Nimeona nimuachie tu mtoto

Nimeona nimuachie tu mtoto

Hakuna limit ya kumwona mtoto huyo Ni damu yako asikupangie namna ya kumwona mtoto.

Akisumbua fuata utaratibu wa sheria,kuwa makini Sana na mtoto asije kukuza tabia za ajabu ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mengi sana.

Huyu ni binti ambaye alikuwa mchumba wangu nilimchukua kutoka nyumbani kwao, kwa wazazi wake, akalea mimba na kujifungua kwangu, baada ya kukaa naye kwa muda wa mwezi mmoja akaanza changamoto ya kiburi na jeuri. Nikaamua nimrudishe kwao kwanza na kuwaeleza wazazi wake matatizo yake kumpa muda wa kujirekebisha, hapo mtoto akiwa na mwezi mmoja.

Nilimwambia endapo akihitaji kuendelea na mimi, arekebishe mapungufu niliyoyasema kwao, kuwa na lugha mbaya na tabia ya kutokuwa na shukrani...Basi nikamwacha hapo nikiendelea kuhudumia mtoto kama kawaida.

Baada ya muda akaniambia kuwa hanihitaji tena kwa kuwa amempata mwanaume mwingine ambaye anamjali na kumpenda yeye na mtoto zaidi yangu, nikamwambia tatizo liko wapi? Akasema mimi simjali yeye wala hakuna kitu chochote nilichowahi kumfanyia cha maana, mimi ninamjali mtoto tu, na mwenyewe ni mpaka pale nitakapojisikia, japo niliiwahi kumueleza kuwa uchumi ndio unasababisha huduma zangu zielekee kwa mtoto kwa kiasi kikubwa, japo yapo niliyoyafanya kwake ila hapo hatukuelewana.

Jana kanieleza kwamba nisifike kwao tena kumuona mtoto, kama nitahitaji kumuona nitamuonea njiani tu. Kwa kifupi kasema hakuna chochote ambacho nishawahi kumfanyia yeye labda mtoto kwa kiasi kidogo sana, pamoja na kwamba kila kitu ni mimi ndio anayetegemea nitimize yeye hana kazi hana kipato, hivyo kuanzia kujifungua mpaka sasa mtoto ana miezi minne, ni mimi ndio nilikuwa nawajibika.

Nyumbani anafahamika kwa wazazi, Mojawapo ya matakwa yake kwamba hatofika nyumbani kwetu tena na anahitaji kuwaeleza kuwa kapata mpenzi mwingine, kwahiyo asihesabiwe kwa lolote lile. Mimi pia kanieleza nisifike kwao kumuona mtoto wala kuwaeleza anapokosea, ili ajirekebishe niache tu maana namchafulia, nimpishe huyo mwingine, aje yeye.

Nimekubali madai yake kuwa sijamtreat kwa kiwango atakacho, na jinsi alivyotaka...ndio maana hawezi kurudisha mapenzi kwangu...Sina namna nyingine. Japo nilijitahidi kwa kadri ya uwezo kutimiza kile kinachohitajika nimekuwa nikiiangalia kama familia yangu, hata kama sina nilikuwa radhi nikakope.


Imefika mahali nimeona ngoja tu aende, kuanza upya si ujinga, japo nguvu zangu nyingi nimetumia hapo...

Hapa nilianguka, na kukosea, nimekubali ili nianze kurekebisha...Nimeona nimwage huku hiki kisa maana hakuna anayenijua.

Niliamua kumuwekea uvumilivu na kuwa mtaratibu sana kwake sababu nilishaona simuwezi, hivyo nimeacha tu ajichimbie kaburi mwenyewe. Nimeacha afanye atakacho ili yaishe kwa amani. Na mimi niendelee na mambo yangu mengine.



View attachment 1463216View attachment 1463217View attachment 1463218
Kwa hizo chating zenu,mtarudiana tu...mnatunishiana misuli tu
 
Kama mwanaume sio lazima mpendane na mama mtoto wako cha msingi timiza wajibu wako kama baba tuma matumizi afu piga kimya hamna salamu wala i love you.

Kama huna hela kwa sasa ndo muda wa kutulia kufanya yako,usitume chochote ila ukipata pesa weka akiba siku wakipata tabu sijui mtoto anaumwa watakutafuta ila tafuta mpenzi mwingine huyo mwanamke sio mke ni mzazi mwenzio tu.
 
Dogo kuwa mwanaume, narudia tena kuwa mwanaume!
Acha kuhangaika na mwanamke ambaye hata hujafunga nae ndoa! Ana uhuru wa kwenda popote na wewe una uhuru wa kwenda popote!
Acha kuwaza kuwa yeye ndo mwanamke bora kwako kuliko wengine...wapo wanawake bora wazuri utawapata kwa kumshirikisha Mungu.
Unachukua muda mwingi mno kumwandikia meseji ,piga chini...piga chini kaa kimya, lakini nakuhakikishia atarudi muda si mrefu na akirudi jitahidi uwe mwanaume kwa kutompa nafasi tena
 
Kama amu alivyosema.
Usiache kumhudumia mtoto.utakachopata wewe mtumie tu kwa ajili ya upendo wa mtoto.
Mtoto mdogo ni gharama sana.
Hata asiposema ahsante wewe mtumie tu.huyo malaika ni damu yako.
Yakimshinda atarudi tu.usiache kumpokea.
Maana mtoto anahitaji malezi yenu wote wawili kwa upendo sana.
Kumpokea yataka moyo ingawa mengine umesema kweli
 
pumbafu sana wewe...tena mpuuzi sana.....huna akili kabisa......mwanamke akikwambia anae mwingine ujue keshazini hata kwenye mawazo tuuu, umemuonyesha nia......bado hakutaki......unasuburu nini hapo......hata mtoto braza kuwa makini.......anaebeba mimba ni mwanamke.....yeye ndie ajuaye kaichukulia kituo kipi.......kuwa makini.....nasema wewe ni pumbafu wa MBUNYE....
 
pumbafu sana wewe...tena mpuuzi sana.....huna akili kabisa......mwanamke akikwambia anae mwingine ujue keshazini hata kwenye mawazo tuuu, umemuonyesha nia......bado hakutaki......unasuburu nini hapo......hata mtoto braza kuwa makini.......anaebeba mimba ni mwanamke.....yeye ndie ajuaye kaichukulia kituo kipi.......kuwa makini.....nasema wewe ni pumbafu wa MBUNYE....
Yaani angekuwa karibu, ningemchapa makofi huyu mvulana
 
Mwanamke ni kichwa cha mwendawazimu. Hapo hajamaanisha chochote anatingisha kibiriti kutaka kuona reaction yako . By the time akili inamrudia ushaoa na mtoto juu. Yeye anabaki kua single mama strong woman.
 
Back
Top Bottom