Nimepata addiction

Nimepata addiction

VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
9,105
Reaction score
14,452
Wakuu,

Sijui natokaje kwenye hii addiction ila alietengeneza hiki kitu hakika ni fundi na amenikamata na sijui ametumia formula gani. Kila nikitumia hua kuna maswaali najiuliza huyu ametumia formula gani?

Haipiti siku namaliza chupa hata 3 mpaka 4.
Addiction.
Screenshot_20260414_000945.jpg
 
Duuh! Pole sana Mkuu jaribu kwa kupunguza idadi, mf kama unakunywa nne kwa siku unaanza kupunguza mdogo mdogo mpaka ufikie moja kwa siku ukiweza kufikia hiyo stage utakuwa upo pazuri.

Na inakubidi upambane haswa maana hizo sukari plus Chemical za humo inakuwa hatari na nusu
Sawa mkuu issue sio sukari hujaelewa kuna ladha fulani hivi ya tofauti hususani ukinywa ya baaridi ile inayokaribia kuganda ili kukata hangover
 
Angalia kwanza Screen time yako ...Angalia unakaa eneo moja kwa muda gani na huwa unafanya nini ?
Mkuu,

Nikwambie kitu? Mimi sipeendi kukaa muda mwingi hua natembea hata nikiwa nafungua hio chupa sipendi kunywa nimekaa chini hua nakunywa huku natembea nakunywa mpaka naimaliza yote
 
Hivi vitu situmii kabisa huwa napiga kahawa tu. Ila nadhani train your mind to stop using those things and each time tengeneza picha unapewa sumu polepole.
Kweli mkuu ila kuna kitu kimoja wewe unapenda kahawa ila mimi kahawa siiwezi sio kahawa tu hata chai siiwezi labda uniwekee mchaichai ila sio majani ya chai siwezi kabisa huwezi amini, hio ninapenda ladha [flavour] sensation of taste fulani hivi imewekwa humo kwenye hio chupa hio ndio inaniita sio kingine kuna kiladha fulani hivi cha tofauti humo, sasa nikianza kunywa sometimes nafikiria sijui nini yaan ningekua hata na pipa limejaa tu hio mimi kazi yangu ni kuchota na kunywa tu, feelings
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom