Nimenunua powerbank feki , msianguke nilipojikwaa

Nimenunua powerbank feki , msianguke nilipojikwaa

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
2,973
Reaction score
8,991
1.jpg

2.jpg

3.jpg

4.jpg

5.jpg

Nimeamua kuweka uzi huu kwasababu hata TBS wanaopaswa kutulinda wamebaki kuwa watazamaji, kuna bidhaa feki nyingi sana mtaani

Kuna bidhaa za kampuni ya ORAIMAB ikiwemo powebank niliyonunua, kaeni nazo mbali.

Sehemu nilipo kumeanza mgao wa umeme, Siku ya jana (Jumanne) nikaingia Facebook kutafuta power bank. Niliona moja ya 10,000mAh kwa bei ya elf 12. Bei ilinipagawisha nilidhani muuzaji kapewa hajui thamani ya kitu anachouza kwasababu bei elekezi ya powerbank za 10000 mAh ni zaidi ya elf 30, Nilimpigia muuzaji, tukakutana nikachukua nikidhani nimeokota embe dodo chini ya mti.

Nikaichaji kwa masaa sita hadi 100%. Asubuhi ya leo umeme ulikatika, nikaiunganisha na simu. Mambo yalianza kunishangaza—charge ikashuka haraka: 100% kwenda 75%, ghafla 50%, ikadrop 25% ikakaa kidogo ikaacha kabisa kuchaji.

Powebank ya 10000 Mah huwa kwa wastani inabidi ichaji simu mara mbili, hii ilichaji simu kwa dakika 23 hivi na simu haikufika hata asilimia 30%.

Cha kusikitisha, niliifuta namba ya muuzaji lakini nilipojaribu kusechi upya nikaona kuna matangazo tofauti tofauti ya power bank kama niliyonunua na nyingine kubwa zaidi za mAH 40,000 na mAH 50,000 zote zinauzwa elf 15
 
View attachment 3434188

View attachment 3434189

View attachment 3434190

View attachment 3434191

View attachment 3434192

Nimeamua kuweka uzi huu kwasababu hata TBS wanaopaswa kutulinda wamebaki kuwa watazamaji, kuna bidhaa feki nyingi sana mtaani

Kuna bidhaa za kampuni ya ORAIMAB ikiwemo powebank niliyonunua, kaeni nazo mbali.

Sehemu nilipo kumekuwa na changamoto ya umeme, Siku ya jana (Jumanne) nikaingia Facebook kutafuta power bank. Niliona moja ya 10,000mAh kwa bei ya elf 12. Bei ilinipagawisha nilidhani muuzaji kapewa hajui thamani ya kitu anachouza kwasababu bei elekezi ya powerbank za 10000 mAh ni zaidi ya elf 30, Nilimpigia muuzaji, tukakutana nikachukua nikidhani nimeokota embe dodo chini ya mti.

Nikaichaji kwa masaa sita hadi 100%. Asubuhi ya leo umeme ulikatika, nikaiunganisha na simu. Mambo yalianza kunishangaza—charge ikashuka haraka: 100% kwenda 75%, ghafla 50%, ikadrop 25% ikakaa kidogo ikaacha kabisa kuchaji.

Powebank ya 10000 Mah huwa kwa wastani inachaji simu mara mbili, hii ilichaji simu kwa dakika 23 hivi na simu haikufika hata asilimia 30%.

Cha kusikitisha, niliifuta namba ya muuzaji lakini nilipojaribu kusechi upya nikaona kuna matangazo tofauti tofauti ya power bank kama niliyonunua na nyingine kubwa zaidi za mAH 40,000 na mAH 50,000 zote zinauzwa elf 15
TBS ipo kwa maslahi binafsi. Haina udhibiti kamili kwa bidhaa mbovu za ndani na za kutoka nje. Bidhaa nyingi za umeme badala ya kutumia shaba sasa ni mwendo wa chuma, au kupaka shaba au brass juu. Ni hatari tupu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom