjo wengi mfano Gwajima walivyokuwa wakitabiri?

Kwa mliowahi kuchomwa chanjo ya Corona mmpetawa na hali gani hasa mbaya ambayo mnaihusisha na chanjo hiyo?
Wamekuwa ng'ombe Moo
 
Hayo ni mapuuzi..hao hao wanapinga halafu wanapeleka wtt wao wakapatiwe chanjo tena wakiwa wachanga kabisa..watasema za wtt zimefanyiwa utafiti..haya sisi ndo wale tuliaanza kuchanjwa sindano za kifua kikuu na donda koo enzi hizoo zimeanza anza mbona tupo mpk leo?
 
Jiulize kwanza ambao waligoma kuchanjwa wamepata madhara yoyote?
Waliochanjwa waliona afya zao ni mgogoro kama wazee na wenye magonjwa ya muda mrf..walichanja ili kuboost imunity yao..kwa sisi ambao hatukuchanja tunajijua afya zetu ngangari wengine tuna miaka 5 hatujaugua chochote...hivyo ni mtu na mwili wake..
 
Ikiwa ni takribani miaka minne tangu watu waanze kupata chanjo ya Corona kuna mtu yeyote aliyegeuka zombi tangu achomwe chanjo ya Corona kama wapinga chanjo wengi mfano Gwajima walivyokuwa wakitabiri?

Kwa mliowahi kuchomwa chanjo ya Corona mmpetawa na hali gani hasa mbaya ambayo mnaihusisha na chanjo hiyo?
we zombie, haujui ... la simba madangote
 
Hii chanjo mi niliishtukia kuna mda ilionekana kama lazima kwa watumishi wa serikali nikajiandikisha ila sikuchanja. But madhara yake yanaweza kuanza kuonekana hata kizazi cha 3 sio sada hivi. Wazungu huwa wana plan zao za muda mrefu sana
 
Back
Top Bottom